Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Ahaaa hapo ndiyo siasa za bongo zinaponishinda.

Kuna upendeleo wa waziwazi unaofanywa na polisi hasa ikifikia suala la maandamano kwa wanaCCM. Wao wakitaka kufanya maandamano wanaruhusiwa mara moja.

Ila inapokuja kwa wapinzani kufanya maaandamano basi utawasikia polisi wakisingizia kuwa watavuruga amani na kuchochea vurugu!

Nyie mapolisi na serikali kama hamtaki demokrasia ya vyama vingi basi mseme na siyo kuwanyima haki wapinzani kwa visingizio visivyo na msingi.

Wembe.
 
Ahaaa hapo ndiyo siasa za bongo zinaponishinda.
Kuna upendeleo wa waziwazi unaofanywa na polisi hasa ikifikia suala la maandamano kwa wanaCCM.Wao wakitaka kufanya maandamano wanaruhusiwa mara moja.Ila inapokuja kwa wapinzani kufanya maaandamano basi utawasikia polisi wakisingizia kuwa watavuruga amani na kuchochea vurugu.!!

Nyie mapolisi na serikali kama hamtaki demokrasia ya vyama vingi basi mseme na siyo kuwanyima haki wapinzani kwa visingizio visivyo na msingi.

Wembe.
tatizo hao wasioombwa vibali ndio hao hao wanaoamrishwa wavae kiraia ili waandamane kama wanachama wa CCM kumbe ni mazombi.
 
Kasheshe,
Labda nikwambie hivi tatizo kubwa ni watu kama nyie mnaofikiria kesi ndogo kama ya EPA sio kabisa mwanzo mbaya wa Utawala bora...
Hapa mkuu, Waziri mkuu aliyetoka alijiuzuru kwa sababu ya dollar laki tano tu ambazo hazikuwa za serikali..Ni ushirika wake ktk kampuni binafsi na utoaji wa kibali ambacho hakutakiwa kufanya...yaani ni mambo ya kawaida kabisa ktk mazingira ya Afrika lakini leo jambo zito kama la EPA wewe unaliona dogo hali mnachojaribu ni kuwa na utawala bora kama wa nchi hizi?... hapa mkuu si tunafukuza upepo!

Nimesema mimi nimesoma vipande vipande na ndivyo nilivyotolea mfano... hakuna sehemu ambayo hata ktk vipande hivyo ameonyesha ni kero kubwa ktk Utawala wake hivi sasa. Ni vitu ambavyo vinaweza kusubiri ama kupewa muda..wakati unajua wazi kuwa hili ni tatizo linalotakiwa kushughulikiwa...
Mkuu soma tena maandishi yangu na kisha nambie wapi nimekosea kutokana na hotuba ya Kikwete..
Wewe umeisikia yote ni vizuri ukitutaarifu kila sehemu ambayo umeona watu hawakuelewa ama hawafahamu kutokana na hotuba uliyoisikia..

Utawasaidia zaidi kuliko kuhoji fikra zao wakati wewe mwenyewe huonyeshi mazuri aliyoyasema..
 
This is how CCM and JK continue to amaze me with their cheap tactics to enhance the validity of their absent and empty leadership!

Wameona mapokeo ya wananchi si chanya bali ni hasi kukuiwa na hasira, hivyo wanatumia rungu la Chama kuhamasisha maandamano ili wale ambao hawakusikia utumbo ulioropokwa waamini na kuona kwa Rais na Mwenyekiti alisema kitu cha maana sana!

Kwangu mimi ikiwa sasa ni miaka 2 tangu sakata la EPA lianze, Miaka karibu 3 tangu ajitape kuwa ataleta Muafaka, Mwaka mmoja tangu mambo ya Rochmond na Buzwagi yabainike na matatizo makubwa ya kiutendaji na uzembe wa uongozi hayajapatiwa ufumbuzi thabiti na kuonyesha makali ya Kiti cha Uraisi au Uenyekiti wa CCM, alichosema Bungeni bado ni tupu na batili!
 
Mzee Mwanakijiji,

Is the broadcast still live? I think I missed it, is it recorded somewhere? Keep up this exceptional work.
 
Tunaweza kabisa kuyafananisha mapambano dhidi ya mafisadi na mapambano ya nduli pale alipoamua kuingia nfdani ya mipaka yetu 1978 na kuikalia sehemu ya nchi yetu.

Mwalimu hakumbebeleza nduli wala kumuomba aondoe majeshi yake katika ardhi yetu, bali alitwambia Watanzania kwamba tumevamiwa na nduli Idi Amin na tulikuwa na nia ya kumtoa nduli Idi Amin katika mipaka yetu, sababu tulikuwa tunazo na uwezo pia tulikuwa tunao, lakini katika mapambano dhidi ya mafisadi msanii JK hana nia ya kupambana na mafisadi, hana uwezo wa kupambana na mafisadi na hana sababu za kupambana nao pamoja na kushinikizwa na Watanzania afanye hivyo.

Anachofanya JK ni kichekesho kwa sababu yeye mwenyewe kaingia madarakani kwa kutoa rushwa kutoka pesa alizopokea toka kwa mafisadi mbali mbali. Rushwa hiyo ilitolewa kwa wajumbe waliopiga kura kumchagua mgombe toka chama cha mafisadi. Sasa anaogopa kwamba akiwa mkali mno dhidi ya mafisadi basi wanaweza kabisa kumgeuzia kibao na kuanika hadharani ufisadi alioufanya na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania.

Ndiyo matatizo ya kuwa na Rais aliyepatikana kifisadi. Kamwe hatakuwa jasiri kufanya maamuzi ya kuweka maslahi ya nchi mbele. Siku zote kwake yeye watu wa ataweka mbele maslahi ya wale marafiki zake waliomsaidia kuingia Ikulu. Na ukiangalia si ajabu hata katika EPA kuna marafiki wa JK wanaohusika na ufisadi huo.

Sasa mnathubutu kumwita eti ni mwanasiasa smart!!!!! Alitoa ahadi chungu nzima wakati wa kampeni zake lakini hadi hii leo hakuna hata moja aliyofanikisha. Amepata oppportunities chungu nzima za kurudisha credilibility yake kwa wananchi lakini zote hakuzitumia kwa sababu anajua akiwashughulikia mafisadi basi na wao pia wanaweza kabisa 'kumshughulikia'

Eti aliwaomba warudishe pesa walizoiba baada ya miezi sita, sasa kawaongezea miezi mitatu mingine kama vile mafisadi walimwambia kwamba mabulungutu waliyoiba watayaweka majumbani kwao na wakitakiwa kuzirudisha pesa hizo basi watafanya haraka kuzirudisha!!!!! Pia na wao mafisadi wanastahili kupewa haki za binadamu!

Hana usmart wowote kama mwanasiasa, wala hana sifa za kiongozi na kuna dalili chungu nzima kwamba nchi imemshinda!!! Kama hamtaki kuliona hilo basi mtajiju lakini wengine tumeshaliona siku nyingi tu.
 
Maskini Wadanganyika wanakokotwa huku na kule kama mizoga na chama cha mafisadi!
 
Hivi Wadanganyika wanao andamana, kuunga mkono hotuba isiyokuwa na kitu na iliyokosolewa na Spika wa Bunge, wanalijua walitendalo?
 
nimedokezwa hata mbeya wamefanya leo.Mwanye kigoda wa mkoa Mulla amewahutubia

….wapinzani kwa nini msiandamane nchi nzima kupiga hotuba MBOVUU YA

kiwete...jangala..michosho....na kuunga mkono ushauri[agizo] wa [la]spika kwa kikwete
 
Polisi watawaambia wapinzani haina mapolisi wa kutosha kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa salama, na wakiendelea kuyafanya bila ruhusa basi FFU watatembeza mkong'oto kwa washiriki wote.
 
On Serious note, there is a need for opposition party and other groups to rally to show disatisfaction from President's speech, hii ndiyo itakuwa demokrasia ya kweli na tutaona kama Serikali na vyombo vyake vitakuwa na busara na kuruhusu maandamano haya!
 
Nasikia kichwa kinauma, tumbo linaunguruma , natetemeka kwa hasira, lakini pia nina aibu, kumbe wakati tunalia serikali mbaya wengine, wenye hali mbaya zaidi za kimaisha kuliko mimi, wanashangalia hotuba ya Kikwete.

Vyama vya upinzani havipo, nakiona kimoja tu, Makanisa na misikiti ccm, wasomi mlimani wengi wanamtandao. masikini pia ndio hao, kwa nini CCM isiendelee kuongoza hadi 2080? kweli nitapona magonjwa ya moyo na hasira za mara kwa mara nikiishi TZ? kweli inauma sana......
 
•
Kukithiri ufisadi:Mzee Msuya avunja ukimya

Habari Zinazoshabihiana
• Kingunge avunja ukimya kukosa Kamati Kuu CCM 11.11.2007 [Soma]
• 'Watakaojihusisha na rushwa ya ngono sasa kukiona' 20.01.2007 [Soma]
• Mama Karume avunja ukimya,awashukia wanasiasa wenye tamaa 06.04.2008 [Soma]

*Ataka wahusika waburutwe kortini
*Asema hata vigogo wasionewe haya
*Amkumbusha JK mbinu za Nyerere
*Akerwa na mjadala wa Zanzibar nchi

Na Hassan Abbas

WAZIRI Mkuu wa zamani na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mzee Cleopa David Msuya amelazimika kutoka katika maisha yake ya ustaafu na kuvunja ukimya akilithibitishia Majira Jumapili kuwa anakerwa kuona hakuna hatua za haraka zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa rushwa na ufisadi nchini.

Mzee Msuya aliyepata kuwa Waziri Mkuu kwa vipindi viwili tofauti akifanyakazi katika wadhifa huo na Marais, Julius Nyerere na baadaye Ally Hassan Mwinyi kabla ya kustaafu siasa Oktoba 29, 2000 alisema bila taifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya matatizo yaliyopo, nchi itaelemewa.

Moja ya mijadala mikubwa iliyoligubika Taifa hivi sasa ni juu ya hatua walizochukuliwa watuhumiwa wa ufisadi uliofanyika kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambako kiasi cha sh. bilioni 133 ziliibwa.

Akizungumza kwa hisia na kuonesha wazi kupata wasiwasi juu ya hatma ya taifa hili aliloshiriki kulijenga akifanyakazi tangu siku za mwanzo za uhuru, Mzee Msuya katika mahojiano hayo maalum yaliyofanyika nyumbani kwake Upanga, Dar es Salaam katikati mwa wiki hii, amesisitiza staili hiyo lazima iachwe, kama nchi inataka kupiga hatua.

"Kuna mijadala mingi sana inaendelea kwa sasa, haya ya watumishi wa umma kuhusishwa na rushwa ni sehemu tu ya matatizo tuliyonayo, lakini kubwa zaidi ni kwamba inachukua muda mrefu sana mambo haya kushughulikiwa," alisema.

Mjadala mwingine uliolitikisa taifa ni ule wa zabuni ya kufua umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond ambayo baadaye ilibainika haikuwa na uwezo wa kitaalamu wala fedha na kuibua kashfa nzito iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

Akizungumza bila kutaja kashfa yoyote moja kwa moja,Mzee Msuya alisisitiza kuwa zipo mbinu rahisi za kupambana na wala rushwa Serikalini. "Katika utawala bora kuna utawala wa sheria, huu ukitumika ipasavyo haki itaonekana inatendeka.

"Utawala wa sheria ukifuatwa unasaidia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Mfumo huu utasaidia kupambana na wala rushwa hata kama ni vigogo. Kama mimi Msuya ninatuhuma za rushwa ichunguzwe na kisha nipelekwe mahakamani ukweli ukajulikane, " alisema na kuongeza:

"Lakini mnapojenga staili ya uongozi ambapo kila jambo linaibuka na watu wana tuhumiana hakuna hatua zinazochukuliwa, mijadala inaendelea tu mitaani, hatuwezi kujenga taifa, niseme wazi sioni mustakabali mwema huko baadaye."

Alipotakiwa kueleza uzoefu wake wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere katika kushughulikia kashfa nzito, Mzee Msuya alisema Mwalimu hakuruhusu wala rushwa kutamba wala kuendekeza mijadala.

"Linapoibuka suala zito la kitaifa, kuna wakati Mwalimu alikuwa akiunda tume kimya kimya kuchunguza. Baada ya kupata ukweli alikuwa akitafuta siku ya kulizungumzia suala hilo na kutangaza hatua alizochukua kisha analiambia taifa kuwa mjadala huo umekwisha watu waendelee kuchapa kazi.

"Kwa staili hii Taifa wakati wa Mwalimu lilikuwa haliingii katika mijadala isiyokuwa na tija kama inavyoonekana sasa," alisisitiza.

Akizungumzia mjadala wa Zanzibar kuwa nchi, Mzee Msuya alisema huo ni mfano mwingine wa mijadala ambayo imekuwa ikimsikitisha.

"Kama nilivyosema awali, mjadala wa Zanzibar nao umeonesha ni kwa kiwango gani taifa letu linakwenda kubaya. Ukitazama watu walivyokuwa wakitumia nguvu katika mjadala huo unashangaa.

"Mjadala huo haukuwa na tija yoyote kwa taifa kwa sababu mwaka 1964 mtu yeyote mwenye akili timamu anafahamu kuwa ziliungana nchi mbili zenye mamlaka kamili na kuzaliwa nchi moja Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar na baadaye ikaja kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wanaodai Zanzibar ni nchi waseme bayana wanachokitaka kuliko kujificha katika mjadala huo. Kwa nini hawasemi kuwa Tanganyika nayo ni nchi. Kwa mtazamo wangu mjadala huu umeonesha tatizo kuu la kitaifa tulilonalo kwa sababu tulijadili suala lililo wazi-Zanzibar kama Tanganyika zote si nchi," alisema mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Mbunge wa jimbo la Mwanga, Kilimanjaro.

Alisema analiombea dua taifa lipate viongozi bora watakaoendelea kulinda misingi iliyowekwa na waasisi na watakaokuwa makini katika kupambana na changamoto zinazojitokeza.

Wasifu wa Mzee Msuya

*Januari 4, 1931: Alizaliwa Chomvu, Usangi wilayani Mwanga, Kilimanjaro.

*1952-1955:Chuo Kikuu cha Makerere (baada ya kufaulu kutoka sekondari ya wavulana Tabora) alikotunukiwa Shahada ya Sanaa akibobea katika Historia, Sayansi za Siasa na Jiografia.

*Januari 11, 1959: Alifunga ndoa na Bibi Rhoda Christopher ambaye kwa sasa ni marehemu.

Nyadhifa za kisiasa

*1964-1972-Alikuwa Katibu Mkuu katika wizara mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Jamii,Ardhi na Makazi,Uchumi na Mipango na Wizara ya Fedha.

*1972-2000-Alikuwa Mbunge wa Mwanga kwa vipindi tofauti ambapo pia alipata kuwa Waziri katika wizara za Fedha (1972-1975), Viwanda (1975-1980), Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (1980-1983) ambapo aliushika tena wadhifa huo chini ya Serikali ya Awamu ya Pili kuanzia Desemba 1994 hadi Novemba 1995.

*Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 alikuwa mmoja wa wagombea watatu wa Urais kupitia CCM waliongia hatua ya mwisho akiwa na Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa aliyeshinda.

Mzee Msuya pia alikuwa mwanachama wa TANU na baadaye kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa CCM.

Kwa sasa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na anajishughulisha na shughuli binafsi za biashara, kilimo na ushauri.

Source: Majira

Kasheshe, nadhani kama wazee wengi wastaafu hivi ndio wanavyoona hapo juu naona rais wetu kuna mahali amepotoka.
 
Mimi sishangazwi wala nino maana ndio demokrasia lol....mkipinga wenzenu wanaunga mkono....!! Mwendo mdundo.
 
Mkandara

kama hoja zote Mh. Rais alizoongelea hamjaziona kweli... taifa liko njia panda kutokana na wananchi wake yenyewe.

Tanzania haiko njia panda kutokana na Watanzania bali ni kutokana na viongozi walioshindwa kuiongoza Tanzania pamoja na kuwa walitoa ahadi chungu nzima za kuiptia upya mikataba ya madini ambayo Watanzania tuliilalamikia kwamba haina maslahi yoyote kwa Watanzania bali inawaneemesha Wageni na mashareholders wao.

Watanzania mpaka sasa hatujaona initiatives zozote za kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, bali tunachokiona ni maisha bora kwa kila fisadi. Ahadi tulizoahidiwa za ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya pia hatujaziona bali tunaona uzembe na woga wa hali ya juu katika kupambana na mafisadi ambao wanasemekana wamekupua kati ya shilingi bilioni 300 mpaka shilingi trilioni.

Hizi ni pesa nyingi sana kwa nchi 'maskini' kama Tanzania hasa ukitilia maanani kwamba wafadhili nao wametaa kutoa shilingi bilioni 812 walizoahidi kutoa kusaidi budget ya mwaka 2008/2009 kutokana na kutoona juhudi zozote za kuwashtaki waliokupua mabilioni ya BoT. Hili litaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Tanzania.

Tuache udanganyika kwa kutetea mediocre perfomances, tuseme kweli fitina kwetu mwiko kwa maslahi ya nchi yetu.

Alutta Continua!
 
mimi sirudi huko nategemea kuja kuchukua familia yangu niishi ughaibuni! Siwezi kuishi na watu mbumbu!
 
Kwa CCM kufanya hivyo sio ajabu si ni amri na mikakati kutoka juu Mwenyekiti ,Katibu na wakuu wengine wa chama.Wamewapa vijana wao pesa ya lunch ,ndio hivyo.

Ila ndio hivyo wanalazimisha ionekane kuwa kaongea la maana.
 
Ila ndio na sisi tusiolidhika nasi tuandamane kumunga mkona spika na ku demestrate kutopendezwa na hotuba ya rais pamoja na approach zake.
 
Back
Top Bottom