Tanzania: Nyumba nyingi dining room zinajengwa, ila hazitumiki

Tanzania: Nyumba nyingi dining room zinajengwa, ila hazitumiki

Dah, mama yako anafanana sana na wangu! Aisee kwa wiki ikitokea sijapigwa basi ni Mara mbili au tatu, asipokua bize na mambo yake basi wiki nzima atatembeza stick,ikifika jioni unaanza kuwaza Leo ntakua nimekosea wapi.. Wife nae anatabia hii,hana dogo, yaani muda wa kula ndio anaanza kuhukumu kesi za watoto! Nakerekaga sana.
Mwambie, na umwambie ni kiasi gani hiyo tabia ya kusemwa wakati wa kula imekuathiri.

Wasitumie chakula kama adhabu, kuwa "nitampata tu wakati wa kula".

Kuna watu hawana msisimko na chakula, wanakula tu ili wasife, sababu ya athari za kimtazamo walizozipata wakati wa makuzi yao. Mfano nina rafiki yangu hali nyama kabisa, anasema alivyokuwa mdogo alikuwa anapenda nyama sana kiasi cha kudokoa akikuta, siku akafumwa na Bi mkubwa wake, alipigwa kipigo cha mbwa koko kiasi kwamba akahitimisha kuwa yeye na nyama basi kuanzia siku hiyo, hadi leo hii anaziangalia tu nyama hali. Ni kastori chakuchekesha lakini ni cha kuhuzunisha sana.
 
Mwambie, na umwambie ni kiasi gani hiyo tabia ya kusemwa wakati wa kula imekuathiri.

Wasitumie chakula kama adhabu, kuwa "ntampata tu wakati wa kula".

Kuna watu hawana msisimko na chakula, wanakula tu ili wasife, sababu ya athari za kimtazamo walizozipata wakati wa makuzi yao. Mfano nina rafiki yangu hali nyama kabisa, anasema alivyokuwa mdogo alikuwa anapenda nyama sana kiasi cha kudokoa akikuta, siku akafumwa na Bi mkubwa wake, alipigwa kipigo cha mbwa koko kiasi kwamba akahitimisha kuwa yeye na nyama basi kuanzia siku hiyo, hadi leo hii anaziangalia tu nyama hali. Ni kastori chakuchekesha lakini ni cha kuhuzunisha sana.
Ni kweli Mkuu, tushaongea sana ila mwenzangu naona ipo kwenye damu yake.!

Inaonekana kina mama wengi wanapenda haka kautaratibu.
 
Wakuu,

Nimefanya utafiti usio rasmi.

Ndani ya Tanzania yetu. Nyumba nying Sana zinajengwa zikiwa na sehemu ya dinning room.

Cha kushangaza, nyumba nyingi Sana Dinning room zimegeuzwa eneo la wazi na lisilotumika kwa ajili chakula Kama ilivyokusudiwa.

Wengi Sana Nmeona bado wana utamaduni wa kulia chakula sebleni (living room).

Hii imekaaje, nini MTIZAMO Wako kuhusu ili suala.

My take:
Kama mtu hapendi kulia chakula dinning room, ni Bora tu kwenye ramani yake asiijenge.

Ni upotezaji wa rasilimali fedha kujenga kitu usichokua na matumizi nacho.
Dinning Table ya kazi gani na wakati chakula ushapakuliwa kwenye sahan!? Hizi tamaduni tumecopy bila kuelewa maana yake..

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Kula pamoja mezani na kusali pamoja ni vitu muhimu ambavyo vinasahaulika katika jamii. Mnapo sali pamoja ni rahisi watoto kukumbuka sala hata wakiondoka nyumbani. Kula pamoja kunafundisha watoto table manners.

Tatizo linaanza pale uhusiano wa wazazi unapoanza kuyumba. Baba na mama hawako vizuri na hawawezi kukutana mezani.

Wakati mwingine baba anaangalia mpira na chakula chake apelekewe sebuleni. Mama anaangalia Instagram na yeye anataka chakula chake kiachwe jikoni atakula atakapokua tayari.
Na watoto wanataka wapelekewe vyakula vyumbani mwao, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acha dharau mkuu...kama wew unakula snack ni wew.unataka nambia wali maharage mchicha kachumbari na kipandw cha tikiti bila kusaahau maji ya kunywa bariiid ni snacks
Niambie wewe...Anyway ni chakula ambacho hakihitaji mbwembwe kukila.
 
Kabisa,
hapo umenigusa hata Mimi pia.

Nlipokua mdogo Nlkua sipendi kula chakula dinning pamoja na familia.

Sababu kubwa ilkua kumkwepa mama,

yaani MDA wa kula pale dinning hasa Usiku,
Ndo MDA unaanza kusemwa makosa yako Yote uliofanya siku nzima.

Na Kama majibu hayaridhishi, baaada ya chakula Ni stiki.
Umenikumbusha mbali Sana niliwahi kugoma kula dinning brazaa nilicharazwa muda mfupi uliofata
 
Hiyo Kitu utotoni home tumetumia sana then after life with TV aliisha mara moja ilikuwa kazi yake msosi unawekwa kisha watu wanapakua and streight to the sofa.. ukiwa na wageni lazima tu utumie Dinning room so wacha iwepo sababu ni kama kitambi hakiumi wala hakiwashi jenga usiache kamwe
 
Dinning ni kwa ajili ya wanaokula( dinning)Sio kula snacks uende dinning.Wengi tunaishi kwa snacks na sio meal
Mkuu ubwabwa na maharage ni snacks?

Mi nafikiri ni kwasababu ya mfumo wa "kujisevia" unachangia sana

mtu anapakua kwenye sahani yake tena pale kwenye meza ya dining anaenda kula popote, wengine chumbani, mwingine sebuleni, mwingine anakaa nje.. hahahaha.

Lakini pia tatizo ni muda wa familia kujumuika pamoja ratiba haziendani,
 
Wengi huacha wazi kusubiria ndugu zao wa mjini wakija wawe wanalala hapo kwa vile vyumba na idadi ya jinsia havitoshi.
 
Wakuu,

Nimefanya utafiti usio rasmi.

Ndani ya Tanzania yetu. Nyumba nying Sana zinajengwa zikiwa na sehemu ya dinning room.

Cha kushangaza, nyumba nyingi Sana Dinning room zimegeuzwa eneo la wazi na lisilotumika kwa ajili chakula Kama ilivyokusudiwa.

Wengi Sana Nmeona bado wana utamaduni wa kulia chakula sebleni (living room).

Hii imekaaje, nini MTIZAMO Wako kuhusu ili suala.

My take:
Kama mtu hapendi kulia chakula dinning room, ni Bora tu kwenye ramani yake asiijenge.

Ni upotezaji wa rasilimali fedha kujenga kitu usichokua na matumizi nacho.
Kweli
Hata jikoni unakuta fundi umeme anakununulisha cooker switch wakati wengi siku hizi wanatumia gas.
 
Cha kushangaza baba anasema nileteeni chakula changu hapa huko watoto wako wanasumbua sana. Wakati watoto uliwazaa mwenyewe na wanauliza maswali ili waelewe dunia.
Sometimes watoto wanasumbua kweli, hasa wa kiume, japo si kwa ubaya lakini utakuta wanakuzingua ilhali wewe upo deep na mambo yako ya kimaisha.

At times huwa naagiza msosi uletwe chumbani kabisa maana najua huko watagonga mlango na naweza kudeny acces ya wao kuingia pia.
 
Umenikumbusha mbali Sana niliwai kugoma kula dinning brazaa nilicharazwa mda mfupi uliofata
Wee Acha TU,
kibaya zaidi ukute siku iyo amepikwa pilau kuku.

Ladha yote ya chakula inapotea
 
Back
Top Bottom