Tanzania sasa ina uchumi mkubwa kuliko baadhi ya nchi za Ulaya

Mbona huo uchumi hauakisi Maisha ya watanzania?au unakua Kwa wanaccm Tu?
Hao ccm wenyewe wachache ndio wanakula nchi wapo hao wengine ni walala hoi ndio maana wabunge wakirudi majimboni wanagawa 10k wanapewa support angalia mtu kama nape hana msaada wowote kwa wananchi anatetea makampuni ya simu ila walivyo wapumbavu wananchi wake watampigia tena kura wakati now wanaumia kama kawaida
 
Ndiooo ujinga watanzania mbunge hajafanya kitu wala hajatetea maslahi ya wananchi katetea makampuni yamewanyonya wananchi kapewa ten percent yake uchaguzi ujao unamchagua tena watanzania tutajielewa lini
 
Manzanita anatamani kuzamia Crotia ila hakuna m Crotia anaetaka kuzamia Tanzania ili haje kutafuta maisha.

Unakumbuka ile barua ya Msando kwenda Ubalozi wa Marekani kipindi kile Pompeo amampiga Makonda stop kwenda kukanyaga USA?
Vijana wetu mna vituko sana.
 
Takwimu hizo hukua tu kama mtoto mdogo hata wakati wa Mwendazake uchumi ghafi wa nchi ulikuwa.
 
Mbona hata kutoa uji kwa watoto shule za msingi imeshindikana, ,,
 
Sababu tuna population kubwa but interms of per capita income tuko chini ,data za economic growth sio za kujivunia sana sababu huangalia pato la jumla na sababu tuna population kubwa tutaonekana tupo juu tu
 
Umenena kweli,nadhani huyo kakurupuka toka bafuni tu bila hata taulo. Wachambuzi wengine uchwara na uchawa tu.
 
Angalia vyote viwili, ukubwa wa uchumi na ubora wa maisha.
 
Wakati mwingine ukisoma posts Kama hizi unaweza kudhani nchi inawatu na viongozi waliolaaniwa. Nchi ya watu wasiofikiri na kama wanafikiria basi wanafikirishwa na wanaotaka sifa au wameamua kusifia wafikie kusudio lao.
Uchumi wa nchi unapimwa kwa ongezeko la kila mwaka la ASILIMIA na sio ongezeko la pato la taifa kutoka point moja hadi nyingine. Sasa kama mwendakwake aliacha pato la taifa likiwa 70tr leo tuna 85tr ni sawa na kusema uchumi umekua kwa chini ya 2%. Tulitakiwa tulie na kuhudhunika kwa asilimia hizi. Tukisifia tunaoneka wote Tz ni mbumbumbu wa uchumi. Ajabu hata hao wenye dhamana ya kuendesha uchumi wa nchi yetu hawana wanachokijuwa kuhusu macroeconomics na microeconomics. Nao wanasifia anguko letu.
Sasa let us assume uchumi umekua kama anavyodai mleta uzi huu. Hilo ongezeko limeongeza nini kwenye standard of living ya wananchi? Tumuulize pia swali lifuatalo, je kilimo na informal sector ambako ndiko the majority wako employed kumechangia asilimia ngapi za ongezeko hilo la pato la taifa? Maana pato la taifa letu lisipongezwa na kilimo na informal sector halina maana yeyote, well isipokuwa maana ya kisiasa.
Tatizo tulilorithi nchi yetu ni kuwapa madaraka wanasiasa wenye elimu ya kuungaunga ya kuongoza uchumi wetu. Mbunge anamaliza chuo kwa kubabaisha na kununua degree anapewa uchumi wa watu milion 70 kuupngoza. Research yake iliyompa degree ameificha na yeyote atakayethubutu kuifichua atajuta kuwa duniani.
Tuna wachumi wengi Tz lakini waliopata dhamana wamegeuka wanasiasa. Kwasababu siasa inalipa kuliko fani yoyote Tz. Accordingly wanafanya maamuzi ya kisiasa kuliko kiuchumi. Ndio maana tatizo la ajira miongoni mwa vijana wetu waliomaliza vyuo haliongelewi na ngazi yeyote ya uongozi nchini. Hawawezi kuliongelea maana sio "maji yao". Wameamua kwa umoja wao kutolifanya kuwa tatizo la nchi.
Naamini tatizo la nchi yetu ni ukosefu wa viongozi waliobobea kwenye sekta mbalimbali ambako wakipata madaraka hawageuki kuwa wanasiasa. Sambamba na hilo ni elimu ya ubabaishaji ya hao waliopata dhamana ya kuongoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…