Pundit,
Lakini unapiga kura ktk mfumo ambao ni wa Kifisadi!...
Mkuu nifahamu hapa, Mafisadi wote mimi nawaita Wanyapala.. kwa hiyo unamchagua/humchagui nyapala ambaye unajua kabisa kwamba bado wewe utabakia ktk mtumwa... tofauti ya mtazamo wako ktk kumchagua Nyapala haiwezi kukuletea mabadiliko ya Utumwa..
Now, wewe kama mtumwa umefanya nini kuondokana na Utumwa kwani waafrika ndivyo tulivyo inabeba mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwepo ktk kundi la mbuzi ama kondoo.
Wapo wanyapala, watumwa na wengine waliendesha maisha yao hivyo hivyo chini ya kutawaliwa...
The all picture ni kwamba huna Uhuru kamili hata kama hukuchagua fisadi... umefanya nini kuondokana na hali hiyo!
I just love JF!
Back to the "Ndivyo tulivyo" Huu msemo, ni dhahiri ni wa kebehi sana. Lakini why cant we prove otherwise? Kuna aliyesema eti yeye ni tofauti na bunch of irresponsible people! Ok, granted. Tofauti yako ni ipi? kujua kizungu/kiiengereza na kukiandika vizuri au nini, Kuishi ulaya au America? kusoma mpaka PhD Oxford au kipi haswa?? NOTE: Iam not saying kwamba wewe siyo tofauti, lakini nauliza hiyo tofauti ni ipi? Ambayo inaweza kumkomboa mwafrika mwenzio?
Jiulize waafrika wote universally tuna attribute ya umaskini! Nenda angalia waafrika wanaoishi nje na bara letu ndo maskini wa kutupwa huko waliko..iwe brazil, Ulaya, USA kwenyewe na ofcourse HAITI! Waafrica wako associated na umskini..we can spin it the way we want..ila ndiyo ukweli huo! Ukisema wazungu ndivyo walivyo..unafikiri kuna atakayenuna au kulalamika? Hapana kwa sababu ndio ukweli wao attribute yao kubwa ni mafanikio, hata kama wako wachache ambao ni homeless! Lakaini mafanikio yanaonekana. Ndo maana wengi wetu walipotaka kwenda kusoma nje, HAKUNA ALIYEOMBA VISA YA KWENDA HAITI! kILA MTU ALITAKA AENDE KWENYE NEEMA.
Friends tuache longo longo hapa. Waafrica ndivyo tulivyo kwa sababu WE JUST DONT GET IT. What is insanity? Einstein alisema; It is doing the same thing again and again expecting different results. Iwe ni demokrasia mbovu ya kukataa matokeo ya chaguzi tulizoziitisha wenyewe..ni Africa..na kwingineko waliko weusi..
Tumekuwa na viongozi ambao wametupeleka kwenye lindi la umaskini lakini tunawachagua hao hao. Tulililia uhuru kwamba tunanyonywa..lakini leo sisi ndo tunawakabidhi mali mchana kweupe... Tulisema kwamba wakoloni walikuwa wananyanyasa wananchi wetu, leo hii sisi ndo tunawanyanyasa hao raia vibaya mno..na wao wanachekelea tuu... Tulisema akina Mangungo walituuza kwa akina Karl Peters kwa vile hawakusoma, lakini leo wanaotuuza wanashahada za harvard na vyuo vingine mahiri duniani. Haya watu wanaiba billions ambazo zingesaidia wote, lakini hapa hapa tunakuja kuwatetea simply because aliyeiba ni mjomba au baba na wewe ulipatapo, leo Africa viongozi wanakuja kutuomba kura na sisi tunawapa na baada ya hapo tunaanza kulalamika, Tunasema kwamba turudishe wasomi tojka ulaya ndo waje kutusaidia kwa vile wana "exposure" hao hao ndo wanatutenda... .The list is endeless.
Ok, ingekuwa ni isolated cases nadhani Nyani angekuwa na lake jambo kutu-generalize. Lakini je, nenda Zimbabwe, Sierra Leone, Liberia, Kenya, Congo, Guine etc..we ALL face similar problems!
Perhaps huo msemo unauma sana, labda unaweza kutufanya tukabadilika.
Inauma sana kukubaliana na huo msemo, alkini jee, alternative yetu ni ipi? au ni kuendelea kuilaumu historia tuu.
Subiri na madudu ya JK yooote na umasikini unaotishia uhai wa watanzania..come 2010. Tutamchagua huyu huyu kwa landslide.
Mwenye kubisha na abishe but Iam with Mkandara on the same wevelength!