Tanzania na vifo tata vya watu bila Postmortem Wala kumhusisha Coroner

Tanzania na vifo tata vya watu bila Postmortem Wala kumhusisha Coroner

Hiki kifo kimetokea wakati mbaya sana, ndio maana kimeacha maswali mengi vichwani mwa watu.

Inawezekana kweli sababu ikawa ni hiyo tuliyoambiwa na daktari wake, au pia ikawepo nyingine zaidi ya hiyo, lakini hao wenye jukumu la kufanya huo uchunguzi watafanya hivyo?

Kawaida yao wamezoea kujikausha, hawajihangaishi miaka yote na malalamiko ya aina hii, hasa tukikumbuka vizuri sintofahamu ya aina hii ilianzia kwenye kifo cha Nyerere, ikaja kwa Magufuli, leo kwa Membe, who will be next...

Kwingine kote kifo hospitali ni kimatibabu lakini safari ya mtu haikamiliki bila postmortem na inquest chini ya Coroner. Duniani na hasa kule makwetu Tanzania wauaji ni wengi mno.
 
Hiki kifo kimetokea wakati mbaya sana, ndio maana kimeacha maswali mengi vichwani mwa watu.

Inawezekana kweli sababu ikawa ni hiyo tuliyoambiwa na daktari wake, au pia ikawepo nyingine zaidi ya hiyo, lakini hao wenye jukumu la kufanya huo uchunguzi watafanya hivyo?

Kawaida yao wamezoea kujikausha, hawajihangaishi miaka yote na malalamiko ya aina hii, hasa tukikumbuka vizuri sintofahamu ya aina hii ilianzia kwenye kifo cha Nyerere, ikaja kwa Magufuli, leo kwa Membe, who will be next...
Vifo vya Edward Moringe Sokoine, Horace Kolimba, Julius Nyerere, Benjamin Mkapa, John Magufuli, na Membe ni vifo vinohitaji uchunguzi wa "Coroner".

Hayati Sokoine uchunguzi wake ulifanywa na Dr Shaba na baadae akastaafu, na ripoti ya kisababishi cha kifo cha Nyerere akiwa St Thomas Hospital London itakuwa ilitolewa na imepotezwa.

Kifo cha Horace Kolimba ambae hakujisikia uzuri baada ya kikao cha CC chini ya Mwalimu Nyerere pia kilikuwa na utata.

Hayati Mkapa nae ghafla tu siku moja au mbili baada ya kulazwa akapatwa na umauti na John Magufuli ambae kifo chake bado ni kitendawili pamoja na kuambiwa ni "matatizo ya moyo ya muda mrefu".

Bernard Membe nae hivyohivyo baada ya kuonwa mahala moyo ukapata mgandamizo.

Lakini wengi wasahau vifo kama cha mzee Reginald Mengi ambae nae pamoja na utajiri mkubwa alokuwa nao nae alifikia mahala akashindwa kuzuia nguvu ya mgandamizo wa moyo, kifo chake pia kilihitaji ripoti ya "Coroner" ingawa ni "private" lakini ipo imehifadhiwa.

Lakini vifo vya viongozi wa juu waandamizi wa serikali vyahitaji ripoti ya "Coroner" sawa na ripoti ya CAG kwa sababu ni kwa maslahi ya umma na taifa na pia kuonyesha uwajibikaji wa wale walopewa dhamana ya kulinda afya zao.
 
Back
Top Bottom