Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Hakuna rais ambaye kwenye nchi hakulalamikiwa na wananchi.
Mwalimu Nyerere
Raisi kwa kwanza Tanzania huyu aliogopwa sana matajiri, masikini lakini alifanya mengi ya kukumbukwa. Aliunganisha watu na kuondoa mgawanyiko wa kieneo.
Mzee Mwinyi
Huyu alokoselewa sana na waislamu kwa kuifungua nchi. Huyu mzee alifanya wafanyabishara kupiga hela kweli kweli. Utawala wa kipindi hiki hapa ukiuza karanga unapiga hela, huyu ndio alifanya Dar iwe kimbilio la kila mtu. Sababu mtu alikuwa akija Dar mwaka tu anarudi na hela nyingi.
Ben Mkapa
Huyu ndio rais aliebuni Tanzania ya mifumo,akaiondoa kuwa shamba la bibi. Rais mbunifu alipambana kiasi chake,ana mengi ya kukumbukwa aliondoka sukari ikiwa kg 600,soda 200 bia 500 unga kg 200.
Alilaumiwa sana kwenye ukandamizaji wa demokrasia,hasa mauwaji kadha wa kadha.
Jakaya Kikwete
Huyu kwanza alipendwa na kina mama na wanawake, rais tabasamu, inapendwa kauli mbiu yake,ari mpya kasi mpya nguvu mpya. Lakini tulishuhudia maovu mengi,nchi kuwa shamba la bibi. Wakati nchi ni shamba la bibi kuna watu wanapiga hela kweli kweli,wachache wakapata wengi wakalia. CCM ikachokwa na wengi ikapendwa na wachache. Akaondoka alikumbukwa kwa upole wake na kuifanya demokrasia kukuwa Tanzania.
John Magufuli
Chuma,uso wa mbuzi mchapakazi kweli kweli,akapendwa ghafla na kila mtu,mara akachukiwa na wachache,wapiga dili wakamkataa,mabeheru wakamchukia kwa msimamo wake,hali ikawa ngumu sababu ya miradi mingi na mikubwa, matajiri wakamchukia kweli kweli,watu wa mitandao wakamkosoa sana na kumchafua. Wenye nguvu wakapambana kumpaka tope ila achukuwe na wengi zaidi. Na hatimaye akaondoka. Anakumbukwa kwa mambo ya kuonekana kwa macho mengi sana. Tanzania ya uchumi wa kati. Alilaumiwa na wanaharakati, matajiri na wachache pia.
SH Suluhu
Amefungua nchi,amesamehe wengi mwanzoni ameonekana ni mama anaejali ghafla upepo umegeuka tena anakosolewa na watu wa hali ya chini sana ambao wakati wa Magufuli waliitwa "Wanyonge " ila wakati huohuo wazee wa fursa wakipiga kwelikweli. Huyu mama ataondoka lakini 99.9% atakumbukwa sana. Kwa sasa nchi ni jalala mwenye kuweza anazoa ila atakapokuja rais arekebishe udhaifu wa mama hali itabadilika sana na kuwa ngumu na mama ataanza kukumbukwa.
Binafsi sioni tatizo za mama,japo nyumba isiyokuwa na mwanaume kila mtu hupangusia hapo tope lakini ni wakati wa kufanya unayoweza kwa sasa kuliko kulalamika na kutamani aje rais mwingine. Hata Chadema ikitawala bado malalamiko yatakuepo tu. Na hii ni kwa dunia nzima japo Tanzania unafiki ndio unatufanya tumuone kiongozi fulani ndio mbaya.