haya nimekutana na habari hizi tena kwenye magazeti yetuu kuwa safu yetu ya ushambuliaji itatisha kinyama mjini younde hadi kina song walie siku hiyooo
Washambuliaji Taifa Stars wadai kubuni mbinu mpya dhidi ya Cameroon
MSHAMBULIAJI wa Taifa Stars, Danny Mrwanda amesema wamebuni mbinu mpya ya kupambana na mabeki wa Cameroon ili kuhakikisha wanapata mabao kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi jijini Yaounde.
Stars iliikamata vilivyo Cameroon katika sehemu ya kiungo na ngome wakati timu hizo zilipotoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa Jumamosi iliyopita, lakini mashambulizi yake ya kushtukiza hayakuwa na madhara kwa wababe hao wa soka barani Afrika, zaidi ya kutoa nafasi moja ya wazi, ambayo Mrwanda alishindwa kuitumia baada ya kupiga kiki wakati akianguka.
Katika mechi hiyo ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, Mrwanda alichezeshwa kama mshambuliaji wa kwanza, akisaidiwa na Mrisho Ngassa, ambao vimo vyao ni vigogo kulinganisha na ukuta wa Cameroon wenye mabeki warefu, wakiongozwa na mkongwe Rigobert Song.
Hata hivyo, Mrwanda na Ngassa waliisumbua sana ngome hiyo lakini hawakuweza kuunganisha wavuni mipira ya juu kutokana na urefu wa mabeki hao wa Cameroon.
Akizungumza baada ya mazoezi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jana, Mrwanda alisema walitumia mbinu ya kuwakimbiza mabeki wa timu hiyo kwenye mchezo uliopita, lakini sasa watabadilisha mbinu hiyo na kutumia nyingine ambayo wana imani itakuwa na ufanisi.
''Tuliwakimbiza sana wale mabeki kwa kuwa tulijua hawawezi mpira wa kasi na kwa hilo tulifanikiwa kwa kiasi fulani kwa kuwa tulifanikiwa kuingia na mipira mingi ndani ya eneo la hatari, lakini tukashindwa kufunga,'' alisema mshambuliaji huyo anayesakata soka Kuwait.
?Lakini, nina imani watapata taabu sana mechi ijayo. Sasa tutabadilisha mbinu kidogo pamoja na kuwakimbiza tutaongeza vitu vingine ambavyo vitatufanya tupate mabao kwani nia yetu ni kuhakikisha tunafunga ili tujiweke pazuri na hilo hata kwa Cameroon linawezekana bora tuwe pamoja.?
Kocha wa Stars, Marcio Maximo, ambaye hakumchezesha mshambuliaji wake tegemeo Emmanuel Gabriel, bado anaonekana kutoridhishwa na safu yake ya ushambuliaji na jana alionekana kuendelea kufundisha mbinu za kupata mabao.
Kocha huyo Mbrazili amekuwa akifundisha washambuliaji wake na wachezaji wa kiungo kujaribu kiki za mbali na amekuwa akiwatumia sana Abdi Kassim, ambaye aliingia mwishoni mwa mechi na Cameroon, na Nizar Khalifan, ambaye alitoka kumpisha Kassim