Tanzania: Nchi pekee ambayo wapinzani wanathubutu kunajisi Utawala wa Sheria

kibokomchapaji

Senior Member
Joined
Aug 18, 2017
Posts
165
Reaction score
307
Na Mwamba wa Kaskazini

Nimefuatilia masuala kadhaa katika siku mbili hizi nikashindwa hata kushangaa.

Tanzania mwezi huu inatekeleza kitendo kikubwa sana cha demokrasia ambapo wananchi watachagua viongozi wao wa ngazi za chini kabisa; aina ya demokrasia ambayo hata katika baadhi ya nchi za Ulaya haipo.

Kituko sasa ni wapinzani wetu tunaowapenda sana na tuliowaamini sana kuwa ni watu wanaoenzi demokrasia, lakini loh wemeanza kuonesha usanii katika uchaguzi huu.

Yaani watu wanalilia utawala wa sheria lakini hawataki kuona sheria zinafuatwa!

Tumeona juzi kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani walikatwa kwa kukiuka sheria au taratibu za uchaguzi.

Nilidhani tungeona wapinzani, kama anavyofanya Rais Magufuli kwa watendaji wake wazembe, nao wakienzi misingi ya utawala bora kwa kukemea watendaji wao waliozembea hadi makosa ya kijinga yakajitokeza kwa wagombea wao kutojua namna ya kujaza fomu, lakini hali ni tofauti.

Cha ajabu, wapinzani wetu wa Tanzania wanakimbilia kuona wameonewa. Wanasusia uchaguzi na kutaka waonewe huruma. Kama kawaida yao.

Sanjari na hilo kituko cha pili kinachoendana na hicho ni wapinzani wetu hawa, wanaofahamu fika kuwa zoezi la uchaguzi lina kanuni za kukata rufaa, bila kusubiri rufaa zilizokatwa na wagombea wao, wakabaka tena demokrasia na utawala wa sheria kwa kutangaza kujitoa katika uchaguzi!!

Haya leo rufaa nyingi zimepita na wagombea wao wameshinda, wapinzani hao hao wasiotaka kuona sheria zinafuata mkondo wake wameibuka na kuwatisha wagombea wao walioko tayari kuendelea na uchaguzi. Hii ndio demokrasia wanayoipigania miaka yote?

Nimeshangaa sana, mara wanasema nembo za vyama vyao zisitumike katika karatasi ya kura. Kituko kingine hiki. Kiongozi wa kitaifa unataka kubinya haki za kiongozi wako wa chini? Tena kibabe??Ndio demokrasia mliyoipigania tangu 1992.

Hivi vyama vinasimamia nini hasa katika siasa za nchi hii? Vikishika dola hivi si tumeangamiza hili Taifa?

Yani chama hakina itikadi, hakina falsafa, hakijui sheria zikoje, hakifuati sheria bali kila siku ni kuona kimeonewa tu, unatarajia nini!

Nchi hii imefika hapa kwa sababu ya mifumo inayoenzi demokrasia, utawala wa sheria na hizi ndizo tunu za utawala bora.

Aiseee! Kazi kweli kweli.
 
Vyama vya upinzani Tanzania vinadekezwa mno ingekuwa Nchi za Wenzetu walioendelea vingefutwa vyote
 
Yani vyama vya upinzani siku zote huwa vinakaa mkao wa kulalamika tu. Aina hii ya siasa haitowafikisha popote. Sera wanaweka pembeni wanabaki na kazi moja ya kulalama tuuuu
 
Acha ujinga wewe hii mifano yako yote haina Mashiko , wapinzani wapo sahihi uonevu upo kwani hata kujaza form wapo ambao hawakukosea lakini walienguliwa na pia wapo CCM waliokosea kujaza fomu lakini wamepitishwa wapo, watendaji wa kata hawafanyi kazi kwa mujibu wa sheria bali wanafanya kazi kwa mujibu wa maagizo toka juu, hakuna Uhuru wa kufanya siasa, Magufuli kapiga marufuku mikutano ya siasa kinyume cha sheria, CCM haina nia ya Demokrasia hawataki vyama vya upinzani sasa, chama hakina itikadi hakifuati sheria kivipi?

Wewe umeamua kujiandikia bila kusoma ulichokiandika? Hakuna tunu za utawala bora bali kuna tunu za uchakachuaji mkubwa na kuibaka Demokrasia, usitegemee Teuzi kwa kuleta Uzi kama huu wako usio na tija, wananchi wapo makini wanajua kuwa CCM hii ya sasa haina nia njema na Nchi hii, hata mje na nyuzi 5000 za kujinasua hakuna atakayekubali uongo wenu.
 
Yani vyama vya upinzani siku zote huwa vinakaa mkao wa kulalamika tu. Aina hii ya siasa haitowafikisha popote. Sera wanaweka pembeni wanabaki na kazi moja ya kulalama tuuuu
Yaani wewe unataka vyama vya upinzani vifanyiwe mambo ya hovyo na CCM kisha vikae kimya? aina ipi ya siasa haitawafikisha popote? Kama wapinzani hawana nguvu iweje CCM mnaweweseka kuwafanyia figisu figisu ni kwa nini msiwaachie wananchi waamue kwa uhuru wao?
 
Kwa kweli akili zako zinafanana na jina lako maana hujui ukiandikacho
 
Rais Ni Ccm.
Makamu Wa Rais Ni Ccm.
Waziri Mkuu Ni Ccm.

Halafu Wewe Nimekuteua Unasema Huna Chama.
Yaani Nikupe Nyumba ,Gari na Mshahara Halafu Nisikie Mmemtangaza Mpinzani Kashinda.

Mtoa Mada Unaweza Kunipa Muongozo wa Haya Maneno Yaliyo Tamkwa Na Kiongozi mkubwa Ambae Anatoka kwenye Nchi Unayoiita Serikali yake Inatawala Kwa Mujibu Wa Sheria?.
 
Vyama vya upinzani Tanzania vinadekezwa mno ingekuwa Nchi za Wenzetu walioendelea vingefutwa vyote
Nadhani nyinyi ndio mnashobo wenzenu wapo pembeni nyinyi mnaangaika?

Nadhani tujitaidi kubalanceshobo.
 
Hawa jamaa ni wa ajabu kabisa maana unataka Demokrasia halafu hutaki utawala wa sheria ndio maana yake nini , wanataka huruma kutoka kwa wananchi hilo wasahau hawa.
 
Nadhani itapendeza zaidi endapo utawahimiza viongozi wetu kusimamia haki maana bila haki, amani ya kweli haiwezi kuwepo.
 
Umeamua kuudhihirisha ujinga wako hadharani. Hongera aiseee
 
Wengine walinyimwa fomu. CCM wanapewa fomu uchochoroni. Ofisi za watendaji zikiwa zimefungwa.

Wengine walipewa fomu, wakati wa kurudisha, ofisi zimefungwa. Za wana CCm zinapokelewa mafichoni. Wengine zilipokelewa, zikaenda kujazwa upya ili zionekane zina makosa.

Hivi kwenye mazingira hayo, mtu ambaye ni mzima wa akili, atawalaumu wapinzani?

Kwa upumb.avu uliofanywa safari hii, sioni ni kwa namna gani Rais na msaiduzi waje jafo wanaepuka kila aina ya lawama juu ya dhamira yao chafu kwa Taifa letu. Wamelinajisi kwa kiwango cha pekee.
 
Nenda Russia, nenda Spain,nenda Cuba, and the list goes on
Huwezi kuta Vyama vya upinzani vinaleta fujo zisizo za maana

Wewe unapinga kila kitu,unadharau viongozi,then bado unawafatilia for what?

Mind your own business, acha Watanzania wazalendo tuijenge Nchi yetu,hatuwezi kuisaliti Nchi yetu kama nyie

Taja nchi iliyoendelea then “ikafuta” vyama vya upinzani?

Maccm yakiamua kuharisha kutegemeana na katiba za bongo zao mbovu ni taabu sana!
 
Waliojitua kwenye uchaguzi chafuzi wapo kimya ila sisi wanaccm tunaangaika ..Hii maana yake ni nini?
 
Tulieni dawa iwaingie vizuri ninyi ma ccm.
Mnavyozidi kurukaruka sindano inaweza kuvunjika...ohoooooo shauri lenu!!!
 
Rais Ni Ccm.
Makamu Wa Rais Ni Ccm.
Waziri Mkuu Ni Ccm.

Halafu Wewe Nimekuteua Unasema Huna Chama.
Yaani Nikupe Nyumba ,Gari na Mshahara Halafu Nisikie Mmemtangaza Mpinzani Kashinda.

Mtoa Mada Unaweza Kunipa Muongozo wa Haya Maneno Yaliyo Tamkwa Na Kiongozi mkubwa Ambae Anatoka kwenye Nchi Unayoiita Inatawala Kwa Mujibu Wa Sheria?.

Na Mwamba wa Kaskazini

Nimefuatilia masuala kadhaa katika siku mbili hizi nikashindwa hata kushangaa.

Tanzania mwezi huu inatekeleza kitendo kikubwa sana cha demokrasia ambapo wananchi watachagua viongozi wao wa ngazi za chini kabisa; aina ya demokrasia ambayo hata katika baadhi ya nchi za Ulaya haipo.

Kituko sasa ni wapinzani wetu tunaowapenda sana na tuliowaamini sana kuwa ni watu wanaoenzi demokrasia, lakini loh wemeanza kuonesha usanii katika uchaguzi huu.

Yaani watu wanalilia utawala wa sheria lakini hawataki kuona sheria zinafuatwa!

Tumeona juzi kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani walikatwa kwa kukiuka sheria au taratibu za uchaguzi.

Nilidhani tungeona wapinzani, kama anavyofanya Rais Magufuli kwa watendaji wake wazembe, nao wakienzi misingi ya utawala bora kwa kukemea watendaji wao waliozembea hadi makosa ya kijinga yakajitokeza kwa wagombea wao kutojua namna ya kujaza fomu, lakini hali ni tofauti.

Cha ajabu, wapinzani wetu wa Tanzania wanakimbilia kuona wameonewa. Wanasusia uchaguzi na kutaka waonewe huruma. Kama kawaida yao.

Sanjari na hilo kituko cha pili kinachoendana na hicho ni wapinzani wetu hawa, wanaofahamu fika kuwa zoezi la uchaguzi lina kanuni za kukata rufaa, bila kusubiri rufaa zilizokatwa na wagombea wao, wakabaka tena demokrasia na utawala wa sheria kwa kutangaza kujitoa katika uchaguzi!!

Haya leo rufaa nyingi zimepita na wagombea wao wameshinda, wapinzani hao hao wasiotaka kuona sheria zinafuata mkondo wake wameibuka na kuwatisha wagombea wao walioko tayari kuendelea na uchaguzi. Hii ndio demokrasia wanayoipigania miaka yote?

Nimeshangaa sana, mara wanasema nembo za vyama vyao zisitumike katika karatasi ya kura. Kituko kingine hiki. Kiongozi wa kitaifa unataka kubinya haki za kiongozi wako wa chini? Tena kibabe??Ndio demokrasia mliyoipigania tangu 1992.

Hivi vyama vinasimamia nini hasa katika siasa za nchi hii? Vikishika dola hivi si tumeangamiza hili Taifa?

Yani chama hakina itikadi, hakina falsafa, hakijui sheria zikoje, hakifuati sheria bali kila siku ni kuona kimeonewa tu, unatarajia nini!

Nchi hii imefika hapa kwa sababu ya mifumo inayoenzi demokrasia, utawala wa sheria na hizi ndizo tunu za utawala bora.

Aiseee! Kazi kweli kweli.
Vyama vya upinzani Tanzania vinadekezwa mno ingekuwa Nchi za Wenzetu walioendelea vingefutwa vyote
Yani vyama vya upinzani siku zote huwa vinakaa mkao wa kulalamika tu. Aina hii ya siasa haitowafikisha popote. Sera wanaweka pembeni wanabaki na kazi moja ya kulalama tuuuu
Hawa jamaa ni wa ajabu kabisa maana unataka Demokrasia halafu hutaki utawala wa sheria ndio maana yake nini , wanataka huruma kutoka kwa wananchi hilo wasahau hawa.

Hebu jibuni post #10 hapo.
 
Back
Top Bottom