Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)


izihaka umenikuna mpaka nimezinduka toka usingizini na kukumbuka nikiwa pale mlimani huyo Kyaruzi aliyetajwa kama mshauri wa serikali katika vitambulisho hivyo ni yule aliyekuwa na mgogoro na chuo cha uholanzi kwa kujiita Dr wakati hakumaliza phd yake na sio hivyo tu, alikiingiza chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) katika mradi kama huo wa smart card kwa wanafunzi ambao mpaka leo hii hauna kichwa wala miguu.

Ukiona hizo smart card ndugu yangu utashangaa ni jinsi gani huyoi mtu alivyo fisadi tena kweupeeee mpaka chuo kilimpa deadline la sivyo watamfukuza kazi. Alibahatika kupata kazi pale TIC japo uwezo wake na uzalendo ni mdogo!

Huyu atakuwa chanzo cha huo mradi na maimu ambaye ni rafiki yake mkubwa katika swala zima la ufisadi. Kyaruzi anaelekea kuwa na sifa kama za Maimu katika ufisadi kwani wote walishawahi kufoji elimu zao Kyaruzi (PHD) na Maimu (Masters).

JK huo ni mkenge mwingine unaingizwa shimoni nao,na this time WE WONT FORGIVE YOU'
 
Mimi nakumbuka mradi flani hivi wa "speed governers". Huwa nacheka mpaka leo. Sijui tutaamka lini jamani.
 
Huu Mradi kama tuna akili , ni vizuri ufanywe na Wa Tz if Possible Chuo Kikuuu Kipewa, ili kwanza kukuza elimu yetu na hii pesa ikilipwa bongo itasaidia maendeleo Mengine.

Jingine Mradi huu ufanyiwe tathmini zaidi na Wataalamu kuliko Wanasiasa. Tatu uwe chini ya Wizara ya Mambo Ya Ndani, mambo ya nje na vitambulisho vya taifa wapi na wapi?
 
Lisemwalo Lipo Au Laja Kwa Mujibu Wa Waswahili.
Mwikalo Na Mbopo Walikuwa Wakibisha Nini? Mwikalo Si Mmarekani Kaingiaje Humu?
 

KAKA MADA YA LOWASSA IPO INAYOJITEGEMEA NAONA HAPA HUJACHANGIA ZAIDI YA KUTOA HASIRA ZAKO KWA LOWASSA AMBAYE TUMEMSULUBU SANA KWENYE THREAD NYINGI, WEWE HUKUJA MBIO KAMA HAPA. AU MKUU NAWE NI SEHEMU YA HII DEAL YA VITAMBULISHO? INAONESHA KAMA UNA INTEREST KWENYE MRADI HUU.
 
Huu Mradi kama tuna akili , ni vizuri ufanywe na Wa Tz if Possible Chuo Kikuuu Kipewa, ili kwanza kukuza elimu yetu na hii pesa ikilipwa bongo itasaidia maendeleo Mengine.
Jingine Mradi huu ufanyiwe tathmini zaidi na Wataalamu kuliko Wanasiasa. Tatu uwe chini ya Wizara ya Mambo Ya Ndani, mambo ya nje na vitambulisho vya taifa wapi na wapi?

MRADI WA VITAMBULISHO UPO CHINI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI. KUNA TIMU MBILI ZILIPEWA JUKUMU LA KUANDAA TATHMINI YA MRADI, NAO NI: GOTHAM INTERNATIONAL LTD NA ECONOMIC RESEARCH BUREAU YA UDSM WAKISHIRIKIANA NA NATIONAL BUREAU OF STATISTICS. GOTHAM INTERNATIONAL WALIPENDEKEZA TECHNOLOGY YA SMARTCARD NA ERB/NBS WALIPENDEKEZA BARCODE. SERIKALI ILIPITISHA REPORT YA GOTHAM INTERNATIONAL. TATHMINI YA MRADI WA ID INA MAENEO MAKUWA YAFUATAYO: HALI YA KISIASA, KIUCHUMI, KIUTAMADUNI, KITEKNOLOGIA NA KIUSALAMA. REPORT YA GOTHAM IMEELEZEA VIZURI SANA MAENEO YOTE HAYO. HII NI KWA TAARIFA TU.
 

KAKA TUNAJUA UKO KWA MBOPO (MEMBE) MAMBO YENU SAFI ALIYOYATAKA MEMBE YAMEKUWA. KAPATA TENDA YA VITAMBULISHO TULILISEMA MAPEMA HILI. KAPATA PESA YA KAMPENI YA URAIS 2015.
 
Ndg yangu Mtalii, si kweli hayo uyasemayo. Kuna upotoshwaji MKUBWA sana wa taarifa za kweli ktk mradi huu. Watu wengi wanatizama namna ya kula tu. Si muda mrefu ukweli utawekwa wazi na watu watajua nini kilichokuwa kinafichwa. Tusubiri.
 
KAKA TUNAJUA UKO KWA MBOPO (MEMBE) MAMBO YENU SAFI ALIYOYATAKA MEMBE YAMEKUWA. KAPATA TENDA YA VITAMBULISHO TULILISEMA MAPEMA HILI. KAPATA PESA YA KAMPENI YA URAIS 2015.

Tatizo humu ndani kuna watu kazi yenu ni kutengeneza majungu tu. Mkijibiwa mnakuja na propaganda zenu za kutaka kutishana etu tunakujua. Kama kuna uzushi mkubwa ni kumhusisha membe na suala la vitambulisho. Ukaribu wake na baadhi ya wahusika wa mradi huu na haswa GOTHAM International ni ujinga na jungu lisilo na kiwango.

Ushindani wenu kisiasa unataka kutumika kuvuruga kila mpango wa nchi hii halafu baadaye mnalia na kukosekana na maendeleo na amani. Mkiambiwa ukweli mnaanza kutoa vitisho eti tunakujua mkidhani kuna watu wanawaogopa wakati hakika mnabaki kuwa vijibwa koko vinavyobwekea nje ya uzio wa nyumba. Mnaboaaaaaaa

Kama kweli mnabweka kwa manufaa ya nchi ni bora mkawa tayari kufuatilia taarifa zote za mradi huu na mingine kwa usahihi wake na sio kula na kulishana sumu kama mnavyoendelea.

Na wale wapambe wa fisadi Richimonduli na kikampuni chake feki na wengine wanaonyemela mradi huu bila ya kukubali yaishe wasubiri dharuba inayokuja soon.....pale mchele na pumba zitakapotenganishwa na ukweli utakapojulikana.

Tanzanianjema
 

Ndugu yangu KINVABA nafikiri wewe ni mtu mzima, naposema utekelezwe na wa tanzania , si maanishi kampuni iwe kama Mambo ya RICHMONDULI, so GOTHAM INTERNATIONAL ni ya akina nani???
MAAna mradi wowote TZ lazima uingize share holders wa kitanzania, sasa wether GOTHAM Nchinga au INTERNATIONAL, suala hiyo kampuni ni kweli ya KItanzania that is ONe, pili INauwezo?

MAana hi context ya kuwemo Wa tanzania au iwe ya kitanzania huwa inatumika vibaya, kwanini isiwe idara ya serekali yenye wa tanzania Ndani yake moja kwa moja badala ya kusema ni Kampuni ya Kitanzania in Quote , wakati dhana na madhumuni yake no tofauti?

tumeona NETGROUP tuliwaweka mashemeji zetu, IPTL alikuwemo au Yupo Rugemalila, tuna akina AGREKO, ARTUMAS etc.

Na ukumbuke hapo mwanzo kuna SOFT ya Kenya ilisha kunywa hizo hela za Mradi.
 
Vitambulisho vya uraia, ufisadi unaopikwa

Mwandishi Wetu Mei 21, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

MRADI mkubwa wa Vitambulisho vya Taifa bado umegubikwa na utata, huku kukiwa na sura dhahiri ya ukosefu wa uwazi na hata kuonekana ni kinyanganyiro cha ulaji.

Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, akitangaza kuwa zabuni ya mradi huo itatangazwa kabla ya mwisho wa wiki hii, tayari ofisi ya mradi huo ipo na inafanya kazi na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) ameteuliwa.

Masha anasema: Ninachofahamu mimi ni kwamba tutatangaza tenda kabla ya mwisho wa wiki. Tutatangaza kwa uwazi kabisa.

Raia Mwema ilipowasiliana na maofisa wa Idara ya Uhamiaji, iliambiwa tayari ofisi ya mradi huo ipo Kinondoni, Dar es Salaam, na CEO wake anaitwa Dicksom Maimu.

Taarifa zilizopatikana zinahoji kuwapo kwa ofisi hiyo, inayofanya kazi, huku zabuni ikiwa haijatangazwa, ikiwa ni kukinzana na Sheria ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPAA).

Kwa kawaida sheria inataka taasisi ya umma, katika serikali kuu, iwe na bodi ya zabuni pamoja na vitengo vya manunuzi. Kama kuna ofisi au taasisi ya Serikali inakwenda kinyume na utaratibu huo, basi ni uvunjaji wa sheria, alisema ofisa mmoja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).

Kwa mujibu wa ofisa huyo, Sheria ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma inaitaka taasisi ya umma kuwa na bodi ya zabuni yenye wajumbe wanane, ingawa inalegeza masharti kuwa idadi hiyo yaweza kupungua kulingana na udogo wa taasisi.

Raia Mwema iliwasiliana na maofisa wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kuhusu uadilifu kwa maofisa wa serikali kushiriki kwenye utafiti wa mradi kisha hao hao ama wakawa washauri wa kampuni zinazoshiriki kwenye zabuni, au wakakabidhiwa madaraka kwenye taasisi inayozaliwa kutokana na utafiti huo.

Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kama kuna uvunjivu wa maadili kama huo, maofisa wa PPRA wanapaswa kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko yanayohusu zabuni au manunuzi.

Kwa msingi huo, mimi ninadhani kama kuna watu walishiriki katika kufanya utafiti na halafu wakakabidhiwa mikoba ya kuendesha taasisi waliyoifanyia upembuzi yakinifu, hiyo itakuwa ni kashfa. PPRA wanapaswa kufanya uchunguzi, anasema ofisa huyo.

Mradi huo unaonekana kuwa lulu ya thamani kubwa.Tangu mwanzo ulikuwa unasimamiwa na maofisa wa serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Rais (Utumishi), kama washauri, ambao sasa tayari wamelipwa kutokana na kazi yao.

Gharama za sasa za mradi huo zinakadiriwa kufikia Sh. Bilioni 250, zikiwa zimekua kutoka Sh. bilioni 152 za makisio ya awali, ambazo zinakifanya kitambulisho hicho kuwa ghali kuliko hata kile cha nchi zilizoendelea kama Sweden.

Lakini pia mradi unaonekana kama kinyanganyiro cha ulaji fedha kwa kuwa baadhi ya watendaji walishiriki katika kufanya upembuzi yakinifu wa mradi, na ndio hao hao sasa wameshika hatamu katika mradi huo.

Raia Mwema imedokezwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mradi, Dickson Maimu, alishiriki hatua za awali za maandalizi ya mradi, kisha akateuliwa kuingia katika nafasi hiyo ya juu ya mradi, jambo ambalo linatia shaka.

Mradi wa Vitambulisho vya taifa umekuwa ukipita katika hatua za kuiva na kufifia, kwa kuwa zabuni ziliwahi kushindaniwa, washindi wakapatikana, lakini hazikutangazwa hadharani, ikiwamo kampuni mmoja kutoka Malaysia.

Miaka takribani 10 iliyopita, kampuni kutoka Malaysia ilishinda zabuni ya utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa, lakini zoezi zima halikutangazwa kwa umma.

Raia Mwema ilipowasiliana na Masha kuhusu uwezekano wa kampuni hiyo ya Malaysia kwenda mahakamani endapo mshindi mwingine wa zabuni atatangazwa, alisema tayari Serikali ilishitakiwa baada ya kuvunja mkataba na kampuni hiyo.

Serikali ilivunja mkataba, kampuni ikaishitaki serikali mahakamani. Law firm yangu ikaitetea ile kampuni na tukashinda kesi, anasema Masha ambaye sasa wizara yake ndiyo msimamizi mkuu wa mradi huo.

Lakini pia mradi huo umekuwa na hitilafu nyingine, kwa maana vitambulisho ambavyo vitapatikana vitakuwa na gharama kubwa wakati vikiwa na taarifa chache ndani yake.

Taarifa zinasema kwamba mradi huo wa fedha nyingi umekuwa ukigombewa na wakubwa: Mambo ya Ndani; Mambo ya Nje; Ofisi ya Waziri Mkuu na ulibuniwa na wajiriwa serikalini na kisha kampuni yao ya Gotham International ikapewa kazi ya upembuzi na hatimaye ikaandaa mchanganuo.

Kati ya waajiriwa hao wa serikali walikuwamo Jack Gotham mwenye uhusiano wa karibu na viongozi wengi serikalini na John Kyaruzi mwajiriwa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambaye ameelezwa kuwa ndiye aliyevuta kampuni moja ya Afrika Kusini, Business Connection (Bcx) kuunda timu ya Gotham International.

Vitambulisho hivyo vilikuwa vianze kutoka kabla ya mwaka ujao, lakini sasa baada ya utata huo baadhi ya wataalamu wa masuala hayo wanaona kuwa hakuna haja tena ya kuwa navyo kama havihusishi pamoja na mambo mengine, kama takwimu muhimu za wapiga kura.

Hicho kitambulisho kinachotafutwa kwanza ni ghali sana mpaka hata Benki ya Dunia ilihoji kama Tanzania inahitaji kitu ghali kama hicho.

Lakini pia sasa Tume ya Uchaguzi inapitia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ungetarajia kitambulisho hicho kiwe na taarifa zote hizo, lakini sasa Serikali inataka kuwa na utambulisho wake na Tume ya Uchaguzi nayo utambulisho wake, hii haileti maana, anasema mtaalamu mmoja wa takwimu.
 
hakuna haja ya kuwa na serikali,na hivi wabunge wetu vilaza basi ndio kabisaaaa
 
Hakuna ulazima wa vitambulisho vya nchi nzima kutengenezwa na kampuni moja.

Kila halmashauri za miji na wilaya zinaweza kutengezena zitambulisho vya wakazi wake.Kazi ya wizara iwe ni kuhakiki viwango katika zoezi hilo.


Mfumo unaotaka kutumika sasa sio tu unaingiza gharama kubwa serikali na kufungua mianya ya ubadhilifu bali pia inachochea urasimu katika zoezi zima la usambazaji, Kazi ambayo ingeweza kufanyika kwa miezi miwili itachukua miaka miwili.

lets get to work.
 
MEMBE MAMBO YAKE TAMBARARE

SASA HEBU NIAMBIENI...HUYU ANATAKA KUWA RAIS...NA TAYARI ANANUKA UFISADI...


ZAIDI SOMA HAPA:
http://www.raiamwema.co.tz/08/05/21/3.php
 
RAIA MWEMA linaendelea kukamua kwa kusema hivi:


http://www.raiamwema.co.tz/08/03/12/3.php
 
He he ngoja nianze kupiga mluzi sasa!!! Naona mambo yanaiva.

GT unafikiria bado kuna ushindani kati ya Membe na Lowassa? Maana from nyepesi nyepesi (msinishike shati, siwezi kuweka maelezo zaidi) ni kuwa Membe ndio amekuwa kipenzi cha Muungwana siku hizi.
 
Maana from nyepesi nyepesi(msinishike shati, siwezi kuweka maelezo zaidi) ni kuwa Membe ndio amekuwa kipenzi cha Muungwana siku hizi.

WHAAAAAAAAT!
 
WHAAAAAAAAT!

Huna habari? kajini tatizo la Membe ni njaa..na kama ujuavyo MONEY TALK PEOPLE LISTEN ...ndio maana Membe anapush huu mradi wa ID kama hana akili vizuri vile..in short Membe keshaanza ufisadi urais hajaupata
 
Game Theory,
Tofauti na ulivyofikiria, mimi nijuavyo Membe ni mshikaji wa JK toka zamani sana sio sasa hivi, isipokuwa nachoshindwa kuchangia mada hii ni kwa sababu namjua Membe kuwa ni mtu mwenye msimamo, clean na kiongozi bora.

Kwa hiyo hizi habari za tender kidogo ni kahawa ya asubuhi kunitoa usingizi pamoja na kwamba bado siamini.
 
28th January 2008, 02:03 AM

THATS THE DATE NILIYOWEKA HII THREAD...NIKAULIZWA MWIKALO NIMEMJUAJE ...MZEE BADO HATUJAFIKA SEPT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…