wacha kujiliwaza mkuu...huwez ukawadanganya waafrika mashariki wote...the Rwandese guy is just telling you the truth...ila naona ni ngumu kumeza...
Nimegundua uzalendo, hasira za kuona Tanzania inaendelea kwa kasi na flustrations za maisha zinakusumbua zaidi kuliko kujenga hoja zenye mashiko, huo ndio ukweli ulio wazi japo ni uchungu kumeza, ukiondo GDP ambayo Kenya iliifikia zamani, kwanza kwa sababu Kenya iliendelezwa na wakoloni wa kiingereza ikilinganishwa na nchi zingine za EA, na baada ya uhuru Kenya iliendelea na kasi ya kujenga uchumi wake haikusima kufanya marekebisho yoyote ya kimuundo wa kisiasa wala kijamii, ilipokea kijiti toka kwa mabepari na kuendelea na ubepari(soma the Wako report ya Kenya).
Tanzania ilipowekwa chini yw uangalizi wa waingereza baada ya vita kuu ya kwanza toka kwa mjerumani, waingereza waliitumia kama sehemu ya kuzalisha mali ghafi za mazao kwa ajili ya viwanda vyao vilivyokuwepo Nairobi, hawakushughulika kuweka miundombinu yoyote kwa kujua kwamba ipo siku wataondoka wakati wowote, na baada ya kupata uhuru, Nyerere hakuanza kujenga uchumi kwanza, yeye aliamua kujenga umoja wa taifa kwanza, alitaka kuunganisha nchi iwe moja na kuondoa tofauti za matabaka ya watu yaliyowekwa na wakoloni, kusitokee mtu kujiona bora kutokana ama na rangi yake, kabila au dini yake, kipato au elimu yake, au cheo chake. Tulifundishwa maneno mengi kama vile; binadamu wote ni sawa, rushwa ni adui wa haki sitopokea wala kutoa rushwa, cheo ni dhamana, watanzania wote ni ndugu zangu na africa ni moja.
Katika kipindi hiki cha kujenga utaifa, sio tu kwamba tulikua hatuzalishi bali tulitumia fedha chache tulizopata kugharimia shughuli hii ya kujenga utaifa na uzalendo kwanza, Nyerere aliamini bila umoja wa kitaifa hakutokua na amani wala uzalendo wa kweli, vitu ambavyo ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara na endelevu.
Msumari wa mwisho katika kusambaratisha uchumi wa Tanzania ni pale Nyerere alipoanza vita vya ukombozi kusini mwa Afrika na kumalizia vita vya Uganda, kumbuka kipindi chote hiki Kenya iliyokua mbele tokea enzi za ukoloni ilikua inaendelea kujenga uchumi wake, haijawahi kusimama kupitia lolote lililopunguza kasi ya uchumi wake(Soma article ya Dr. David Ndii).
Sent using
Jamii Forums mobile app