Tanzania na vifo tata vya watu bila Postmortem Wala kumhusisha Coroner


Kwingine kote kifo hospitali ni kimatibabu lakini safari ya mtu haikamiliki bila postmortem na inquest chini ya Coroner. Duniani na hasa kule makwetu Tanzania wauaji ni wengi mno.
 
Vifo vya Edward Moringe Sokoine, Horace Kolimba, Julius Nyerere, Benjamin Mkapa, John Magufuli, na Membe ni vifo vinohitaji uchunguzi wa "Coroner".

Hayati Sokoine uchunguzi wake ulifanywa na Dr Shaba na baadae akastaafu, na ripoti ya kisababishi cha kifo cha Nyerere akiwa St Thomas Hospital London itakuwa ilitolewa na imepotezwa.

Kifo cha Horace Kolimba ambae hakujisikia uzuri baada ya kikao cha CC chini ya Mwalimu Nyerere pia kilikuwa na utata.

Hayati Mkapa nae ghafla tu siku moja au mbili baada ya kulazwa akapatwa na umauti na John Magufuli ambae kifo chake bado ni kitendawili pamoja na kuambiwa ni "matatizo ya moyo ya muda mrefu".

Bernard Membe nae hivyohivyo baada ya kuonwa mahala moyo ukapata mgandamizo.

Lakini wengi wasahau vifo kama cha mzee Reginald Mengi ambae nae pamoja na utajiri mkubwa alokuwa nao nae alifikia mahala akashindwa kuzuia nguvu ya mgandamizo wa moyo, kifo chake pia kilihitaji ripoti ya "Coroner" ingawa ni "private" lakini ipo imehifadhiwa.

Lakini vifo vya viongozi wa juu waandamizi wa serikali vyahitaji ripoti ya "Coroner" sawa na ripoti ya CAG kwa sababu ni kwa maslahi ya umma na taifa na pia kuonyesha uwajibikaji wa wale walopewa dhamana ya kulinda afya zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…