Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Tuseme ulikiwa unafanya biashara maeneo yasiyo rasmi (machinga) ukatolewa na serikali.
Ukatoka na msingi wako wa 2ml kwenda mtaani kuanza biashara unaamua kuuza kiduka cha vitu vidogo vidogo labda na gas za kupikia majumbani.
Kutokana na msingi kuwa mdogo na hali ya biashara mauzo yako yanakuwa hayazidi 60k kwa siku moja.
Kwa kawaida huwa maduka ya mtaani ukiuza 10,000 faida buku, kwa hiyo mauzo yako wastani ni 50k ina maana faida ni 5k tu.
Kodi ya pango ni 30k kwa mwezi umeme ni zaidi ya 10k
Manispaa inakuja kukukamata ukachukue leseni 80,000 kwa mwaka na city service levi 50,000.
TRA wanataka ukachukue TIN ya mlipa kodi kwa mwaka 150k makadirio ya chini kabisa.
Hujakaa sawa serikali ya mtaa inakuja inatakiwa kulipa ulinzi shirikishi 2000 na takataka 15,000 kwa mwezi.
Kama hutaki usifanye biashara
Weka matumizi yako ya kawaida kila siku ya lazma, kuna kutoboa kweli hapo?