Tanzania SGR Bridges vs Kenyan

Nashukuru umeleta vitu vyenye akili. Mwenye macho haambiwi tazama but kwa kuwa sisi wengi wetu ni bongo lala, hatujawahi kutumia muda wetu kujadili mambo makubwa kama haya. Ni ngumu kusifia kitu chako hadi kikutoke lakini kingejengwa kwingine, ungesikia maneno yasiyokwisha.
 
Motochini ndio mrundi najua cha ukweli!!
Huyo jamaa ndio katibu mkuu wa mashabiki wa ccm, bujumbura section...kila siku huwa na sema humu immigration wa tz hovyo sana, sisi tulishamjua alivoingiaga kenya na kanzu yake anazuga zuga tu eti anaenda mombasa.
 
Huyo jamaa ndio katibu mkuu wa mashabiki wa ccm, bujumbura section...kila siku huwa na sema humu immigration wa tz hovyo sana, sisi tulishamjua alivoingiaga kenya na kanzu yake anazuga zuga tu eti anaenda mombasa.
Alijifanya ustadh na kanzu yake Mombasa wakamchuja. Hehe! Alipost hadi picha zake hapa utadhani ndo alikuwa amefika ulaya. Yaani kale kakofia ka walai hungekaona ana bonge la bichwa *****, walai yake ungedhani ni kile kijitambaa cha kichwani chake Papa mtakatifu. 😀
 
Wakenya nimeshawasoma mkiona mada imewakamata mbavu hamna pakutokea mnaanza kuleta vitu nje ya mada, kiukweli huyu mleta mada amewafangua macho kwamba sgr yenu ilikua ni wizi mtupu japo mpaka saivi aliyelitambua hilo ni mmoja tu kati yenu nyote.
 
Nlimshangaa Sana huyo mrundi, anajianika humu mitandaoni huku anajua anatumia hati feki za usafiri eti yeye ni mtanzania, niliwatumiaga immigration wetu hizo information na sasa wanamlia timing tu hapo mpakani siku anaingiza pua tu, analala cello kisha ataleta mrejesho humu[emoji191]
 
Bahati nzuri hao ni wachache sana kati ya mamilioni wenye akili na tunaotambua hizi harakati za JPM.

Vivaa JPM
Hautasahaulika kamwe
 
Viongoz wa kiafrica wana matatizo "mtambuka",huyo "magu"...au "dereva wa lori",ameirudisha democrasia ya hii nchi miaka 100 nyuma!...hatukuzoea kutekana na kupigana risasi kama rwanda,its happening now,nchi inaendeshwa kwa matamko,mihimili yote ya nchi imekuwa chini ya executive,nyie angalieni kwa nje lkn hali si shwari huku,maisha ya watu yamekuwa magumu kuliko kipindi yoyote ile,tunaisoma namba kwa kirumi!
 
hata sgr ya tz iwe nzuri aje i will never say that ours is baaaaad!!!!!!!
 
Utaeleweka ukimsema Magufuli katika kubinya vyama vya siasa na uhuru wa habari, hilo kweli ni tatizo au Mapungufu ya Magufuli, lakini kwamba maisha yamekua magumu hilo ni tatizo la mtu binafsi, alichofanya Magufuli ni kupunguza ugumu wa Maisha kwa;
1)Kudhibiti mfumko wa bei(is the lowest in EAC)
2)Kupunguza sana rushwa nchini, hasa katika maeneo za huduma za jamii
3)Elimu kuwa bure
4)Kudhibiti bei za Petrol, Diesel, na mafuta ya taa
5)Kudhibiti upandaji wa nauli kiholela
6)kuondoa kodi nyingi kwa wakulima
7)Kutotoza kodi ya mapato katika biashara ndondogo
8)Kufuta road licence
9)kuhakikisha kunakuwa na duka la dawa la serikali katika kila hospitali kubwa ili zipatikane kwa bei nafuu
10)Kushusha gharama ya bima ya afya hadi 15,000 kwa mwaka kwa familia ya watu sita
11)Kushusha bei za pembejeo za kilimo

Haya mambo yanamaanisha kwamba, kwa kipatochako kilekile ulichokua unakipata, sasa hivi kinauwezo wa kununua bidhaa nyingi zaidi kuliko kabla ya Magu, wewe inapozungumzia ugumu wa maisha una maanisha nini?.
 
Nilimaanisha gari moshi ya diesel daah
 
Hapo ni vita baridi kati ya wachina na waturuki.. Usidhan waturkey watakubali kushindwa kirahisi
 
Respect kwako kaka
 
Mkuu nimekuangushia like ya unyenyekevu sasa hii ya magu je angekuwa mamvi
 
Sina uhakika kama hiki kitu kitafika mwisho, maana kila kukicha Tanzania inadaiwa madeni bado Magufuli mwenyewe akisafiri kwenda nje wanamushikilia hukohuko
 
Sina uhakika kama hiki kitu kitafika mwisho, maana kila kukicha Tanzania inadaiwa madeni bado Magufuli mwenyewe akisafiri kwenda nje wanamushikilia hukohuko
Muda utasema
 
Huyo jamaa ndio katibu mkuu wa mashabiki wa ccm, bujumbura section...kila siku huwa na sema humu immigration wa tz hovyo sana, sisi tulishamjua alivoingiaga kenya na kanzu yake anazuga zuga tu eti anaenda mombasa.
Hivi huwa mnajisikia raha sana mnapo jadili mtu na kuacha mada husika!
 
Watu wanaoadhirika na awamu hii ni

1wauza madawa ya kulevya
2 wenye vyeti fake
3 wafanyakazi hewa beneficiary
4 waliokua wakiiba madawa, vifaa, vya serikali na kwenda kuuza mitaani
5 majangili wa nyara za taifa
6 wala rushwa hasa serikalini
7 waliokua wakinufaika na magendo bandarini, mipakani, misitu na maliasili
8 waliokua wakijilipa miposho, safari, seminars, off, na ujanja ujanja.
9 waliokua wakihudumia tenda za hovyo za kujuana na overestimate serikalini
10 wale wote wenye connection na hawa watu wawe marafiki, michepuko, ndugu, watoto na jamaa zao, wateja wao ni lazima waadhirike na uongozi wa Magufuli.

Sababu mianya yote hiyo ameiziba ila kwa wale ambao source za mapato yao haiwahusu hawa waliokua wananufaika na upigaji kwao maisha yanaendelea vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…