Tanzania ni nchi ngumu sana kutoboa bila shortcut, hakuna uwazi

sasa mnataka tuwe marajiri wote nani ataosha magari yenu na kupiga deki nyumba zenu? hayo ma sufuria mtadugua na mikucha yenu hiyo mirefu watoboe wachache tu ili maisha yaende kila mtu akimiliki mzigo wa pesa ni sawa na kuwa maskini wa kutupwa sababu nani sasa atakaye tumwa? [emoji1787] yaani hivi tulivyo ndivyo tunavyo takiwa kuwa ni lazima kundi fulani li nyonywe tu tofauti na hapo maisha yana weza kuwa magumu sana [emoji22]
 
Mkuu hujui kua tunatofautiana? Hujui kuna watu wameridhika na hayo unayoyaongea, kuna watu wanapambana kwa nguvu nyingi sana kua maskini na akina sisi tunapambana kwa njia zozote kua MATAJIRI..ikiwezekana kukaa sehemu moja na Lucifer kufanya mkataba.
Wee jamaa hujapata connection bado?
 
Tanzania hatuchukii ufisadi ila huwa tuna chuki wale waliopo kwenye channel wakati huo.Kila Mtanzania anapenda kuwa fisadi amini kwamba.
Asante mkuu,kwa ugumu huu ni lazima kila mtu atamani kuwa fisadi tu.
 
Tatizo wa Tanzania tunavipaji vya kulalamika sana,mnahisi kuna watu wanakodi nyingi kama marekani kila siku watu wanafilisiwa,mfano mdogo angalia wasanii wakubwa na waliobaki nikilio hatari huko.Tujifunze kulipa kodi na michango mengine kwa serikali
 
Kati ya tozo na mikopo kipi kimejenga madarasa nchi nzima? Halafu tuliambiwa madarasa yatakua na talizi mbona hata siling bod mtihani?
Akili za kuambiwa changanya na za kwako ndio utajua maana ya maneno yako
 
Tatizo wa Tanzania tunavipaji vya kulalamika sana,mnahisi kuna watu wanakodi nyingi kama marekani kila siku watu wanafilisiwa,mfano mdogo angalia wasanii wakubwa na waliobaki nikilio hatari huko.Tujifunze kulipa kodi na michango mengine kwa serikali
Mkuu Africa ndiyo bara pekee ambalo viongozi wake wanakamua ng'ombe maziwa bila kuwalisha vizuri. Huko Marekani ng'ombe wanalishwa vizuri kwanza halafu ndiyo wanakamuliwa maziwa.

Wafanya kazi wanalipwa mishahara mizuri kisha ndiyo wanakatwa kodi. Wafanya biashara wanaandaliwa mazingira mazuri na sera nzuri za biashara kisha ndiyo wanakatwa kodi.

Hatukatai pengine watanzania tunapenda sana kujilalamisha lakini pia serikali yetu imejisahau sana. Kuajiri hawataki watu wakijiajiri wanawabebesha mizigo ya kodi kuzidi vipato vyao.
 
Tatizo wa Tanzania tunavipaji vya kulalamika sana,mnahisi kuna watu wanakodi nyingi kama marekani kila siku watu wanafilisiwa,mfano mdogo angalia wasanii wakubwa na waliobaki nikilio hatari huko.Tujifunze kulipa kodi na michango mengine kwa serikali

Kwahio ndo tuseme rushwa imekuja kutuokoa kiasi fulani sio?

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
Rushwa ni tamu ukiitoa wewe ila akutolee mtu ndio utaona ubaya wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…