Tanzania nchi yangu inafurahisha sana!

Tanzania nchi yangu inafurahisha sana!

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu Heshima mbele.

Binafsi kuna kitu kinanishangaza sana. Tanzania ni nchi ambayo raia wanaongoza kwa malalamiko dhidi ya serikali. Si serikali ya raisi yoyote ile iliyowahi kuwepo madarakani watanzania wasilalamike.

Lakini ukifika kwenye uzi kama wa battle Dar es salaam Vs Nairobi ni watu hao hao wanaolalamika wapo mbele kuitetea nchi yao kwa kuwa na maendeleo na uchumi mkubwa kushinda kenya.

Tukirudi kwenye nyuzi zetu ni kulalamika mama anauza bandari, mama anafukuza wamasai na maneno mengi. Ukija mtaani huku ndio kabisa ni kulalamika ugumu wa maisha huku lawama, matusi, kejeli vikienda kwa serikali.

kuna jamaa mmoja mkenya yupo pale city mall ana biashara akawa anasema Tanzania vijana wengi wanahitimu chuo, lakini ukija katika Qualification (ubora) kufiti katika kazi wengi wanapwaya. Huwezi kukuta namba kubwa ya Watanzania hata katika kutafuta fursa za kimataifa au taasisi za kimataifa kama yalivyo mataifa mengine.

Kwa kiasi fulani ni kweli serikali haipo Accountable na transparecy kwa raia wake. Lakini raia hawa hawa wanaolalamika kwamba nchi ni mbovu nenda kawaangalie kwenye uzi wa Dar es salaam vs Nairobi.

Nina rafiki nilimaliza nae advance akaenda kusoma Lugha, alianza kwa kutafuta wanafunzi linkedln, baadae akapata wazungu akawa anawafundisha online na analipwa kwa masaa. Anakuambia Lugha hii hii ya kiswahili ambayo kenya wanajikanyaga kanyaga ndio wamejazana huko wanafundisha wazungu na wanaingiza $ nyingi tu kuzidi Tanzania.

Hata kama serikali inafanya ovyo, lakini watanzania tunapaswa kubadili mentality zetu, tuondokane na unafki kama serikali inafanya vbaya tunasema inafanya vbaya kama inafanya vzuri tunasema inafanya vzuri.

Tuache malalamiko tufanye kazi.

Jumapili njema wana jamii forum.
 
Back
Top Bottom