joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Tatizo ninaloliona kwako ni kudhani kwa sababu Kenya imefanya au imejenga kwa phases, basi hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo, hapana jaribu kufungua masikio usikilize watu au nchi nyingine zinafanyaje, hii inaweza kusaidia kuboresha utendaji wenu siku zijazo ili msirudie makosa.Nimekua busy sana, kuhama nyumba, kazi mpya laptop mpya...nk
Anyway nikirudi vizuri mtandaoni nitajaribu ku reply kulingana na timing...
Anyway ninachosema kuhusu WB, kama unataka mmalize ujenzi wa SGR yenu 2030 basi endeni na WB, kumbuka SGR sio mradi wa mpigo mmoja kama BRT au bandari, Sgr ni mradi wa phases,sections...etc pesa hazitatolewa kwa hatua moja mtakua mnapewa nusu mwaka huu alafu mnaambiwa mgonje tena mwaka ujao ndo mpewe pesa za section 2,3..
Kama SGR ya Tanzania ingejengwa kwa mtindo wa phases kama ya Kenya, ingachukua zaidi ya miaka ishirini kukamilika, kwa sababu urefu ni zaidi ya 2000km, ukijumlisha na reli ya kusini kwenye chuma na coal, Tanzania phases zote zinaenda kujengwa kwa wakati mmoja, kwa hiyo pesa lazima ikusanywe kwa pamoja, zitapishana miezi michache tu ili kupisha kipindi cha kumpata contractor wa kujenga hiyo phase husika kwa sababu kila phase inajitegemea kwa hiyo tenda inatangazwa separately, Tanzania phase maana yake ni reli tofauti, inatangazwa tenda na watu wanaomba, sio hadi phase moja ikamilike ndiyo ianze ingine, hazihusiani wala hazisubiriani. Kiufupi BRT inajengwa kwa mtindo sawa sawa na SGR ya Kenya.
Kama nilivyokuambia, WB walishasema hawatotoa pesa kwa ajili ya SGR ya Tanzania kwa sababu wametoa pesa ya kukarabati reli ya zamani, ila pesa ya WB ikipatikana ni tamu na ulipaji wake ni wa muda mrefu na riba ni ndogo sana.