Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Ndugu yangu Nungwi nimekusoma na sipati shida sasa kuelwa kwamba kumbe wewe ni wakala wa nani. Kinachonisikitisha tena na kule kuendelea kuishushia hadhi JF. Mimi hoja yangu ni rahisi sana: Kwamba hakuna chcochote kinachounga mkono hoja ya kugombea vitambulisho na majadala wako hapa umedhihirisha kwamba hapa vita siyo ID ni urais na ndiyo maana sasa umeamua kuwa wazi kueleza kwamba Membe hafai kuwa rais na kwa nini. Lakini huko ni kupoteza muda bure kujadili kitu ambacho yeye mwenyewe amekwishasema kwamba hana mpango nacho. Whether sababu za kusema hana mpango nacho ni sababu ulizzotoa au sababu nyingine hatujui lakini ni vema ukajua kwamba unapigia kelele na unakerwa na kitu ambacho yeye si mshindani.
Ndugu yangu naomba nikuarifu kwamba fikra kwamba Mbopo ni Membe ni case ya mistaken identity. Mbopo ni Mbopo na wala si Membe na kwa hiyo kama wewe una ugomvi naye basi unayemtukana humu si Membe. Narudia tena kwamba hoja na tuhuma za ugomvi wa ID ilichochewa na hofu ya urais tu na si vinginevyo. lakini pia ninaomba nikuonye hapa kwamba wewe kama mtu msomi na mwenye utashi kwamba hoja haiwi bora kwa kumtukana mtu au kumvunjia mtu heshiam yake. Mimi kama mfuatiliaji wa mijadala mbalimbali ya JF nimeona kwamba hoja zilizoshinda ni zile ambazo mijadala yake ilikuwa ya kistaarabu na yenye ushahidi makini na si kukurupuka kwa ajili ya kulipa deni ya kutumiwa kama mpambe. Simfahamu sana Membe na sihitaji yeye kunifahamu kuweza kujua kwamba hapa anpigwa vita kwa vitu visivyo vyake.Kwanza hata huo mradi wenyewe kandarasi yake haijatolewa.
Ndugu yangu, mimi nakushauri ufuate mfano wa watu kama mwanakijiji ambaye hushusha hoja zake bils jazba na huchukua muda kutafiti kila anachopanga kusema na ndiyo maana nyingi ya hoja zake huenda hata kwenye magazeti na kusisimua wasomaji. Ukweli unabaki palepale kwamba mzee unalazimisha hoja na kila anyejaribu kuwa objective kama mimi na Masatu tunakoga matusi na kashfa zako mzee. NARUDIA KUSEMA MZEE MMECHEMSHA NA SASA HOJA IKO WAZI, NI URAIS NA HOFU YA WALIOKUTUMA. LAKINI WAAMBIE WASIHOFU, MEMBE HAYUKO KWENYE RACE, WALALE TU VIZURI MZEE.
Matusi sidhani kwamba ni majibu ya hoja bali nayachukulia kama Ubabe ambao Sitta anatuletea Tanzania na baadhi ya wana CCM kama Ditopile mbabbe na analindwa na serikali ya Kibabe.
Mbopo naona na wewe umeingia katika mkumbo wa one on one attack ama majibizano na name calling . Mtoa hoja ama leta hoja ni GT. This guy huwa naamini ni smart sana . Narudia kuomba tena.
Popote ulipo GT jitokeze Mbopo kawaka na kutangaza ushindi .Hoja ni ID na fraud yake .Urais si hoja ila mawazo ya watu kama wanavyo zipata habari hizi .Hili ndilo kubwa hapa.
ID tunazitaka sana ama waache kila Mtanzania apewe PP ambazo tayari zipo si not a big deal lakini sasa mgogoro wa nani apewe tenda ama kaanza kuhangaika na tenda bado si issue ila issue itakuwa pale kwamba billions of money ya walala hoi.
Hilo ndilo nadhani limemsukuma GT kuleta hoja kuwa alert kwamba we are watching na kwangu si Urais wa Membe wala nini ila namna mwisho wa siku hizo ID zitakavyo tugharimu.
Now your part I think is over kwamba umesha tetea kwamba Membe hayuko katika huo mpango na Urais ni mawazo ya mtu . Let us now wait and see