Tanzania SGR Bridges vs Kenyan

Tanzania SGR Bridges vs Kenyan

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890
November 8 2016 kampuni hodhi ya rasilimali za Reli ‘RAHCO’ ilitangaza zabuni kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha ‘Standard Gauge’ kipande cha Morogoro-Makutopora. Kampuni ya Yapi Merkezi Insaat ve Sanayi A.S ya Uturuki ilionekana kukidhi vigezovya kiufundi na kifedha.

Leo September 28 2017 Serikali ya Tanzania imetia saini mkataba wa pili wa kujenga reli mpya ya Standard Gauge yenye uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani MILIONI 17 kwa mwaka. Reli itakuwa inapitisha treni za umeme zenye mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

Reli hii kutoka Morogoro hadi Makutupora itakua na makalavati 123 na Madaraja 243
Pia kutakua na tunnels refu zitakazopitisha treni chini ya milima kadhaa.

Tuangalie madaraja ya juu yatakayojengwa maeneo yenye barabara kwa upande wa Tanzania dhidi ya daraja lililokatiza juu ya mbuga ya wanyama ya Nairobi nchini Kenya

Tanzania
IMG_20170930_092624.JPG
IMG_20170930_091503.JPG
IMG_20170930_091644.JPG
IMG_20170930_092427.JPG

Kenya
kenya_railway_wildlife_controversy_c45-0-5241-3030_s885x516.jpeg
Pic-1-960x608_c.jpg
1476722493659.jpg

Ikumbukwe Tanzania SGR yenye umeme inagharimu USD 3 million kwa kilometer moja wakati Kenya iligharimu USD 3.4 million kwa kilometer moja bila umeme.
 
Princple ya Tomaso ilikuwa nzuri sana. Hakuwahi kuamini hadi atie mikono yake.

Ni sawa bei yetu atleast sio mbaya na pia treni yetu itakuwa ya umeme kama ilivyokuwa proposed ukilinganisha na wakenya.

Lakini ni mara mia wakenya project yao inaonekana laiti tomaso angekuwepo angegusa na kutoa jibu. Huku kwetu bado saana ndio kwanza mtoto yuko tumboni.

Itakuwa sio jambo jema kulinganisha Mradi ambao walau umekamilika na kuonekana (SGR Kenya) na mradi wa kusadikika (SGR Tanzania).
 
Tuongee ukweli japo bado sijaona architectural designs za terminus zetu lakini za Kenya zipo poa kinyama zimechukua credit zote za maeneo mengine ya sgr yao.

Nategemea Tanzania na sisi tutawafunika kwenye terminus kama tulivyofanya kwenye electrified railway.
 
Princple ya Tomaso ilikuwa nzuri sana. Hakuwahi kuamini hadi atie mikono yake.

Ni sawa bei yetu atleast sio mbaya na pia treni yetu itakuwa ya umeme kama ilivyokuwa proposed ukilinganisha na wakenya.

Lakini ni mara mia wakenya project yao inaonekana laiti tomaso angekuwepo angegusa na kutoa jibu. Huku kwetu bado saana ndio kwanza mtoto yuko tumboni.

Itakuwa sio jambo jema kulinganisha Mradi ambao walau umekamilika na kuonekana (SGR Kenya) na mradi wa kusadikika (SGR Tanzania).
kilometers 26 tayari tuta limejengwa na kazi zinaendelea.
 
Acha ufedhuli kilometers 26 tayari tuta limejengwa na kazi zinaendelea.
Nadhani hizo 26 km's ni zile initial proposed project layouts. Kusafisha maeneo na kuweka kambi ni vitu kama hivyo pale ambapo rails za SGR zitapita.

Sidhani kama ujenzi kamili wa kulaza, kutandaza na ujenzi wa madaraja effectively umeanza.

I do stand to be corrected.
 
Mbarawa amelifafanua hili taratibu za ujenzi huu
 
Safi sana, SGR itakuwa ktk bridges especially mjini.

Kwa hapo utaanzia bandarini nafikiri mpaka vingunguti au Banana
 
November 8 2016 kampuni hodhi ya rasilimali za Reli ‘RAHCO’ ilitangaza zabuni kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha ‘Standard Gauge’ kipande cha Morogoro-Makutopora. Kampuni ya Yapi Merkezi Insaat ve Sanayi A.S ya Uturuki ilionekana kukidhi vigezovya kiufundi na kifedha.

Leo September 28 2017 Serikali ya Tanzania imetia saini mkataba wa pili wa kujenga reli mpya ya Standard Gauge yenye uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani MILIONI 17 kwa mwaka. Reli itakuwa inapitisha treni za umeme zenye mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

Reli hii kutoka Morogoro hadi Makutupora itakua na makalavati 123 na Madaraja 243
Pia kutakua na tunnels refu zitakazopitisha treni chini ya milima kadhaa.

Tuangalie madaraja ya juu yatakayojengwa maeneo yenye barabara kwa upande wa Tanzania dhidi ya daraja lililokatiza juu ya mbuga ya wanyama ya Nairobi nchini Kenya

Tanzania View attachment 598855View attachment 598856 View attachment 598857 View attachment 598858

Kenya
View attachment 598859 View attachment 598860 View attachment 598861

Ikumbukwe Tanzania SGR yenye umeme inagharimu USD 3 million kwa kilometer moja wakati Kenya iligharimu USD 3.4 million kwa kilometer moja bila umeme.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] naona hiyo ya majirani zetu engen nyuma kuna mabehewa ya kupakia makaa ya mawe
 
Wenye video ya concept design watuwekee nina shida nayo.
 
We ntakufunza kiingereza hadi lini? Acha kuchafua jukwaa bure na ung'eng'e wako gushi, tumia kiswahili bana. Sasa hapo Tanzania SGR Bridges vs Kenyan ....... ni Kenyan what? Watermelons?
 
Back
Top Bottom