asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.
Nashukuru wapo ambao waliokuwa wameona kuwapeleka mahakamani ilikuwa njia ya kuwazawadia na wangetoka na kutamba baada ya kifungo kwa kuwa bado wangekuwa matajiri.
Hoja nzuri!!!!
2. Mwenye akili timamu yeyote anajua huyo aliyefaidika na EPA tayari choka mbaya. hii ni adhabu kubwa sana... kuliko ukimpeleka mtu gerezani... kwa miaka miwili au faini... mil. 5, ambazo huenda ndio ziko kwenye sheria kama adhabu... kumbuka sheria nyingi zina adhabu za juu..... jamaa wangeweka fedha zao kwenye Hisa mfano za NMB. wakitoka kifungo baada ya mwaka au miezi... kwa kuwa hawakutumia silaha misamaha mingi inge-apply kwao... wange-endelea kuwa mamilionea...
.
Date::8/21/2008
Spika Sitta ampa tahadhari Rais Kikwete kuhusu wahujumu uchumi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta, amemkumbusha Rais Kikwete kuwa wahujumu uchumi hawastahili kuneemeka kwa madai ya haki za binadamu.
Na Ramadhani Semtawa
Mwananchi
WAKATI Rais Jakaya Kikwete, akionyesha huruma kwa watuhumiwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Spika wa Bunge Samuel Sitta, amemkumbusha kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.
Spika alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni, ambayo pamoja na mambo mengine iliwapa ahueni mafisadi wa EPA kwa kuwaongezea muda wa kuzilipa hadi Oktoba 31, mwaka huu.
Baada ya hotuba ya rais, Spika alimtaka kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.
"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.
Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.
Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.
Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.
Hakika ni bora na heri Sita ndo angekuwa President wetu, uliona wapi rais mwenye dola anabaki kusikitika na kukosa cha kufanya wakati sheria na kanuni zinakuwepo kulingana na mazingira ya wakati huo.
Kama ndiyo hayo, kweli kazi ipo!!!!! Na afadhali asihutubie kwa sababu hii itakuwa sawa na kung'ang'ania kuzoa maji yaliyomwagika! Nchi inayumba kama washauri ndio wanamshauri rais hivi! Labda anahotuba yake ataitoa mfukoni, siyo hiyo rasmi
Kama ndiyo haya anayotaka kuzungumzia kweli
Je tukimwita ZeCommedy kuna tatizo
Hivi huyu President kwa akili yake nyepesi tu amabzo hakuna hata mtanzania mmoja ambaye hizo statistics hazimuingii hakilini yeye inakuwaje akubali jamani??
Lakini kwa Rais Kikwete sishangai mambo yake
Maana aliagiza kamati aliyounda kuchukua hatua za kisheria na pesa zirudishe, wao wakaja na riport vitu viwili tofauti na akapokea
Report yenyewe hata hajaisoma na kuona ndani yake kuna nini, anawapongeza kwa kazi ngumu na nzuri sana walioifanya
Hivyo kwa mtu kama huyu kwenda kuliutubia Bunge na watanzania wote kwa kupmba kama hizo si ajabu ndugu!!
anyway simkubali hata kidogo na nina mengi sana ya kumuelezea huyu mtu
tusubili hiyo kesho