Usiongee ukubwa wa uchumi, ukubwa wa uchumi unaweza kutokana na ukubwa wa nchi na wingi wa watu tu.
Kwa mfano, ukilinganisha nchi kama Tanzania yenye watu milioni 64 na nchi kama Croatia yenye watu milioni 4, ni rahisi nchi yenye watu milioni 64 kuwa na uchumi mkubwa, lakini, je, ukiuchukua huo uchumi mkubwa na kuugawanya kwa watu milioni 64 utapata wastani mkubwa kuliko ukiuchukua uchumi mdogo wa nchi ya Croatia ukaugawanya kwa watu milioni 4?
Mtu wa Croatia kwa wastani alijenga uchumi kwa US $ 17,685 kwa hesabu za mwaka 2021.
Mtu wa Tanzania kwa wastani alijenga uchumi kwa US $ 1,099 kwa hesabu za mwaka 2021.
Hapo sasa hata Tanzania ikiizidi Croatia kwa size ya uchumi, utasema imeizidi Croatia kiuchumi?
Ongelea GDP per capita, hapo ndipo utaona wastani wa mchango wa kila mtu katika uchumi.
Ukiongelea GDP per capita ndiyo utaona ufanisi wa uchumi.