Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa tungojee sokomoko kati ya 6 na wadau pinzani ndani ya SISIEM. Na huyu hawamuachi kipindi kijacho, wamegundua kimbembe cha kumpa kichaa rungu!
asikudanganye mtu hotuba ilikuwa nzuri sana tena sana,hasa ukizingatia summary aliyotoa ya juhudi za kujenga barabara kuunganisha mikoa yote (na kuna tangible results) na juhudi za kupeleka umeme kila makao makuu ya wilaya nchi nzima.siku zote siri ya maendeleo ni kujenga infrastructure na kuacha wajasiriamali wawekeze kwa raha zao.halafu you could feel his sincerelity na utu wa kutotaka ku abuse powers.let us give credit where it is due na kwa hili la hotuba tumpe haki yake.
we unatuchoza sasa. kwa mjadala unaondelea huku ndani hakuna swali hapo
Date::8/21/2008
Spika Sitta ampa tahadhari Rais Kikwete kuhusu wahujumu uchumi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta, amemkumbusha Rais Kikwete kuwa wahujumu uchumi hawastahili kuneemeka kwa madai ya haki za binadamu.
Na Ramadhani Semtawa
Mwananchi
WAKATI Rais Jakaya Kikwete, akionyesha huruma kwa watuhumiwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Spika wa Bunge Samuel Sitta, amemkumbusha kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.
Spika alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni, ambayo pamoja na mambo mengine iliwapa ahueni mafisadi wa EPA kwa kuwaongezea muda wa kuzilipa hadi Oktoba 31, mwaka huu.
Baada ya hotuba ya rais, Spika alimtaka kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.
"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.
Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.
Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.
Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.
Jibu swali ...tafadhali...
Jibu swali ...tafadhali...