Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Kama Hatuba haifai ,haifai tu hata mkiandamana kuiungabado hamtabadilisha iwe nzuri.

Binafsi ninhekuwa mie ni muungwana ningeiunga mkono hotuba na shukurani ya Spika wa BUNGE kwani ndo ilibeba dhana halisi ya yale ambayo Rais alipaswa kuwaambia Watanzania.

Hivi nyie mnaosimama kidete na kuandaa maandamano ni watanzania wenzetu mnaoishi kwa mlo wa kubahatisha au ndo mamluki mlowekwa madarakani ili kuendeleza propaganda zao, maisha yanazidi kuwa magumu.utawala wa sheria umepotea.

Mahakama zimebaki kuwa za akina Ramadhani na vibaka wadogo wadogo, huku mafisadi wakigongewa milango na kubembelezwa waamke watoe jibu kama wanaweza kurudisha lini hela, bado mnaandamana kuipongeza Hotuba hiyo kweli wanaomsuport Mugabe ni wale wanaoshiba mgongoni kwake.
 
Taifa la wanafiki ambo mchana wao ndio wanalalamikia maisha magumu ila wako tayari kuona watoto wao wanakosa elimu ili mradi CCM isitoke madarakani.

Wako tayari kuona wakinamama wetu wanalazwa chini kwenye hosipitali ,ila kwa garama ya CCM kuendelea kutawala .
 
hahaha Umenikumbusha issue ya Mapanki nilikuwa Musoma Juzi pale kiwanda cha Musoma Fish wanauza Kilo ya Mapanki shilingi 500, wameweka na tangazo nnje.watanzania hatujazowea kuelezwa ukweli.
 
Hivi kuna habari kama polisi iliarifiwa na kuruhusu maandamano hayo ?

Hili ni muhimu kuliangalia kwa udnani kwa sababu kuna uwezekano maandamano haya yamefanyika kienyeji mno. Yamekuwa ya ghafla sana. Hivi watu wakiomba kuandamana kupinga hotuba ya muunwgana wanaweza kuruhusiwa haraka haraka namna hii?
 
..wapinzani kwa nini msiandamane nchi nzima kupiga hotuba mbovuu ya

kiwete...jangala..michosho....na kuunga mkono ushauri[agizo] wa [la]spika kwa kikwete...

sio wapinzani mimi ni ccm damu lakini sijaikubali kabisaa< ni watanzania wote ambao hatukuikubli tunatakiwa tuandamane kuipinga i can assure you more than 99% hawajaikubali, marehemu balali alifukuzwa kwa ajili ya sakata la bot ila waliochukua fedha wanapewa muda wa kurudishwa kwanza mi naonasio sawa inaniuma sanaa.au baada ya kurudisha watafunguliwa mashitaka?
 
tena kibaya zaidi hao ndo wanashida kupindukia Sometimes huwa naomba siku moja nchi ije kuangukia kwenye mikono ya kiongozi dikteta atunyoshwe wote turudi kwenye laini kwani inaonyesha tunahitaji kulazimishwa kufanya kazi wakati ni wajibu wetu,tunasubiri fullana za kampeni tuvae ili tuonekane tunaisuport ccm

tunasubiri ubwabwa na pilau za wagombea wa ccm ili tuwape kura na kulipwa elfu kumi kisha tunaiuza democrasi ya miaka mitano kwa elfu kumi,unajua kinacho niuma zaidi ni huyu Rais ambae nilimpa kura yangu kwa mara ya kwanza

si kwamba nilikuwa sijafikia umri wakupiga kura la hasha ila nilikuwa nawaona kama wagombe wote wasanii furani,ndo maana alipokuja JK Nikaona huyu amelelewa ndani ya Chama na ni vijana wa Mwalimu kumbe hadithi ile ndani ya biblia ya Yesu na wanafunzi waliomsaliti ndio hiyo inayowasumbua CCM.

sasa sitashiriki tena kupiga kura labda mgombea aje kuwa Mwakyembe au Sita namkumbuka Salim mtu wa watu ambae walimpinga mtualieshiba madaraka hivi wenzangu huwa majiuliza why hakupewa nafasi huyu?
 
Jamani,

Wana CCM Dar wameandamana kwa wingi kumuunga mkono JK kuhusu hotuba yake aliyotoa Dodoma bungeni.

Wananchi wa Tanzania wanaelewa kweli hali ya kisiasa nchini?

Naomba maoni yenu

FP

Mkuu ebu elewa swali lako uliloliuliza?Wanaelewa?
Unadhani wangekuwa wanaelewa wangekuwa wanafanya haya madubuwasha?
Wameshachukuliwa msukule na vibabu vya kijijini kwa JK!
 
Rai jana wakatoa toleo maalum kuunga mkono hotuba ya JK kumbe walikuwa pia wakijipanga kuandaa maandamano ..............
 
Sometimes huwa naomba siku moja nchi ije kuangukia kwenye mikono ya kiongozi dikteta atunyoshwe wote turudi kwenye laini

Kwahiyo unatamani tupate mtu kama okello au kama bokasa au Pelves Mushaaraf!!! yaani tusiwe na utawala wa sheria? sijakuelewa hebu fafanua vizuri.
 
^&&*&NY****MBAF****** jakaya na serikali yako,TUNATAKA NCHI YETU
 
Kwahiyo unatamani tupate mtu kama okello au kama bokasa au Pelves Mushaaraf!!! yaani tusiwe na utawala wa sheria? sijakuelewa hebu fafanua vizuri.

Unaweza kuona kuwa utawala wetu hivi sasa ni tofauti sana na watawala hao uliowaorodhesha. lakini botom line, mwisho wa siku, wananchi wanapata shida na maisha yao yanazidi kuwa magumu licha ya viongozi wetu kutofautiana na madikteta uliowataja.

Katika hali kama hiyo, kuna tofauti gani kati ya wanaoongozwa na madikteta na sisi tunaoongozwa na viongozi waliochaguliwa kidemokrasia lakini hawajaleta matunda waliyotuahidi?
 
Kwahiyo unatamani tupate mtu kama okello au kama bokasa au Pelves Mushaaraf!!! yaani tusiwe na utawala wa sheria? sijakuelewa hebu fafanua vizuri.

Wewe Eddy

Ni utawala upi wa sheria unaouzungumzia hapa kwetu? za akina EPA na akina vibaka? ...the bottom line ni kwamba hakuna utawala wa sheria mpaka sheria iwe sawa kwa wote wakubwa na wadogo!!! Lablda kuna sheria ya utawala

Mzimu
 
Lablda kuna sheria ya utawala

Kuna njia nyingi za kufikia mapinduzi ya kweli kama nguvu ya umma, elimu ya uraia na usimamizi wa uwajibikaji.

MTM naona unatamani utawala wa kiharamia, unaweza kwenda kuungana na joseph kony na generali Nkunda, watakukaribisha kwa mikono miwili. Ila kutupigisha porojo baada ya kunywa chai hatutaki.

Hivi leo tukisema twende Kinesi au Garamba kuanzisha rebellion utastahimili kweli!
 
kizuri cahajiuza kibaya cha jitembeza. maandamano ya nini? eti kuunga mkono hotuba.. ingekuwa nzuri wangeandamana? hili ni shinikizo ili hotuba ikubaliwe
 
Katika hali ya kushangaza,hotuba ya mhe.rais bungeni august 21 imekua adimu kuipata katika readable copies.Je ni kwamba muandaaji wa hotuba hiyo alitaka ipotee au ifutike kabisa baada ya Mhe. rais kulihutubia bunge?Katika searching zangu tegemezi lilikua ni katika website ya Bunge www.parliament.go.tz lakini cha ajabu nako imekua haifunguki je ni kisanii au kiufundi?

Wakati nikiptia vyanzo vingine ambavyo vilitarajiwa kua na aidha soft copy au hata hard copy nimeambulia patupu.
Je hii ina maanisha nini ?Kwamba tusiisome na kuichambua kwa umakini?Na ni kwa nini kupata hotuba hii iwe "dili"?
Mwenye ufafanuzi na atusaidie hapa plz
 
Kweli kazi tunayo jinsi ya kuelimisha umma yapi mabaya yapi mazuri......utafika kipindi watu wanaangalia CHAMA hata kama kiongozi kaongea pumba wao watakuwa wanampongeza tu kwa vile nikiongozi wa CHAMA chao.Hiki ndicho kipo sana CCM mtu kaiba kala rushwa watu wanaandamana kumpongeza.....hivi hawa watu wanaandaliwa mapema kabla ya kuandamana?na wanaandamana kwa malengo yapi?
 
Watu wanaandamana kuunga mkono hotuba ya rais? Sisi kweli ni wajinga sana, na tusimlaumu mtu yeyote kwa umaskini wetu; kweli mawazo yetu ni finyu sana

Kama ni kuunga mkono hotuba basi tutaweza kushiba hotuba hizo huku hakuna linalofanyika. Kikwete ni NATO (no action talking only) kwa hiyo kama ni hotuba tu tunaweza kuzipata kwa wingi sana.
 
Watu wanaandamana kuunga mkono hotuba ya rais? Sisi kweli ni wajinga sana, na tusimlaumu mtu yeyote kwa umaskini wetu; kweli mawazo yetu ni finyu sana

Kama ni kuunga mkono hotuba basi tutaweza kushiba hotuba hizo huku hakuna linalofanyika. Kikwete ni NATO (no action talking only) kwa hiyo kama ni hotuba tu tunaweza kuzipata kwa wingi sana.

Naunga mkono kuwa jina lake rasmi sasa liwe NATO
 
Back
Top Bottom