Hata Binti Hellen Kijo alionyesha masikitiko dhidi ya Watanzania kwa nini hawakuandamana na sabb za msingi kwa mujibu wake zilikuwepo...
Lakini still hawa wanaojinasibu kuwa ni wakereketwa wa upinzani wana miss this point...
Nashindwa kuelewa upinzani unawezaje kutusua kama kiini cha tatizo tu hawakijui au wanakipuuza
Umeandika vyema, hasa kule juu, ingawaje hapa chini sikuelewa unamaanisha nini.
Ngoja nikupe mfano pengine utakaoonyesha sisi waTanzania tulivyo tofauti sana na pengine ndiyo sababu ya haya yanayotusibu.
Pale Kenya, ukimgusa Raila Odinga kwa aina yoyote tegemea 'reaction' toka kwa wafuasi wake. Ndiyo maana, hata huko nyuma ilipotakiwa apewe kibano kama wanachokipata hapa akina Mbowe, hakuna aliyethubutu kufamfanyia kwa sababu walielewa kitakachotokea sio kizuri.
Hapa akina Mbowe wanaweza kuhangaishwa vyovyote iwapendezavyo watawala bila ya kuwa na hofu ya kitakachotokea kwa wafuasi wao. Usidhani huko CCM kuko tofauti. Leo hii hawa mabosi wanaotupeleka hati hati ikitokea wakawa ndio wanaopewa mbinyo, usitegemee kuwa kuna watu huko CCM watakaofanya lolote; tena usishangae ukakuta wengi wao ndio wakawa washangiliaji wakuu! Huu ndio unafiki ambao mleta mada alitakiwa aujengee hoja, lakini bahati mbaya kaishia kuvungavunga tu hii mada yake.
Na wewe hapa hujaeleza sababu za unafiki huu tulionao waTanzania, pamoja na kumweka Bi Kijo bila ya kutaja na kutoa ufafanuzi wa alichokisema yeye.
Ninakubaliana kuhusu kisingizio cha polisi sio sababu kubwa inayofanya watu wasiamue kuchukua uamzi wa kukataa kama wanaona wanayofanyiwa hayafai. Hakuna polisi wa kuzuia watu waliodhamiria kukataa kuburuzwa na kunyimwa haki.
Kinachoweza kuelezwa ni kwamba viongozi wa upinzani hawajafanya mipango mizuri ya kuwaongoza watu kukataa dhulma. Kwa mfano: hivi vyama vya upinzani vingekuwa vimejiandaa kukata na kuzuia uchafuzi wa uchaguzi na kuweka mipango na kuwaanda wananchi kukataa dhulma hiyo katika vituo vyote walikoondolewa wakala wao nchi nzima na kuzuia kuingizwa kwa karatasi zilizochafua kura za wananchi; huu ungekuwa mwanzo mzuri wa kuwahamasisha wananchi na ingewarahishia wananchi kufanya kazi hiyo bila ya maumivu yoyote toka kwa hao polisi, kwa sababu hakuna polisi wa kutosha kila sehemu ya nchi.