Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na kuenea kwa Corona

Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kupambana na kuenea kwa Corona

Status
Not open for further replies.
You Kenyans shut up your mouth
 
Actually nilikosea, nilikua nachanganya tests za Marekani na UK, kule Marekani ndiko wanafanya tests 104,000 kwa siku, na ndio maana namba zao zinapandisha balaa kuzidi mataifa yote duniani kwa sasa wao ndio wanaongoza kwa idadi ya active cases.
Ni muhimu kwa mataifa kupima, pima pima pima huku ukichukua tahadhari, wagundue wote walio kwenye jamii ambao wameambukizwa. Afrika kinachotuokoa kwa sasa ni ile haijafahamika kwanini hiki kirusi kiko lenient kwetu, kusambaa kimesambaa kweli, hiyo sio siri, lakini hatudondoki kama ilivyotegemewa kufa kwa mamilioni, wengi wanacho mtaani lakini kinawatoka hata bila wao kujua walikua nacho, nina uhakika hapa Kenya hatukosi cases 10,000 mtaani.
Mtu alikohoa kohoa tu, au akahisi ovyoo kisha kikamtoka. Nina dada yangu kule Qatar, wamenfungiwa ndani hawatoki, siku tatu amehisi visivyo akiwa ndani, baadaye akapata nafuu.
Hata hawa Wakenya ambao wako karantini baada ya kugunduliwa wanacho, wengi ukifuata wanavyowasiliana na familia zao, mtu haamini anacho maana anajihisi mzima, labda dalili chache hapa na pale lakini hatuna watu kwenye ventilators kama ilivyo UK na mataifa mengine ya wazungu.
Lakini pia hilo sio la kujisifia, ni mapema sana kubweteka, Kenya tunaendelea kujichimbia, shule 900 za bweni zimeanza kuandaliwa kuwa vituo vya karantini, tumekataza misongamano, hatuendi makanisani na kwenye misikiti kama kwenu huko, vilabu vya pombe vimefungwa vyote, hatukusanyi umati kwenye mikutano ya kisiasa kama Makonda wenu huko, na sasa imekua sharti kwa kila Mkenya kuvaa mask kila akienda sehemu yenye msongamano, maana wanasayansi wamebaini kinasambaa hata kwenye hewa kwa kupumuliana na kuongea.
Co tu kwamba Marekani wanapima watu wengi lkn pia idadi ya vifo ni kubwa sana inayopelekea serikali kulazimika kupima watu wengi.
 
Co tu kwamba Marekani wanapima watu wengi lkn pia idadi ya vifo ni kubwa sana inayopelekea serikali kulazimika kupima watu wengi.

Marekani inapaswa iongoze dunia kwa idadi ya vifo maana Wamarekani wanafahamika kama watu walio na uzembe sana kwenye suala la afya, wanaongoza dunia kwa obesity, kisukari, presure na magonjwa mengine mengi yanayotokana na siha mbaya halafu wenyewe wabishi kuliko maelezo.
Mmarekani atapigwa na Corona hadi akome, bora wanapima kwa kasi ili ibainike kinavyotamalaki.
 
Screenshot_2020-04-05-09-32-48.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom