Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Quote of the year

"usipokuwa tayari kuliwa kidogo huwezi kula...huwezi kutaka kula tu bila kuliwa...sina maana hiyo"....\

JK 2008!
 
Sasa tungojee sokomoko kati ya 6 na wadau pinzani ndani ya SISIEM. Na huyu hawamuachi kipindi kijacho, wamegundua kimbembe cha kumpa kichaa rungu!

Sitta hayuko peke yake. Ila sasa, tumfuatilie kwa karibu na kuwaatupia jicho marafiki zake, na wale wanaomuunga mkono. Akizungukwa na mafisadi mchezo utakuwa ni ule ule.



.
 
Wengi tulisha anza kupotezwa na wa roho wa madalaka...
Jk mlizidi kumuona mjinga nyie ndio mna akili..haya sasa hebu tuambieni...
hii hotuba ya pili ya raisi pale BUNGENI Dodoma....umejisikiaje na unasemaje!?

Ni Nzuri
au ni Mbaya
 
we unatuchoza sasa. kwa mjadala unaondelea huku ndani hakuna swali hapo
 
asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.


Wewe unasifia kitugani kizuri kafanya?
Unamsifia kwa wema upi? Kama kuweka umeme Nchi nzima ni kazi yake,Saana alitakiwa atueleze kwanini pesa yetu ya EPA imeibiwa maana hatu imani na mlinzi huyu.

Kwanini mpaka sasa hajaweka umemem vijijini? eeeh! yaani hii sio kuomba ni kazi tulio mpa wewe unafikili ulinzi ni wanini anapewa eeeh! kwasababu ya majukumu makubwa ya kulinda Tanzania (yaani madini yasiibiwe na pesa za EPA zisiibiwe) alafu watu walio iba awashughulikie.


Hizi ni HAKI wala hatuitaji kuomba eti Rais awafunge majangiri wa BOT
cha msingi hapa asipo wafunga atakuwa katu nyima haki yetu ya kikatiba na hatakuwa kavunja kiapo(maana aliapa kuwa atailinda nakuiheshimu katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania)katiba inasema kuwa Rais anawajibu wakuilinda nchi yake so Hivyo kutokana wajibu huo basi Sisi tukampa(gobole za kila haina siraha watu mitambo na kadhalika ili avitumie ktk kukulinda wewe)


Mimi simsifii kwa chochote maana nyenzo kapewa,angefanya bila kuwa nyenzo kama alivyo DR SLAAA hana watu wakumlinda hana usalama wa taifa hana jeshi ila anatumia kaweza kufanya mambo ya kishujaa.eeeeh


Shujaa ni kama labda niseme Pailot kaugua ghafla abilia anakamata uscani anashusha ndege chini ikiwa salama huyo shujaa ila mtu alie somea siwezi kuita shujaa hiyo ni wajibu hakuna kujitetea.

Tafakari yangu ni :viongozi watmize WAJIBU tutawadai sikumoja kama sio wao watoto wao watalipa.NGUVU HAIPOTEI
 
Date::8/21/2008
Spika Sitta ampa tahadhari Rais Kikwete kuhusu wahujumu uchumi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta, amemkumbusha Rais Kikwete kuwa wahujumu uchumi hawastahili kuneemeka kwa madai ya haki za binadamu.

Na Ramadhani Semtawa
Mwananchi

WAKATI Rais Jakaya Kikwete, akionyesha huruma kwa watuhumiwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Spika wa Bunge Samuel Sitta, amemkumbusha kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.

Spika alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni, ambayo pamoja na mambo mengine iliwapa ahueni mafisadi wa EPA kwa kuwaongezea muda wa kuzilipa hadi Oktoba 31, mwaka huu.

Baada ya hotuba ya rais, Spika alimtaka kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.

"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.

Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.

Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.

Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.

JK habari ndo hiyo. Afadhali Mhe Sitta umesema mana najua juhudi zako ndo zinaishia hapo
 
hapo nyuma nimesikia kuwa waziri mkuu anasubirikupewa nafasi bungeni ili atueleze watanzania hatua ya richimond ilipofikia, lakini mpaka leo hajapewa hiyo nafasi na bwana six,sasa hawa lao si moja,kuuma na kupuliza.

Na sema hapa tunazugwa tu,hakuna cha six wala mkuu wa kaya wote lao moja.ingekuwa kweli sita anataka kifanyike hicho alichokisema angewapa uhuru wabunge wake wenye hoja za msingi ili zijadiliwe bungeni na sio kuzizuia kama anavyofanya sasa.

Pamoja na tujineno twake mimi sikubaliani naye moja kwa moja,tena nazidi kufananisha na makamba
 
Dr. Slaa, huku shamba hatujakupata kabisaa. Fanya utaratibu through Tz daima,M/Halisi na kadhalika.

Dr. Slaa; naomba CHADEMA muwe na plan ya kuanzisha au kununua radio station. Mimi nitachangia. Plz nipe the way foward. Sijakata tamaa, na simuombi Mungu anisadie kwa sasa. Ipo siku tu, hawa kwa sasa ni saizi yetu. Naamini chama chenu kinathubutu, na ndo ccm wanawaogopa.

Sala maalum

"Mungu nilinde nisaidie vijana hasa wale walio under 18. Nitakapo kuja kwa ajili ya Msaada usiniache mwenyewe. Jina lako lihimidiwe. Bariki Tanzania, Bariki Tanganyika"

Asante
 
JK kawasafisha jamaa zake kwa omo Lowasa sasa msafi na mategemeo atamrudisha kwenye ulaji time is running and will tell, Spika kaongea lakini hakuna litakalofanyika kazi bure kweli itakuwa kama BWM alivyosema kupiga domo domo lakini utendaji Ziro

Hebu jiulize ule msamo wa KAsi Mpya Ari Mpya kwenye hotuba ya jana sikusikia hata kipande kweli huu ni usanii maisha bora ziro
 
Du hii survey ya hotuba inafungwa 2036?,. Haya wale mtakaokuwepo kila la kheri siku ya ufungaji.
 
Hakuna la kufurahia katika hotuba yake. Makosa yafuatayo yalijitokeza wazi
Kumsifia/kumshukuru waziri mkuu aliyepita Lowassa mbona mawaziri waliopita hakuwashukuru? Why Lowassa only JK hajawasoma watanzania wanavyomuona Lowassa!

Kutaja kuwa kuna mambo ya nchi ya Zanzibar na mambo ya nchi ya Tanganyika wakati haipo (Tanganyika)
Kutoa takwimu kwa kujipendelea ili kuonyesha kuwa uchumi na hali ya maisha inaenda vizuri. Kitaalamu kama alishaamua base year ni 2005 basi comparison zote angetumia mwaka huo. Utaona mara base year anatumia 1980s mara 1990s nk. Huu ni ujanja unaomuondolea sifa kama mwanauchumi.

Kuwalinda mafisadi. Rais amekiuka katiba ya nchi; hana mamlaka ya kuzuia mtu yeyote asishtakiwe; mamlaka aliyo nayo ni kusamehe yule ambaye keshatiwa hatiani na mahakama. Hivyo hawa wa EPA alipaswa kusubiri kwanza washtakiwe halafu awasamehe.

Kawadanganya wananchi juu ya fedha za EPA. Waziri wa fedha alishasema fedha hizi si za serikali bali makampuni binafsi. Sasa rais anasema hela hizo wala si bn 133 bali mfuko ulikuwa na bn 600. Anasema hela hizi zilizorudishwa na zitakazorudishwa zitapelekwa kwenye kilimo! Kwa nini serikali igawe fedha zisizo zake?

Anaendelea - hatarajii makampuni husika kuja kudai lakini kama kuna watakaodai basi serikali itawalipa!!. Hapa ndipo tumepigwa mchanga wa macho. Hatujui mfuko umebaki na ngapi, yawezekana zipo bn 200 tu hivyo bn 400 zimeshaliwa. Zitakazorudi ni say bn 100 na zinapelekwa kwenye kilimo, lakini makampuni yatayokuja kudai (lazima yatadai fedha zake) yatadai 600bn na kwa kuwa zipo 200bn basi serikali italipa hiyo tofauti ya 400bn (wakati kilimo kitakuwa kimepokea 100bn tu). Halafu waTZ kama mazezeta vile tunapiga makofi, aibu. Hii ndiyo hali halisi ya almasi na kichupa alichokizunguma Mwl. Nyerere.

Na mengine mengi unayoweza kuongezea
 
For some elites in Tanzania, admitting that we are off truck as far as leadership and accountability is concerned may be unthinkable, but the reality is undeniable that we are! In a sense, the agents or servants whom we charged to protect and keep the constitution - our agreement-, the rule of law are caught in the vicious circle, they are dysfunctional, and definitely they are blind, leading us-the- clueless.

But again in a country with more than 35 million people, there is no such a thing that all are clueless- and that is why we are writing and we are reading today to inform the public on the astride move of the ruling elite in our Republic. It is the urgency of the moment in the history of the United Republic of Tanzania that has been overlooked deliberately for some reasons.

The 21st of August 2008 was the day of hope for every Tanzanian who believed in the course of good governance and accountability that the head of state in his address to the parliament is going to held accountable all those who have looted our economy and shred away more than 130bn Tanzania shillings - US$ 108Million from the External Payment Account Arrears - Central Bank of Tanzania.

This hope has been turned into despair by the highest office of the land. He appealed to them that those who had returned the money will not brought before the court of law but those who did otherwise will be.

Whether they will return it or not, there is only one thing we know about them; they are bandits, looters, culprits, call them any name to their disgrace and they were supposed to be arrested by now, but that is not the case! In contrast, Tanzanian have been divided into classes.

The have not, the poor, the voiceless, the people, are the victims of the law and the bureaucrats and bandits are not. There is no such a thing again that no one is above the law. The ruling elites and the bandits are now above the law.

The entrusted body by the people for the people to oversee and ensure that the rule of law is abided by every citizen in the country is now negotiating with the bandits. Shame on them! The highest office of the land have defaulted the constitution, they have failed us, the people, the voiceless.

But there is one hope still on our hands, they history have been written, be it tomorrow, next month, two or 10 years down the line, we will indeed bring them to the justice, and restored our defaulted agreement, the constitution, the rule of law, to the way it used to be. God bless Tanzania!

Cheers

Thomas David Maqway
Dar es Salaam-Tanzania
 
Kilichonifanya niiione hotuba yake mbaya ni kushindwa kwake kuzungumzia masuala makubwa yanayohusu maisha ya watuw a kawaida.

Ni vema ametoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Muungano na EPA (hata kama ufafanuzi wake hautakidhi haja), lakini kuacha kwake kuelezea kinachotokea katika uchumi kiasi cha kuyafanya maisha ya watu wa kawaida kuendelea kuwa magumu, imenishangaza sana.

watu wengi wa kawaida wanayashabikia masuala ya EPA lakini kiu yao kubwa ni kuona ugali unafika mezani kwao bila shida, ni kuona kuwa wanapata huduma muhimu za maisha bila usumbufu, hilo halikujitokeza katika hotuba hii.

Sanasana alichofanya ni kuzungumzia uchumi mkuu (macro economy) ambao kimsingi uolishajengwa na Mkapa. Wakati anaingia madarakani aliahidi kuhakikisha anajenga uchumi mdogo (M<icro economy) ili kuwafanya wananchi wa kawaida wanufaike na kukua kwa uchumi wanakokuona kupitia takwimu, Hajasema hilo.

Ninachukulia kuwa ameshindwa kulisemea kwa sababu hajalifanya
 
Niliwahi katika luninga yangu saa 2 kabla mhesimiwa hajafika hata Dom airport,kwa ajili ya kuisikiliza speech ya President wetu ya kulihutubia Taifa kupitia Bungeni.

Kwa kweli ktk hotuba yake yapo ALIYONIKUNA hasa katika lile la muungano wetu wa kuendelea kuwa Tz moja na si vinginevyo.

Na yapo ALIYONIKOROGA hasa pale alipo repeat ktk speech yake kuwa umakini ktk kuwachukulia hatua mafisadi kuliko umakini ktk kuwajibu na kuwatuliza wananchi wanaohujumiwa ktk uchumi wao huku kila kukicha maisha bora ni kitendawili.Na hata mheshiwa spika naye alipo-synchronize ki-mtizamo na mimi na kumwomba awe na kaukali kidigo ktk hili.

Je kwa staili hii hotuba kuwahi tena kwenye luninga yangu itanibidi niwe naitafakari zaidi. JE TUTAFIKA AU TUTAFIKWA?
 
Back
Top Bottom