Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
...ten are too many!! Only one with supportive argument as to how will improve well-being of poor Tanzanians who majority couldn't afford two meals a day or go India for treatment!can you please give me 10 reasons why Tanzania need to have national ID CARD at this moment?
Huu ni upuuzi! Kama tunashindwa ku'control' pasipoti zetu ambazo zinagawanywa kwa wachache itakuwa hivyo vitambulisho ambavyo hata mwanakijiji wa Matombo nae atatakiwa apate! Kwanza, tujiulize, huyo mwanakijiji, hicho kitambulisho kina msaada gani kwake kama sio kumuongezea gharama na ukiritimba (tukumbuke vitambulisho sio vya daima, itabidi kila baada ya muda apate vipya) katika maisha yake? Atakipataje, yeye na familia yake? Si itabidi aende mji wa karibu kuvifuata na kupiga picha! Halafu baadae wababe wa huko (madc n.k.) nao watageuza mradi kwa kufanya sachi kwa kila asiye na kitabulisho! Tuna matatizo mengi na hatuhitaji kupotezeana wakati kwenye miradi hii ya alinacha!
Nafahamu kuwa zabuni haijatolewa isipokuwa ndiyo kwanza imetangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nafahamu kuwa hadi sasa kuna washauri walioteuliwa bila kupitia mkondo wa zabuni kwa vigezo vya usalama.Nimepata tetesi kwamba zabuni ya kutengeneza na kusambaza vitambulisho vya kitaifa imetolewa kimizengwe.
Je, kuna mwenye taarifa juu ya tuhuma hizi?
Zabuni imetolewa kwa nani (kampuni gani)?
Nani aliyehakikisha watu hao wanapewa?
Je, waliopewa wana uwezo wa kutimiza masharti hayo?
Tafadhali, mwenye taarifa kuhusu haya awasiliane nami kutumia Ujumbe Binafsi (Private Message).
P.S. Hizi taarifa ni nyeti sana, na ni za hatari. Anaweza kuondoka mtu hapa!
Nafahamu kuwa zabuni haijatolewa isipokuwa ndiyo kwanza imetangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nafahamu kuwa hadi sasa kuna washauri walioteuliwa bila kupitia mkondo wa zabuni kwa vigezo vya usalama. Hawa consultants ni Gotham International Ltd. Nafahamu pia kuwa hata zabuni ilikuwa isitangazwe kwa vigezo hivyo hivyo vya usalama kutokana na unyeti wa kazi yenyewe ya kuandaa taarifa za nani apewe kitambulisho. Katika kuwaajiri washauri hao bila shaka Muungwana alibariki kwa sababu hizo za usalama.
Critics bwana! Yaani wao kila kitu ni kupinga tu. Labda tulaumu mfumo uliotulea na kutujenga kuogopa mabadiliko. Hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya umasikini wetu. TUNAOGOPA MABADILIKO!
Hapa nakumbuka story moja ya miaka ya nyuma kipindi Mrema akiwa NCCR-Mageuzi. Kipindi hicho huyu bwana alikuwa maarufu kweli hasa kwa walalahoi. Sasa, kuna mradi ulikuwa wa kupanua ile barabara ya Morogoro (Morogoro Road), na eneo la kuanzia Ubungo kuelekea Kimara ilibidi njia ipanuliwe sana ili kupisha ujenzi wa "double roads". Upanuzi huu ulihusisha ubomoaji wa nyumba za watu na sehemu za biashara. Wananchi walikuja juu kweli. Mzee wa Kiraracha aklivalia njuga hasa. Watu wakenda hadi kulala kwenye ofisi za NCCR. Lakini serikali kuu ikawa ngangari, nyumba zikabomolewa na barabara ikajengwa. Leo tunapita Ubungo (japokuwa kuna foleni kidogo) kwa amani na raha mustarehe.
Wadau tuwe tayari kukubali mabadiliko. As long as kwamba yatakuwa na faida kwetu. Sio kila kitu tunashabikia tu bila sababu za msingi.
Na salva Rweyemamu naye atapewa kitambulisho cha Uraia????