Viongoz wa kiafrica wana matatizo "mtambuka",huyo "magu"...au "dereva wa lori",ameirudisha democrasia ya hii nchi miaka 100 nyuma!...hatukuzoea kutekana na kupigana risasi kama rwanda,its happening now,nchi inaendeshwa kwa matamko,mihimili yote ya nchi imekuwa chini ya executive,nyie angalieni kwa nje lkn hali si shwari huku,maisha ya watu yamekuwa magumu kuliko kipindi yoyote ile,tunaisoma namba kwa kirumi!
Utaeleweka ukimsema Magufuli katika kubinya vyama vya siasa na uhuru wa habari, hilo kweli ni tatizo au Mapungufu ya Magufuli, lakini kwamba maisha yamekua magumu hilo ni tatizo la mtu binafsi, alichofanya Magufuli ni kupunguza ugumu wa Maisha kwa;
1)Kudhibiti mfumko wa bei(is the lowest in EAC)
2)Kupunguza sana rushwa nchini, hasa katika maeneo za huduma za jamii
3)Elimu kuwa bure
4)Kudhibiti bei za Petrol, Diesel, na mafuta ya taa
5)Kudhibiti upandaji wa nauli kiholela
6)kuondoa kodi nyingi kwa wakulima
7)Kutotoza kodi ya mapato katika biashara ndondogo
8)Kufuta road licence
9)kuhakikisha kunakuwa na duka la dawa la serikali katika kila hospitali kubwa ili zipatikane kwa bei nafuu
10)Kushusha gharama ya bima ya afya hadi 15,000 kwa mwaka kwa familia ya watu sita
11)Kushusha bei za pembejeo za kilimo
Haya mambo yanamaanisha kwamba, kwa kipatochako kilekile ulichokua unakipata, sasa hivi kinauwezo wa kununua bidhaa nyingi zaidi kuliko kabla ya Magu, wewe inapozungumzia ugumu wa maisha una maanisha nini?.