Tanzania nchi iliyojaa wanafiki na wanaojali matumbo yao

Tanzania nchi iliyojaa wanafiki na wanaojali matumbo yao

Amani iwe nanyi!

Sasa ni rasmi, ICC imeitaarifu dunia kuhusu kupokea rasmi maombi ya uchunguzi dhidi ya Magufuli na serikali ya Tanzania juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na makosa dhidi ya binadamu! Maombi haya yametumwa na ACT Wazalendo, Chama cha siasa, Maria Sarungi, mwanaharakati huku na bado inaonekana Kuna maombi ya bwana Robert Amsterdam yapo njiani wiki hii. Hili ni jambo la hatari kabisa kwa sababu kwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa mwaka huu na reaction za wadau wa maendeleo juu ya uchaguzi huu hadi Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ni dhahili Magufuli na Wakuu wake wa vyombo vya ulinzi na Usalama hasa Diwani Athumani, Simon Sirro na Venance Mabeyo hawatapona kwenye hili.

Kwanini tumefika hapa?
Kwa wenye akili tuliona njia ya kuelekea huku tangu kipindi cha pili cha kikwete ambapo zilianza kutungwa sheria mbaya za kuzuia watu kutoa mawazo huru, utekaji pia ulianza kuota mizizi kipindi hiki. Kilichomuokoa Kikwete na kuonwa vibaya na dunia ni kwa sababu Kikwete pamoja na mapungufu yote aliweza vilivyo kumaintain diplomasia ya ndani na nje ya nchi. Aliruhusu maamuzi ya wananchi yaheshimiwe sehemu mbalimbali hivyo kitendo cha wananchi kupata wabunge waliowachagua kihalali kiliweza kupunguza hasira za wananchi na movement dhidi yake. Kikwete aliweza hadi kuwaiita wapinzani ikulu na kuzungumza nao huku akiripotiwa hivyo hadi na vyombo vya nje. Hili lilimuokoa sana

Alipokuja Magufuli wenye akili tulianza kuona shida mahali maana yeye alionesha ni mtu wa mkono wa chuma zaidi na asiyependa kusikiliza wengine. Alianzisha sheria mbaya zaidi za kubana wakosoaji wake kama sheria za takwimu na za tcra, alitekeleza vibaya sheria za Jinai na kupelekea watu kushtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi bila hata kuangalia matokeo yake. Wapinzani walikamatwa hovyo hadi kufungwa jela.

Mbaya zaidi Magufuli aliingilia eneo hatari zaidi la kujaribu kufanya siasa za ubabe kwa kuwakatalia wananchi machaguo yao. Alianza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na mbaya zaidi amefanya vibaya zaidi kwenye uchaguzi uliopita wa 28 oktoba.

Lawama za haya yote lazima ziende kwa wanafiki watanzania hasa CCM, Idara ya Usalama wa Taifa wanaolipwa kwa kodi za wananchi kwa ajili ya kumshauri Raisi na Serikali na viongozi wastaafu ambao wanauelewa mkubwa wa dunia ilivyo na inavyo operate walioshindwa kumshauri Magufuli na kumzuia sehemu fulani kwenye kufanya mambo ya ajabu. Unafiki wao na kujali kwao matumbo sasa kunaenda kuifikisha nchi hii katika sehemu mbaya zaidi kuwai kutokea.

Kwa sasa ni dhahili watanzania wamegawanyika, kuna kundi ambalo linaona limeshatengwa na halisikilizwi na wao wako tayari kuungana na yeyote yule ili kuiangusha CCM na Magufuli na Kuna kundi ambalo wao ndo wanajiona wana hatimiliki na nchi hii na wanaweza kumfanya yeyote chochote wakati wowote.

Unafiki wao na kujali matumbo yao sasa rasmi unatuangamiza!
Wewe unayejiita mwenye akili, unajua ni hatua gani Marekani ilichukua baada ya mashtaka dhidi yake kuwasilishwa hapo ICC? Kwa kifupi hiyo mahakama ipo hapo kwa ajili ya nchi za kipuuzi ambazo haziwezi kutatua masuala yake zenyewe. Aina ya nchi ambayo wananchi wamewazuia wapinzani uchwara kuijenga kwa kwa mara nyingine mwaka huu.

Mlianza na MIGA sasa mmeweka wimbo mwingine wa ICC. Awamu ijayo sijui mtakuja na nini. Fanyeni kazi acheni kuota ndoto za kitoto.
 
Wewe unayejiita mwenye akili, unajua ni hatua gani Marekani ilichukua baada ya mashtaka dhidi yake kuwasilishwa hapo ICC? Kwa kifupi hiyo mahakama ipo hapo kwa ajili ya nchi za kipuuzi ambazo haziwezi kutatua masuala yake zenyewe. Aina ya nchi ambayo wananchi wamewazuia wapinzani uchwara kuijenga kwa kwa mara nyingine mwaka huu.

Mlianza na MIGA sasa mmeweka wimbo mwingine wa ICC. Awamu ijayo sijui mtakuja na nini. Fanyeni kazi acheni kuota ndoto za kitoto.
Kwa iyo unaifananisha Marekani na Tanzania??? Kwa akili yako kwani Marekani ni mwanachama wa mkataba wa Rome????

Endelea tu kuishi kwa kukariri, kwani ni watanzania au wapinzani wamesema juu ya ICC au ICC wenyewe wametoa statement ya kukiri kupokea malalamiko juu ya Tanzania??
 
Kwa iyo unaifananisha Marekani na Tanzania??? Kwa akili yako kwani Marekani ni mwanachama wa mkataba wa Rome????

Endelea tu kuishi kwa kukariri, kwani ni watanzania au wapinzani wamesema juu ya ICC au ICC wenyewe wametoa statement ya kukiri kupokea malalamiko juu ya Tanzania??
Balaa tupu
 
Wapinzani hamkujiandaa kwenye uchaguzi uliopita hizi mbanga mnazozifanya hazitawasaidia kabisaa tushirikishane kuijenga nchi.
 
Kichwa cha habari kilichotumika kiliwahusisha waTanzania, ( raia wake wengi) kuwa wanafiki, jambo amabalo ninakubaliana nalo. Kwa hiyo nilitegemea mada ijikite kuelezea kinagaubaga tabia hii ya waTanzania walio wengi, na sio hao wachache uliowalenga hapa.

Na kumbuka, hawa sio lazima wawe ndani ya chama cha CCM, hata kule upinzani wapo wengi tu, ndio maana unapoona viongozi wao wanapobinywa, hawa wanafiki hawanyanyui hata kidole kuwatetea viongozi wao.
Hata sisi wengine tusiokuwa na vyama, hala hiyo ipo sana kote nchini.

Mkuu wangu 'Lord' nadhani umetumia 'heading pana sana ikiwa inajumuisha, sio kwa makosa, ila nadhani hapo katikati ya kujieleza ukajikuta unasahau 'ujumla' wa hiyo 'heading' uliyotumia.
Nakubaliana na wewe kwa mtazamo wako. I just wanted to be specific kwenye maelezo
 
Mambo yatapokuwa mambo hao hao wachumia tumbo na wasaka tonge watamkimbia jiwe na hata kumkana kabisa.
 
Back
Top Bottom