Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

lakini World Bank wameuliza kwa nini serikali yetu inangangani hii project?

ninachotaka kusema kuwa sisi hatuna track record nzuri na hizi projects kuanzia ubinasishaji wa DAWASA mapka RICHMOND

trust me my brother 5 years from now kama JF itakuwa bado ipo utakuja niambia kuwa if we only knew back then.

Hii siyo project ya mwaka mmoja ni project ya miaka 5 na inaendelea hivyo ulaji upo kila mwaka na kutokana na serikali ya JK ilivyo incompetent i am sure 100% haiwezi ku pull it off

watch this space
 
GT,
World bank wamehoji gharama za vitambulisho hivyo hapo sielewi wao wamependekeza vitambulisho gani na kwa gharama gani badala ya hivyo vilivyochaguliwa..Pili, WB siku zote wamekuwa against miradi ambayo haihusiani na uwekeshaji wa makampuni yao makubwa nchini.

Mara zote hupenda miradi ambayo inahusiana sana na Miundombinu, iwe mawasiliano, Umeme, Umeme, Maji, Madini, Mafuta, reli Ndege na kadhalika lakini miradi kama hii huwa ni haina hakika ya kurudisha fedha yao kupitia njia mbili yaani sisi kulipia interest deni lao na ile kampuni ya Ulaya kuendeleza kujenga uchumi wa nchi kubwa.

Hivyo mkuu WB ni kiungo cha haya mataifa makubwa kuweka koloni la kiuchumi Afrika na ndio maana wamegawana tayari nchi zetu..Ndio maana walipata taabu sana wakati wa Mwalimu hadi ikafikia wakati wakasema hawatatoa tena mkopo..

Tatu, Unajua tena wazungu mahesabu yao!..Wanatuona sisi kama pori mbugani hivyo mtazamo wao kuna kila haja ya kuwa na vitambulisho Ulaya ambako hata mbwa, Paka, ngombe wana vitambulisho wengine hata majina wamepewa lakini Afrika haiwaingii akilini kama wanyama wetu wanavyoranda ovyo Ngorongoro... kweli unaweza kuwawekea vitambulisho?.. maaanake kwa macho yao sisi hatuna tofauti kubwa na wanyama hao.

Ebu fikiria mradi wa kuwapa Nyumbu wa Serengeti vitambulisho sii kazi mpya hiyo, huu ndio mtazamo wao mkuu amini maneno yangu kuna mengi hawa jamaa wanatudharau kiasi kwamba hata tatizo hili la chakula duniani wapo wanaosema Afrika hatuhitaji chakula kwa sababu tumeshazoea kushinda njaa! hatufahamu nini maana ya upungufu wa chakula ati hakijawahi kuwepo..
 
mkandara

you are still hitting around the bush

can you please give me 10 reasons why Tanzania need to have national ID CARD at this moment?

I am ready to take notes

6jafyps.jpg
 
can you please give me 10 reasons why Tanzania need to have national ID CARD at this moment?
...ten are too many!! Only one with supportive argument as to how will improve well-being of poor Tanzanians who majority couldn't afford two meals a day or go India for treatment!
 
Watoto wetu wengi wanasoma kwenye madarasa yaliyoezekwa kwa nyasi; tena wanakaa sakafuni kabisa kwenye vumbi! Zahanati vijijini hakuna kitu; Majengo ya Mahakama za Mwanzo na nyumba za Mahakimu hakuna au ni mbovu sana; Maji ni tatizo kila mahali; barabara vijijini na mijini ni balaa tupu.
Tanzania HATUNA KABISA VIPAUMBELE vyetu kama NCHI? Mahitaji ya watu wetu kwa sasa ni vitambulisho hivi kweli?

Mradi huu hauna tofauti na mingine mibovu tuliowahi kuwa nayo kama RADA, NDEGE YA RAIS, JENGO LA KIANASA LA BUNGE, MINARA PACHA YA BOT,..., na mingine mingi ambayo haiendani na hali halisi ya uwezo wetu wa KIUCHUMI. Tutakuja sutwa siku moja!

Hivi tunaathirika nini kwa kutokuwa navyo vitambulisho hivi? Mbona Watanzania hatuhurumiani katika hali tuliomo sasa? Kama ni kura ya MAONI hili la VITAMBULISHO ndio la kupigiwa hasa.
 
GT,
Kwanza huduma zote zinazohitajika kwa mwananchi raia zitatolewa kwa ufasaha zaidi na record zake zitakuwepo.

Vitambulisho vinarahisisha kazi zote za serikali ikiwa ni pamoja na vibali, kazi, kodi pia kutofautisha ktk utoaji na uingizaji mali nchini kwa mwananchi na mgeni. Wapo wageni wengi wanaofaidika na uhuni wa kifisadi kudai Uraia wa karatasi wanapoingiza mali ama kutoa, wanapoomba vibali ama viwanja, kupata kazi, kufungua miradi ya biashara na kadhalika..kumbuka vyote hivi vina tofauti zake kubwa kati ya raia na mtu asiyekuwa raia hivyo kupunga pato la taifa na nafasi raia wake.

Kisha TZ sio nchi isipo kuwa na mwenyeji, lakini utamtambua vipi mwenyeji kama hakuna vitambulisho ama ndio huo mtindo wa South Afrika kuua watu kutokana na sura zao. Vipi nasi kwa njia nzuri tukitaka kila mkimbizi arudi kwao tutaweza vipi kuwatambua ikiwa sisi wenyewe hatuna vitambulisho!

Ni moja ya njia kuu za kufanikisha ukusanyaji kodi na utoaji huduma kwa wananchi.. sasa hapo mkuu unaweza kuweka huduma zote utakazo fikiria wewe ambazo ni haki yako kama mwananchi.. hata kama tukitaka kuanzisha huduma nyingine mpya.

Kama nilivyokwisha sema Passport na driver's licence haviwezi kutumika kwa sababu sio lazima kwa mwananchi kuwa navyo! zaidi ya hapo ni asilimia chini ya moja wenye passport ama uwezo wa kusafiri na pia ni asilimia chini ya 10 wenye ujuzi wa kuendesha magari hivyo vitu hivi usivihesabu isipokuwa tunachosema sisi ni kwamba kuna kila haja ya kuwa na kitambulisho kwa kila raia.

Unachojaribu kuuliza hapa ni sawa na kuniuliza nikupe sababu KUMI kwa nini kila mtu duniani ana jina lake!..sielwi unachotaka nijibu zaidi ya hayo hapo juu...
 
Mradi wa vitambulisho uliisha omgelewa sana na kupitishwa ndio sababu nikaanzisha mada ya Tenda ambayo kuna fununu kwamba Membe and Co. wanaubia wa kuipata. Tatizo hapa sio ID cards bali ni kuwa na washabiki wenye upeo mdogo ambao hawawezi kuchanganua na kuona dunia inakwenda wapi.

Leo hii huwezi kusema usinunue computer au simu ya mobile kwa sababu ni ghali ni afadhali upande punda kwenda kupeleka ujumbe. Lets go with time na hawa wanaogawana tenda kinyemela tuwashughulikie na kuona kwamba swala hili linafanyika kwa uwazi. Ingekuwa hivyo basi hata passport zisitolewe maana ni ghali. JF members wegine (GT) wamesema tayari wenyewe wana usongo na Membe sasa utawezaje kuanza kujadili swala la kitaifa wakati unaingiza ubinafsi.

Hata tukikoroma hapa kama chura hiyo ndio imetoka tuone kwamba hii Tenda inatolewa kwa anayestahili na kutengeneza hizo ID ambazo hazizidi 40 million na tuone gharama ambayo inakubalika kwenye world makert. Baada ya hapo ni kiasi kidogo sana kila mwaka kutokana na jinsi tunavyoongezeka.
 
Naona cronies wa Membe wamemkalia GT kooni lol...
 
Mkuu tafadhali sana mimi sio crony wa Membe Tuheshimiane.. Naona sasa umeota vijidevu vya mbuzi unaona unaweza sema ovyo.

Nachozungumzia ni ID card ambazo zimepitishwa kabla hata Membe hajapewa wadhifa huu aliokuwa nao. Swala hapa ni umuhimu wa ID card, hayo ya MEMBE na deal na kama yapo tuyazungumze nje ya Umuhimu wa hizi card.

Kama anapewa tenda yeye leteni facts, hata mimi nitakuwa nanyi katika hili...
 
Huu ni upuuzi! Kama tunashindwa ku'control' pasipoti zetu ambazo zinagawanywa kwa wachache itakuwa hivyo vitambulisho ambavyo hata mwanakijiji wa Matombo nae atatakiwa apate!

Kwanza, tujiulize, huyo mwanakijiji, hicho kitambulisho kina msaada gani kwake kama sio kumuongezea gharama na ukiritimba (tukumbuke vitambulisho sio vya daima, itabidi kila baada ya muda apate vipya) katika maisha yake?

Atakipataje, yeye na familia yake? Si itabidi aende mji wa karibu kuvifuata na kupiga picha! Halafu baadae wababe wa huko (madc n.k.) nao watageuza mradi kwa kufanya sachi kwa kila asiye na kitabulisho!

Tuna matatizo mengi na hatuhitaji kupotezeana wakati kwenye miradi hii ya alinacha![/FONT]
 
Huu ni upuuzi! Kama tunashindwa ku'control' pasipoti zetu ambazo zinagawanywa kwa wachache itakuwa hivyo vitambulisho ambavyo hata mwanakijiji wa Matombo nae atatakiwa apate! Kwanza, tujiulize, huyo mwanakijiji, hicho kitambulisho kina msaada gani kwake kama sio kumuongezea gharama na ukiritimba (tukumbuke vitambulisho sio vya daima, itabidi kila baada ya muda apate vipya) katika maisha yake? Atakipataje, yeye na familia yake? Si itabidi aende mji wa karibu kuvifuata na kupiga picha! Halafu baadae wababe wa huko (madc n.k.) nao watageuza mradi kwa kufanya sachi kwa kila asiye na kitabulisho! Tuna matatizo mengi na hatuhitaji kupotezeana wakati kwenye miradi hii ya alinacha!

Critics bwana! Yaani wao kila kitu ni kupinga tu. Labda tulaumu mfumo uliotulea na kutujenga kuogopa mabadiliko. Hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya umasikini wetu. TUNAOGOPA MABADILIKO!

Hapa nakumbuka story moja ya miaka ya nyuma kipindi Mrema akiwa NCCR-Mageuzi. Kipindi hicho huyu bwana alikuwa maarufu kweli hasa kwa walalahoi. Sasa, kuna mradi ulikuwa wa kupanua ile barabara ya Morogoro (Morogoro Road), na eneo la kuanzia Ubungo kuelekea Kimara ilibidi njia ipanuliwe sana ili kupisha ujenzi wa "double roads". Upanuzi huu ulihusisha ubomoaji wa nyumba za watu na sehemu za biashara. Wananchi walikuja juu kweli.

Mzee wa Kiraracha aklivalia njuga hasa. Watu wakenda hadi kulala kwenye ofisi za NCCR. Lakini serikali kuu ikawa ngangari, nyumba zikabomolewa na barabara ikajengwa. Leo tunapita Ubungo (japokuwa kuna foleni kidogo) kwa amani na raha mustarehe.

Wadau tuwe tayari kukubali mabadiliko. As long as kwamba yatakuwa na faida kwetu. Sio kila kitu tunashabikia tu bila sababu za msingi.
 
Nimepata tetesi kwamba zabuni ya kutengeneza na kusambaza vitambulisho vya kitaifa imetolewa kimizengwe.

Je, kuna mwenye taarifa juu ya tuhuma hizi?

Zabuni imetolewa kwa nani (kampuni gani)?

Nani aliyehakikisha watu hao wanapewa?

Je, waliopewa wana uwezo wa kutimiza masharti hayo?


Tafadhali, mwenye taarifa kuhusu haya awasiliane nami kutumia Ujumbe Binafsi (Private Message).

P.S. Hizi taarifa ni nyeti sana, na ni za hatari. Anaweza kuondoka mtu hapa!
Nafahamu kuwa zabuni haijatolewa isipokuwa ndiyo kwanza imetangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nafahamu kuwa hadi sasa kuna washauri walioteuliwa bila kupitia mkondo wa zabuni kwa vigezo vya usalama.

Hawa consultants ni Gotham International Ltd. Nafahamu pia kuwa hata zabuni ilikuwa isitangazwe kwa vigezo hivyo hivyo vya usalama kutokana na unyeti wa kazi yenyewe ya kuandaa taarifa za nani apewe kitambulisho.

Katika kuwaajiri washauri hao bila shaka Muungwana alibariki kwa sababu hizo za usalama.
 
Nafahamu kuwa zabuni haijatolewa isipokuwa ndiyo kwanza imetangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nafahamu kuwa hadi sasa kuna washauri walioteuliwa bila kupitia mkondo wa zabuni kwa vigezo vya usalama. Hawa consultants ni Gotham International Ltd. Nafahamu pia kuwa hata zabuni ilikuwa isitangazwe kwa vigezo hivyo hivyo vya usalama kutokana na unyeti wa kazi yenyewe ya kuandaa taarifa za nani apewe kitambulisho. Katika kuwaajiri washauri hao bila shaka Muungwana alibariki kwa sababu hizo za usalama.

Maua Mazuri,

Karibu sana JF
 
Critics bwana! Yaani wao kila kitu ni kupinga tu. Labda tulaumu mfumo uliotulea na kutujenga kuogopa mabadiliko. Hii inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya umasikini wetu. TUNAOGOPA MABADILIKO!

Hapa nakumbuka story moja ya miaka ya nyuma kipindi Mrema akiwa NCCR-Mageuzi. Kipindi hicho huyu bwana alikuwa maarufu kweli hasa kwa walalahoi. Sasa, kuna mradi ulikuwa wa kupanua ile barabara ya Morogoro (Morogoro Road), na eneo la kuanzia Ubungo kuelekea Kimara ilibidi njia ipanuliwe sana ili kupisha ujenzi wa "double roads". Upanuzi huu ulihusisha ubomoaji wa nyumba za watu na sehemu za biashara. Wananchi walikuja juu kweli. Mzee wa Kiraracha aklivalia njuga hasa. Watu wakenda hadi kulala kwenye ofisi za NCCR. Lakini serikali kuu ikawa ngangari, nyumba zikabomolewa na barabara ikajengwa. Leo tunapita Ubungo (japokuwa kuna foleni kidogo) kwa amani na raha mustarehe.

Wadau tuwe tayari kukubali mabadiliko. As long as kwamba yatakuwa na faida kwetu. Sio kila kitu tunashabikia tu bila sababu za msingi.

Hapana, Mkuu. Tunajua uwezo wetu ndiyo maana tunaupinga huu mradi. Hilo la barabara angalau tuna uwezo nalo kiasi lakini si hili.

Soma huko wenye thread ya NHIF usikie jinsi walivyotumia mapesa kibao kununua software lakini bado wanajaza fomu kwa mkono na kutabulate kwa calculator! Huu mradi hauleti maendeleo yeyote kwa mwananchi wa kawaida (ambaye si wewe au mimi) isipokuwa adha tuu!
 
Na salva Rweyemamu naye atapewa kitambulisho cha Uraia????
 
Tatizo kubwa linalofanya wengi tuwe critics wa miradi ya serikali especially miradi mikubwa ni mazingira ya USIRI yanayotawala process nzima ya hii miradi, kufichwa kwa information ambazo zinatakiwa ziwe wazi kwa public, kutokueleweka kwa gharama halisi za mradi/miradi na namna tenda zinavyogawiwa.

Ninaamini kama kila kitu kingekuwa wazi na hakuna usiri basi hata Membe & Co wakishinda zabuni ya mradi ni dhahiri wanakuwa wameshinda kihalali....lakini damn it...kila kitu Bongo sasa hivi ni kipigiana cross.
 
Darisalama, ambapo pengine ndipo pana neema nchini mwetu, watu wanatembea kutoka Kimara hadi mjini kwa kukosa nauli ya daladala.

Leo unataka kumlazimisha huyu bwana au bibi ajinunulie yeye, mke wake, watoto wake na wale anaowalea walioachwa yatima na dugu zake! Huyu yuko mjini. Je yule wa kijijini ambako hakufikiki isipokuwa kwa helikopta au boti?Au hivi vitambulisho ni kama pasi, kwa wale wenye uwezo tuu?

Leo wanatugelesha na database wakati wenzetu wa Brela wenye uwezo mkubwa bado wanatuza kumbukumbu kwenye mafaili! Nchi ambayo ni asilimia 10 ya watu wake ndiyo wenye access na umeme inataka kuleta mambo ya smart card? Ni vijiji vingapi vina studio za kupiga picha? Au mambo yenyewe yote ni digital nchini mwetu! Leo asilimia 31 ya wananchi wetu hawajui kusoma wala kuandika, hivyo vitambulisho vitawasaidia vipi?

Hapana, nchi yetu ni masikini na hata tukijibhalaghua vipi ukweli unabaki hivyo hivyo. tunachangiwa vyandarua na wacheza sinema lakini hatuoni tatizo kutapanya mabilioni kwa miradi ya kipuuzi kama hii!

Amandla!
 
Fundi mchundo,
Vitambulisho vya uraia huwa ni daima tofauti na Passport, kitambulisho chga kazi ama driver's licence ambavyo unahitaji ku renew baada ya muda fulani.

Kutokana na maelezo yako yaliyotangulia inaonyesha wazi hufahamu kabisa matumizi ya vitambulisho hivi tunavyoongelea hapa.

Namba unayoipata ni namba yako wewe hadi kufa haiwezi kupewa mtu mwingine yeyote!
 
Back
Top Bottom