wale mliofika ulaya si mnasemaga kule hakuna mambo ya kudeka deka kila mtu anaishi kivyake? kumbe wanaheshimu mambo ya familia? sasa mbona tunadanganyana huku Mpanda.Tatizo kubwa ni uchumi wa kati. Baba na mama wanakuwa hawapo karibu ili wale na watoto. Wanakuwa busy kutafuta fedha.
Kuna jamaa aliniambia nchi ya uswisi inaheshimu familia kula pamoja na ndiyo maana muda wa jioni maduka yanafungwa ili kulipisha hilo zoezi. Sina uhakika kama ni kweli.
mzee hili li ugali langu la dona nalokula nalo ni snacks?Dinning ni kwa ajili ya wanaokula( dinning)Sio kula snacks uende dinning.Wengi tunaishi kwa snacks na sio meal
daah. kuna wakati nafika nyumbani niko hoi bin taabani vibarua huko nilikotoka vinataka kunitoa roho. mara vingine vimebuma na vingine nimepigwa hasara na faini. sasa napofika nyumba watoto wanaanza kuuliza hiki na kile nachanganyikiwa. nachofanya naoga fasta chakula kitanikuta chumbani nalia chini kwenye mkeka, mto nashusha hapo hapo hata kitandani sipandi nalala kama nyoka.Cha kushangaza baba anasema nileteeni chakula changu hapa huko watoto wako wanasumbua sana. Wakati watoto uliwazaa mwenyewe na wanauliza maswali ili waelewe dunia.
Ile mara nyingi ipo kwa ajili ya Oven zinazobeba umeme mwingikweli
Hata jikoni unakuta fundi umeme anakununulisha cooker switch wakati wengi siku hizi wanatumia gas.
Mimi shughuli inaishia bar...Mimi huwa nalia jikoni.
Sio kwamba na dining room pawe na TV! Huko living room wengi wanafuata TV!! Kama ni aina ya viti, basi viwekwe dining pia ingawaje sio sehemu yake!Wakuu,
Nimefanya utafiti usio rasmi.
Ndani ya Tanzania yetu. Nyumba nying Sana zinajengwa zikiwa na sehemu ya dinning room.
Cha kushangaza, nyumba nyingi Sana Dinning room zimegeuzwa eneo la wazi na lisilotumika kwa ajili chakula Kama ilivyokusudiwa.
Wengi Sana Nmeona bado wana utamaduni wa kulia chakula sebleni (living room).
Hii imekaaje, nini MTIZAMO Wako kuhusu ili suala.
My take:
Kama mtu hapendi kulia chakula dinning room, ni Bora tu kwenye ramani yake asiijenge.
Ni upotezaji wa rasilimali fedha kujenga kitu usichokua na matumizi nacho.
Wakati wa kula ni muda wa Aman sana kwangu hakuna kuongea makosa Nani kafanya nn au kipi kimekuaje tukimaliza tunapeana abc za baadaye, kama ni usiku ibada inafuataKabisa,
hapo umenigusa hata Mimi pia.
Nlipokua mdogo Nlkua sipendi kula chakula dinning pamoja na familia.
Sababu kubwa ilkua kumkwepa mama,
yaani MDA wa kula pale dinning hasa Usiku,
Ndo MDA unaanza kusemwa makosa yako Yote uliofanya siku nzima.
Na Kama majibu hayaridhishi, baaada ya chakula Ni stiki.
Kula huku utani wa mbali mzuri sana au unashusha kastori kazuri yaaan watoto watatamani kula na ww kila mudaSebuleni kuna tv wengi wanasave time. Anakula while anaangalia movies...habari...ila hii ni tabia mbaya maana muda wa kula hutakiwi kufanya chochote hata kuzungumza.
ila leo nikila mkono mmoja nina simu....
Falsafa ya modern architecture imeegemea towards "open" structures and spaces majumbani na ofisini .majumbani kwa mfano Kitchen,living,na dining inakaribia a single space mnaonana na kupiga gumzo .Pia maofisini idara zote zipo single open space badala vyumba vyumba. Hiii inachochea team work kutimiza malengo na mahusiona mazuri idara na idara.Sebuleni kuna tv wengi wanasave time. Anakula while anaangalia movies...habari...ila hii ni tabia mbaya maana muda wa kula hutakiwi kufanya chochote hata kuzungumza.
ila leo nikila mkono mmoja nina simu....
Ni jamii na jamiiWanaume hawatakiwi kukaa pamoja na wanawake kwenye meza ya chakula.
Nyumba lazima itenganishe sebule ya wanawake na wanaume.
Mtoto wa kiume afundishwe ya kiume kwenye kikome na mtoto wa kike afundishwe ya kike huko jikoni na mama zake.
Hata kama ni makande Tu mkuu lazima iwe hivyoYani upike tembele na ugali uhangaike kupeleka dinning room!?
unapiga juu kwa juu
Facts tupu nimekuoenda bureKula pamoja mezani na kusali pamoja ni vitu muhimu ambavyo vinasahaulika katika jamii. Mnapo sali pamoja ni rahisi watoto kukumbuka sala hata wakiondoka nyumbani. Kula pamoja kunafundisha watoto table manners.
Tatizo linaanza pale uhusiano wa wazazi unapoanza kuyumba. Baba na mama hawako vizuri na hawawezi kukutana mezani.
Wakati mwingine baba anaangalia mpira na chakula chake apelekewe sebuleni. Mama anaangalia Instagram na yeye anataka chakula chake kiachwe jikoni atakula atakapokua tayari.