Tanzania na Zanzibar ni vitu wivili tofauti kabisa, yawezekana hata viongozi wetu hawawezi kutofautisha kati ya Tanzania na Zanzibar

Tanzania na Zanzibar ni vitu wivili tofauti kabisa, yawezekana hata viongozi wetu hawawezi kutofautisha kati ya Tanzania na Zanzibar

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kuna neno Tanzania na Kuna neno Zanzibar, haya maneno mawili hayana shida, yako vizuri tu na yanaeleweka ila unapojaribu kuyaweka kwenye sahani moja ndipo utaona utata wake.
Utata usiomithirika.
•Ukifika wakati wa uchaguzi mkuu ndipo utagundua kuwa haya maneno yana utata sana. Kuna watu wanapeleka wabunge ng'ambo ya bahari kulinda maslahi yao huku wengine hawawezi kuvusha hata wajumbe wa nyumba 10 ili wakalinde maslahi yao upande ng'ambo ya bahari.
•Ukiwa mfanyabiashara wa kuvusha bidhaa baina ya Zanzibar na Dar es salaam (Tanzania) ndio utaona haya maneno hayaelezeki na yawezekana hata viongozi wenyewe hawawezi kutofautisha kati ya Tanzania na Zanzibar.
Je, Zanzibar ni nini?
Ni muungano wa Mikoa ya kisiwani yenye mamlaka na Sheria zake?
Kama Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, je, inaruhusiwa mkoa mmoja kuwa na mamlaka yake ya kodi?
 
Usahihi ni Tanganyika na Zanzibar maana hizi mbili ndio zinaunda Tanzania
 
Back
Top Bottom