Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
660
Reaction score
1,081
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote.

Nini nataka kusema?

Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.

Zaidi, soma: Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.
 
IMG_1033.jpg

Royal bando

IMG_1032.jpg

Mega bando kwa wiki

IMG_1031.jpg

Internet kwa wiki

Kwa mabadiliko haya ya vifurushi kwa nini Waziri Ndugulile asijiudhuru kwa kuudanganya Umma wa Watanzania. Tuliaminishwa kwamba vifurushi vitapatikana kwa gharama nafuu, imekuwa kinyume chake.

Kwa heri Halotel, niliwapenda lkn ndo basi tena. Na jana nimetoka kuwapigia chapuo kuwa mko vizuri, kumbe sikujua masaa machache yajayo ingekuwaje.

Baada ya kutoa yangu moyoni, tujuzane wapi pa kukimbilia kwa sasa.
 
Haya wale walikua wanasema watapandisha bei za internet yamekua, sasa kwa sh 2000 unapata mb 900 na 1000 unapata mb 420.

Hao ni Halotel kifurushi cha siku, wakati vile vifurushi pendwa vya usiku vimepigwa panga.

CCM mbele kwa mbele.
 
😂😂😂😂, dah

Halotel mega bando ya 10k hakuna tena na ile ya 1000 imepigwa panga hatarii. Bando ya youtube 1k kwa 1.2GB haipo tena.

Tusubiri voda hiyo tarehe 2 kama sio 20mb kwa buku sijui😅 na 10k kwa 200mbs sijui.
 
Sasa ni rasmi tumestaafishwa kufuatilia movies, series, tutorials kwa njia ya mtandao.

Bando la usiku limeondoshwa

Halotel hongereni

Upande wa zantel kwa huku Zanzibar

Kutoka GB 3 kwa siku kwa shilingi 2000 hadi mb 900 kwa shilingi 2000

Watu wa Airtel vipi huko?

donor country imekuwa sembe country
 
Mimi hili nilianza kuliona huku voda tangu waliposhusha kifurushi cha jimwage cha wiki kutoka kupewa 4gb kwa 5,000 mpaka 2gb. Namimi katika kujibu mapigo nilichofanya ni ku uninstall instagram with immediate effect!

Sasa hiyo 2gb naitumia jf na whatsapp tu na inabaki! Sasa nasikia hata hiyo ya 2gb kwa 5,000 nayo wanaiona nyingi, wanaifuta sijajua wataleta nini ila niwahakikishie tu na mimi sitakubali, lazima nile nao sahani moja. Kama vipi tunarudi kwenye sms tuu kwani nini bana?
 
haya yale walikua wanasema watapandisha bei za internet yamekua, sasa kwa sh 2000 unapata mb 900 na 1000 unapata mb 420 hao ni haloteli kifurushi cha siku, wakati vile vifurushi pendwa vya usiku vimepigwa panga. CCM mbele kwa mbele


🤔🤔🤔
 
haya yale walikua wanasema watapandisha bei za internet yamekua, sasa kwa sh 2000 unapata mb 900 na 1000 unapata mb 420 hao ni haloteli kifurushi cha siku, wakati vile vifurushi pendwa vya usiku vimepigwa panga. CCM mbele kwa mbele
Weka halo pesa 3000 nunua GB3 dakika 30 na sms ngapi sijui, Halotel wana afadhari,achana na Vodacom hawafai hata kidogo
 
Mimi hili nilianza kuliona huku voda tangu waliposhusha kifurushi cha jimwage cha wiki kutoka kupewa 4gb kwa 5,000 mpaka 2gb. Namimi katika kujibu mapigo nilichofanya ni ku uninstall instagram with immediate effect! Sasa hiyo 2gb naitumia jf na whatsapp tu na inabaki..! Sasa nasikia hata hiyo ya 2gb kwa 5,000 nayo wanaiona nyingi, wanaifuta sijajua wataleta nini ila niwahakikishie tu na mimi sitakubali, lazima nile nao sahani moja. Kama vipi tunarudi kwenye sms tuu kwani nini bana..?
Kama kampango kao ni kutupiga sisi kodi kubwa humu ili wawalipe wasanii tukiangalia nyimbo zao huko youtube sasa nami na natoa youtube,instagram na kila mtandao wenye video online, hii nchi wanaendesha wanavyotaka wao sio wananchi
 
Hii ndio ilikuwa Sera ya magufuli ktk kuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao
Sasa tutabaki wachache online. Kudownload movie itakuwa shida
 
kama kampango kao ni kutupiga sisi kodi kubwa humu ili wawalipe wasanii tukiangalia nyimbo zao huko youtube sasa nami na natoa youtube,instagram na kila mtandao wenye video online, hii nchi wanaendesha wanavyotaka wao sio wananchi
Wanaendesha wanavyotaka wao kwa sababu tumekuwa wavivu kupaza sauti physically tuna kalia kupaza sauti mitandaoni ambapo wanapita na kuzipuuza kama vile hawazioni.
 
Back
Top Bottom