Tanzania: Nyumba nyingi dining room zinajengwa, ila hazitumiki

Tanzania: Nyumba nyingi dining room zinajengwa, ila hazitumiki

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Wakuu,

Nimefanya utafiti usio rasmi.

Ndani ya Tanzania yetu. Nyumba nyingI Sana zinajengwa zikiwa na sehemu ya dinning room.

Cha kushangaza, nyumba nyingi Sana Dinning room zimegeuzwa eneo la wazi na lisilotumika kwa ajili chakula Kama ilivyokusudiwa.

Wengi Sana Nimeona bado wana utamaduni wa kulia chakula sebleni (living room).

Hii imekaaje, nini MTIZAMO Wako kuhusu ili suala.

My take:
Kama mtu hapendi kulia chakula dinning room, ni Bora tu kwenye ramani yake asiijenge.

Ni upotezaji wa rasilimali fedha kujenga kitu usichokua na matumizi nacho.
 
Tatizo kubwa ni uchumi wa kati. Baba na mama wanakuwa hawapo karibu ili wale na watoto. Wanakuwa busy kutafuta fedha.

Kuna jamaa aliniambia nchi ya uswisi inaheshimu familia kula pamoja na ndiyo maana muda wa jioni maduka yanafungwa ili kulipisha hilo zoezi. Sina uhakika kama ni kweli.
 
My take:
Kama mtu hapendi kulia chakula dinning room, Ni Bora TU KWENYE ramani yake asiijenge.
Ni upotezaji wa rasilimali fedha KUJENGA kitu usichokua na matumizi nacho.
Kuna kuamua kuuza, kupangisha au kubadili matumizi ya nyumba kulingana na wakati.

Kwahiyo usemalo si sahihi.

Halafu hao wanaokula chakula sebuleni mbona wastaarabu sana, wengine baada ya kupata ration yake ya chakula anaingia chumbani.
Watanzania wengi hutumia dinning room kwa matukio maalum zikiwemo siku wametembelewa na mgeni.
 
Kula pamoja mezani na kusali pamoja ni vitu muhimu ambavyo vinasahaulika katika jamii. Mnapo sali pamoja ni rahisi watoto kukumbuka sala hata wakiondoka nyumbani. Kula pamoja kunafundisha watoto table manners.

Tatizo linaanza pale uhusiano wa wazazi unapoanza kuyumba. Baba na mama hawako vizuri na hawawezi kukutana mezani.

Wakati mwingine baba anaangalia mpira na chakula chake apelekewe sebuleni. Mama anaangalia Instagram na yeye anataka chakula chake kiachwe jikoni atakula atakapokua tayari.
 
Kuna kuamua kuuza, kupangisha au kubadili matumizi ya nyumba kulingana na wakati.

Kwahiyo usemalo si sahihi.

Halafu hao wanaokula chakula sebuleni mbona wastaarabu sana, wengine baada ya kupata ration yake ya chakula anaingia chumbani.
Watanzania wengi hutumia dinning room kwa matukio maalum zikiwemo siku wametembelewa na mgeni.
Sawa sawa, point Muhimu Sana hiyo
 
Tatizo kubwa ni uchumi wa kati. Baba na mama wanakuwa hawapo karibu ili wale na watoto. Wanakuwa busy kutafuta fedha.

Kuna jamaa aliniambia nchi ya uswisi inaheshimu familia kula pamoja na ndiyo maana muda wa jioni maduka yanafungwa ili kulipisha hilo zoezi. Sina uhakika kama ni kweli.
Kula na familia, linaiweka familia pamoja
 
Cha kushangaza baba anasema nileteeni chakula changu hapa huko watoto wako wanasumbia sana. Wakati watoto uliwazaa mwenyewe na wanauliza maswali ili waelewe dunia.
Kabisa,
hapo umenigusa hata Mimi pia.

Nlipokuwa mdogo nilikuwa sipendi kula chakula dinning pamoja na familia.

Sababu kubwa ilikuwa kumkwepa mama,

Yaani MDA wa kula pale dinning hasa Usiku,
Ndo MDA unaanza kusemwa makosa yako Yote uliofanya siku nzima.

Na Kama majibu hayaridhishi, baaada ya chakula Ni stiki.
 
Dinning ni kwa ajili ya wanaokula( dinning)Sio kula snacks uende dinning.Wengi tunaishi kwa snacks na sio meal

Kama nakuona na bande lako la ugali mkavu na maji ya kunywa as if una keki na juice
 
Sebuleni kuna tv wengi wanasave time. Anakula while anaangalia movies...habari...ila hii ni tabia mbaya maana muda wa kula hutakiwi kufanya chochote hata kuzungumza.

Ila leo nikila mkono mmoja nina simu.
 
Kabisa,
hapo umenigusa hata Mimi pia.

Nlipokua mdogo Nlkua sipendi kula chakula dinning pamoja na familia....
Dah, mama yako anafanana sana na wangu! Aisee kwa wiki ikitokea sijapigwa basi ni Mara mbili au tatu, asipokua bize na mambo yake basi wiki nzima atatembeza stick, ikifika jioni unaanza kuwaza Leo nitakua nimekosea wapi.. Wife nae anatabia hii, hana dogo, yaani muda wa kula ndio anaanza kuhukumu kesi za watoto! Nakerekaga sana.
 
Kula pamoja mezani na kusali pamoja ni vitu muhimu ambavyo vinasahaulika katika jamii. Mnapo sali pamoja ni rahisi watoto kukumbuka sala hata wakiondoka nyumbani. Kula pamoja kunafundisha watoto table manners...
Mpira hauwezi kuwa kigezo cha kuondoa ustaarabu. Mbona Dinning room nyingi zina TV nazo? Afterall sitting room hakupaswi kuwa na TV ni bora ikakaa katika chumba chake ili wapenzi wa TV wakae huko. Siamini kama mgeni kwa sasa anataka kuja kwako kuangalia TV kama wakati wa Enzi za Mwalimu, kuvinjali video.
 
Wanaume hawatakiwi kukaa pamoja na wanawake kwenye meza ya chakula.

Nyumba lazima itenganishe sebule ya wanawake na wanaume.

Mtoto wa kiume afundishwe ya kiume kwenye kikome na mtoto wa kike afundishwe ya kike huko jikoni na mama zake.
 
Back
Top Bottom