OffOnline
JF-Expert Member
- Apr 23, 2022
- 644
- 478
Wale wanaopiga kelele kwamba Tanzania tunakopa na tumekopa Sana msikilize huyu Mwamba vizuri ndio utaelewa kwanini Mungu alimleta Rais Samia wakati huu,
Mkuu wa mkoa wa Simiyu akihojiwa na kituo cha redio cha E-FM amedadavua kwa undani Sana swala hili la deni la Taifa,
RC Kafulila anasema "tuangalie mjadala kuhusu ukubwa wa deni na afya ya kukopa.
Nianze kwa angalizo tu kwamba masuala ya kupima ukubwa wa deni na afya ya uchumi wa nchi kukopa ni sayansi ya uchumi na zipo kampuni 75 kimataifa (Global Credit Rating Agency). Maarufu ni3( MOODY'S, S&P na Fitch) ambazo zinamiliki zaidi ya 90% ya kazi hizi duniani.
Lakn kubwa kuliko zote ni MOODY'S. Ambayo inamiliki karibu 45% . Kwa mujibu wa Ripoti ya MOODY'S ya Agust30,2021, Tanzania imepewa daraja la B2 (stable) kwa afya yake ya kukopesheka( creditworthiness) ikiwa juu ya Kenya, Namibia, Msumbiji, Ghana, Ivorycoast, Senegal na nchi nyingi ukanda wa kusini, mashariki na magharibi ya Afrika.
Taasisi hii ya MOODY'S inapima uchumi wa USA, nchi za Ulaya, Asia na kote duniani, inatupa daraja hilo, ni kielelezo kwamba tupo imara na thabiti ktk usimamizi wa deni na uchumi.
Bank ya Dunia Juni2022, tathimini yake imeonesha mzigo wa deni kwa uchumi (GDP), Tanzania ni 31% wakati Kenya ikiwa na mzigo mkubwa wa 64% huku Rwanda 49.8% na Uganda 49.7%.
Nikweli deni ni changamoto kwa nchi nyingi za Afrika. Lakn bado afya ya Tanzania eneo hilo inaonekana imara kwa ulinganisho huo na vipimo vya taasisi zinazoheshimika kwa weledi wa kupima mambo haya dunaini."
#Tanzania tuko vizuri Sana, hongera Rais Samia, asante Kafulila kwa kulifungua Taifa kimtazamo.