Wazo la kuwa National IDs ni zuri, nchi nyingi duniani zina aina fulani ya ID; najua UK wanatumia Insurance Number, Australia wanatumia Tax File Number, Marekani wa Social Security Number, Japan nao wana document yao siikumbuki jina tena ila akina-wakuja huwa wanapewa Alien Registration Card, al mradi kila nchi ina namna fulani ya kumpa namba maalum raia wake, na namba hii haina uhusino na namba ya passport yake.
Ukweli kuhusu namba hizi ni kuwa:
(a) Siyo fool proof na zinaweza kutengezwa za bandia; Marekani inasumbuliwa sana na wamexico wanaojitengezea Social security card za bandia. Wengine wao wanazitumia kadi hiz kwa muda mrefu hadi miaka kumi bila kushikwa. Kwa hiyo madai ya kuwa tukiwa na National IDs tutapunguza wazamiaji yanakuzwa tu. Document za aina hiyo ndiyo zinazoweza kufanya wazamiaji wawe wengi. Kama wanapata passport zetu itakuwaje washindwe kupata hizi IDs?
(b) Namba zinazotumika huko nje zina malengo kadhaa na mara nyingi siyo kumtambulisha mtu kuwa ni raia, kwa vile ukienda nchi ile kihalali unaweza kupata kitambulisho hicho hata kama siyo raia. Kwa nchi nyingi, namba hizi hutumika kama index ya mtu kwenye database inayotunza taarifa za kila mtu nchini kwa mfano mapato ya mtu na kodi yake, financial history ya mtu inayosadia kuelewa credit worthness yake, record ya michango yake kwa ajili ya malipo ya uzeeni, tarehe ya kuzaliwa na mahali alipozaliwa, vile vile zinatunza criminal record ya mtu. Hii inahitaji database nzuri sana ambayo sidhani kama kweli Tanzania tumeshatengeza.
(c) Ingawa namba hizo pia zinaweza kutumika kufahamu uraia wa mtu, siyo kawaida watu kutembea na kadi zile kwa vile vitambulisho vingine vya kawaida kama Drivers Licence na Passport vinaweza pia kutumika kuingia kwenye data base na kupata taarifa za mtu.
Kwa maoni yangu, pamoja na faida za vitambulisho hivyo, sidhani kama muda wake umeshafika kwa sababu hatujajenga mazingira ya kuweza kutunza record za raia na kuzipata mara moja, na vile vile kutumia record hizo kujua raia yuko wapi, yaani akitakiwa na serikali aweze kupatikana mara moja.
Nadhani kuwa serikali ingeanza maandalizi ya kutayalisha ujio wa National IDs kwa kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kutengeneza utaratibu mzuri wa kuweka physical addresses za makazi ya kila raia. Huwezi kumtafuta mtu kwa kutumia P.O.Box, lazima kila mtaa upewe jina na kila nyumba iwe na namba. Nyumba zote zilizojengwa kiholea zitafutiwe utaratibu wa kutambulikana, na endapo nyumba itabomolewa, ni lazima serikali ijulishwe. Kwa hiyo, serikali inatakiwa iwe na data za makazi ya kila raia wake, na endapo raia akihama nyumba, ni wajibu wake kwenda kusahihisha record zake serikalini.
(ii) Kujenda database ya kuaminika kutunza record za raia wote. Database hiyo itunze record za vizazi, vifo, criminal record, mali zake na malipo ya kodi, movements na mambo mengine kama hayo. Mtu anapoondoka nchini vile vikaratasi tunavyojaza airport visiwe vinaishia pale, vinatakiwa viingie kwenye permanent record.
Katika mjadala wa katiba nilikuwa nataka kuongelea hili la majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na utunzaji wa record za raia lakini naona nimechelewa sana. Ukweli ni kuwa kwa sasa, hizi record zetu ziko shaghla baghla sana. Kuna miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nahitaji birth certificate yangu ambayo kiukweli serikali haikuwa na record zake kwa sababu nilizaliwa wakati wa mkoloni huko vijijini ambako hakukuwa na utartibu wa kuandikisha vizazi na vifo. Lakini nilipotaka birth certificate ile nilichotakiwa kufanya ni kuandika ninavyotaka cheti kile kisomeke badala ya wao kutafuta record. Kwa bahati nzuri mimi ni mtanzania, lakini je kwa utaratibu huo unadhani mzamiaji atashindwa kupata cheti hicho? Hii ndiyo maana nasema kuwa kwanza ni lazima serikali isafishe nyumba yake kwa kutengeza data base nzuri na ya kuaminika.
Baada ya maelezo hayo machache, naungana na wale wote wanaopinga kuanzishwa kwa vitambulisho hivi kwa sasa hivi. Tutakuwa tunachezea raslimali tu. Kama serikali itasisitiza kuendelea na mradi huu, ni dhahiri kuwa lengo siyo kuwapa vitambulisho wananchi wake bali lengo ni labda ni kupeana ulaji tu kama walivyohisi wachangiaji wengine.