Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

......kwa mtazamo wa haraka, nadhani source yake iko katika mchango waliopeleka TAKUKURU Ikulu kwa ajili ya hotuba. Haingii kichwani hotuba yote ikajaa taasisi moja tu.

...pili sitaki kuamini kuwa JK hatakuwa makini kiasi hicho cha kwenda kuhutumbia bunge na Taifa kwa ujumla juu ya TAKUKURU tu.

The way ilivyokuwa published, nilijiwa na mambo mawili kichwani;

1: Rais anakwenda kureveal mambo makubwa bungeni kurudisha imani kwa watanzania kwamba hajasahau wajibu wake wa kuilinda na kuitetea katiba ya Jamuhuri ya muungano(if any and he believes in it) wa Tanzania. Mambo hayo yakiwa ni pamoja na maadhimio aliyoweka ya kuwakabili mafisadi.

2:Baada ya kuona mambo hayaendi yanavyotakiwa anaenda kutangaza kujiuzuru.

So nilikuwa nimeshikilia pumzi mpaka sasa wala siamini na najiona kwamba sikujitendea haki kwa kuwa na matumaini makubwa kiasi hicho. Rais wangu ambaye watu zaidi ya 37ml. wanamtegemea hakuweza hata kuwaza hayo ambayo mtu wa kawaida kama mimi nimeyawaza. Je mtu huyu ana mawazo mepesi kiasi gani???????
 
Date::8/21/2008
Spika Sitta ampa tahadhari Rais Kikwete kuhusu wahujumu uchumi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta, amemkumbusha Rais Kikwete kuwa wahujumu uchumi hawastahili kuneemeka kwa madai ya haki za binadamu.

Na Ramadhani Semtawa
Mwananchi

WAKATI Rais Jakaya Kikwete, akionyesha huruma kwa watuhumiwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Spika wa Bunge Samuel Sitta, amemkumbusha kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.

Spika alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni, ambayo pamoja na mambo mengine iliwapa ahueni mafisadi wa EPA kwa kuwaongezea muda wa kuzilipa hadi Oktoba 31, mwaka huu.

Baada ya hotuba ya rais, Spika alimtaka kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.

"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.

Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.

Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.

Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.
 
I have never been hurt in life! This JK is a complete bore! All my doubts now have been cleared that he is what he is. I am very frustrated because no hope for Tanzania is any near. I am even more frustrated that politicians are capitalising on the ignorance of the majority of Tanzanians including their own parents! I have never had a sleepless night for a politician like I had tonight!

I was so disgusted by a 'joke' given by JK that he can order the arrest of Dr Slaa and no one would do anything if he decided to, NO ONE! Some of you may have taken this section very lightly, but to me this was one of the most nauseous! I am not a politician, but I love my country and I think Dr. Slaa derseves some respect for what he has been doing. He is worth more than a big number of CCM MPs put together in a bunch! Dr. Slaa did you also laugh at this JK's remark! I am sure he was trying to send some strong message in this statement which to many sounded like a mere joke! He should have replaced the name Slaa with Aziz/Lowassa! He couldn't have done it, because he was sending some message.

But what JK has forgotten is that his tenure will pass, he will come and join us and another person will take over and have the same powers and give the same 'joke' like he did to Dr. Slaa, but this time the name Dr. Slaa would be replaced with Mr. Kikwete. Who knows, he could be Dr. Slaa (a simple matter of probability!) for the net president. That is when JK will realise being a president is simply kupokezani vijiti!

By reducing criminal offenses to civil (in EPA) without good reasons is just letting the president exercise powers that he doesnt have! This is equal to ordering (without giving reasons) the arrest of a good citizen! Because breaking a law may either be by action or omission! By not prosecuting the EPA culprits is a very serious omission (which looks more of a an ACTION though - I am confused).

Simply, JK's speech was heartbreaking to the MPs and to all sober minds! Sasa ataanza visa na Sitta for overshadowing him!
 
Emmanuel Tatobi alimpongeza Rais kwa uamuzi wa kufilisi mali za mafisadi na kuongeza kuwa uamuzi huo ni ishara kuwa kweli fedha zilizochukuliwa na mafisadi hao zitarudishwa. Tatobi alisema uamuzi wa serikali wa kutowapeleka mahakamani mafisadi hao, kumeiwezesha serikali kuzipata fedha hizo ambazo labda zingeweza kupotea au kuchukua muda mrefu kuzipata kutokana na utaratibu wa Mahakama..

Kumbe wapo wanaofikiria kama mimi!
 
Naona hiyo fedha inatafutiwa au imeshatafutiwa mlaji mwengine kimahesabu , na kimawazo tumehamishiwa katika uhakika wa kuwa fedha hiyo itatumika katika kuendelez\a maendeleo ya kilimo .

Naona hapa tunapigwa chenga ya mwili. Jambo moja ambalo litaiweka CCM pahala pabaya ni kutowashughulikia mafisadi kisheria , wafadhili sidhani kama wataridhishwa na mashairi ya Kikwete na kufungulia mijihela yao ,ikiwa Kikwete amewaeleza WaTanzania ambao wengi wao wanatongozeka kwa maneno mazuri yanayosaidiwa na vyombo vya habari ,lakini kwa wengine ambao wanauchungu na misaada yao isiyotumika kikamilifu , watataka kujua ni hatua gani zimechukuliwa juu ya wale wote waliohusika na ubadhirifu.

Na pia wananchi nao wataikubali kwa muda hotuba ya raisi lakini muda huo utakuwa si mrefu na watarudi upya kwenye mstari na kujipanga kudai hatua za kisheria zichukuliwe.Kikwete atapata mtihani mwengine.
 
Hatuwezi kukubaliana hivyo, kwa sababu kukubaliana na maoni na hoja dhaifu ni kujidhalilisha. Maoni dhaifu kama ya kwako hayaitaji kukubaliwa bali kupingwa moja kwa moja on the get go!.

Tatizo unafikiri ni negative kwangu, as a matter ni negative kwao na positive kwangu na kwa timu (as long as in that team Mwanyika, Hosea, na Mwema hawamo.. or anybody else picked by His Excellency).

Wrong, nataka (sijui wengine) waende mahakamani ili waheshimu sheria na wasiigope. Nataka kutetea utawala wa sheria siyo utawala wa kisheria wa waoga wa sheria!

Watakuzuga wewe tu. Yaani kweli unaamini kuwa fedha hizo zitaingizwa kwenye kilimo? Utaweza vipi kutofauitisha fedha za EPA na fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya Kilimo?

Wewe unaeleweka una agenda gani? kwa hivyo haya usemayo yanaeleweka.

Nashukuru wapo ambao waliokuwa wameona kuwapeleka mahakamani ilikuwa njia ya kuwazawadia na wangetoka na kutamba baada ya kifungo kwa kuwa bado wangekuwa matajiri.
 
samahani Bandugu,

naitafuta hiyo hotuba kamili...........je inawezekana ikawekwa ktk sticky section?
 
Hakika ni bora na heri Sita ndo angekuwa President wetu, uliona wapi rais mwenye dola anabaki kusikitika na kukosa cha kufanya wakati sheria na kanuni zinakuwepo kulingana na mazingira ya wakati huo.
 
najaua atatumia muda mwingi na pesa nyingi kumfuatiliziaa Six .....maana hakutegemea fyongo toka kwa mkuu wa nchi muda kama huu wakati nchi ikiwa hali mbaya kama ile.......JK kwisha habari yake...mimi nilifikiriaa alipoanza kusifia na kupongeza watendaji niliona .....litalofuata ni kujiuzulu apishe wengine...eehh kumbee anaaanza kupiga porojoo dooooooooooooo.....nchi haina mwenyewe
 
Nimesikia hotuba yake ilichukua masaa matatu mfululizo ,magazeti yanadai amezungumza cha maana wapinzani wanadai hakuna hata moja la maana.

Kwa yeyote mwenye uzoefu wakupata nakala za hotuba zitolewazo na Raisi atuwekee hapa haraka kabla magazeti hayajawateka wananchi.
Kwani nasikia ni usanii mwengine kutokana na vyanzo vinavyoponda bila ya kuzingatia kilichozungumzwa ingawa ndivyo inavyotakiwa kwa upinzani kupinga na kuipindua juu chini hotuba hiyo ili ionekane haina mshiko zaidi ya ubabaishaji.
Kwenu wakwasi wa habari kutuwekea ngonjera ya Raisi Mheshimiwa Jakaya Kikwete.
 
asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.
 
Date::8/21/2008
Spika Sitta ampa tahadhari Rais Kikwete kuhusu wahujumu uchumi

"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.

Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.

Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.

Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.

Heko Spika Sitta, You are our ROBERT OUKO of TANZANIA
 
Nashukuru wapo ambao waliokuwa wameona kuwapeleka mahakamani ilikuwa njia ya kuwazawadia na wangetoka na kutamba baada ya kifungo kwa kuwa bado wangekuwa matajiri.

Kwani hawawezi kufungwa na kufilisiwa mali zao???
 
asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.

Hotuba nzuri kama kiburudisho,au? Maana kama humohumo tunaambiwa lazima tuliwe kwanza kabla hatujala
 
asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.

Bishanga,

Hizi tangible results unazozungumzia ungeziweka hapa ili tuzijadili.
 
Hotuba nzuri?

Wakati huu watu wamevuna tu mchele sh 1200 kwa kilo mijini

Consumption ya mtu mmoja sasa hivi mijini si chini ya sh 2500 kwa siku (maji, chakula, malazi, nauli nk)

Tuweni makini jamani. Ushabiki wa aina yoyote hautatuondolea matatizo yetu ya msingi
 
Back
Top Bottom