KAMA kawaida yake mzee wa majungu bwana MEMBE ameanza kumkomalia LOWASSA kwa kutumia gazeti la Tanzania Daima ambalo huwa analitumia mara kwa mara kupitishia majungu yangu yake na fitina kwa wenzake.
hivi karibuni lilipovunjwa baraza la mawaziri Tanzania Daima liliandika sana kuwa Membe ni bora arudi kwenye wizara yake ya mambo ya nje ili anedeleze kazi aliyoianza. hakutajwa waziri yeyote zaidi ya Membe.
alipoteuliwa Asha rose Migiro kuwa katibu mkuu gazeti hili lilimuandika sana kuwa Membe ndiye anayefaa wizara ya mambo ya nje kwani ana uzoefu na elimu ya mambo ya diplomasia. wakati huo Membe ni naibu waziri tu tena kwa miezi kama kumi tu, jee uzoefu kautoa wapi?
hawakutajwa watu kama Dr.Mwakyembe au Dr.Ibrahim Msabaha ambaye ni mtaalam wa diplomasia amewahi kuwa mkuu wa chuo cha diplomasia na kuwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na pia elimu yake hadi phd ni mambo ya Diplomasia na wengine wengi ambao ni wabunge wamewahi kuwa mabalozi.
Membe amekuwa na urafiki wa karibu na Balile ambaye kwa sasa ni mhariri wa Mtanzania na alikuwa mhariri mkuu wa Tanzania Daima kwa muda mrefu na amekuwa akiongozana nae sana Membe.nimewahi kuandika thread ya Balile acha kujipendekeza kwa Membe kwenye hii forum hii.
yaliyoandikwa na Tanzania Daima la leo ni makala ya Membe ana vunja nguvu za Lowassa kwa ajili ya urais 2015.kwenye Tanzania Daima la leo kuna makala mbili za kumponda Lowassa na urais ingine inasema Lowassa usijifananishe na Mzee Mwinyi.
Membe tunajua jinsi ulivyompora kiwanja yule mama pale Tangi bovu-mbezi beach jee hiyo haki?
haya hapa maneno ya MEMBE dhidi ya Lowassa.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/2/habari2.php
Bwana Membe suala hili tumekusikia siku nyingi ukimsema Lowassa kuwa ana hekari elfu tatu za ranchi ya Taifa-Tanga na unazusha kuwa kachukuwa kinguvu.
Lowassa mchawi wako ni huyu bwana Joti.