Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Tanzania (Taifa Stars) vs Morocco

Kuna makosa madogo madogo sana kama yatarekebishwa tutakuwa na timu nzuri,sana sana kwenye maamuzi ya mwisho ya mpira.
 
Huyu kocha inabidi awarudishe darasani wachezaji wetu kwenda kuwafundisha upya jinsi ya kutoa pasi. Naona walikuwa na nafasi nyingi tu ya kujenga mashambulizi ya magoli lakini utakuta mtu anatoa pasi mbovu au anaenda kuachia shuti la mbali bila sababu.

Inakuwaje mtu hauko kwenye msukosuko wowote unashindwa kutoa pasi ya uhakika?

Afadhali umeliona hili la pasi. Mi nimeona mengi..kuna ball control mbovu, kutaka kudribble bila sababu, kushoot bila sababu, positioning mbovu..yaani kila kosa wamelifanya. Naona wachezaji wetu wana-lack vitu vya msingi kabisa, tena karibia vyote. Nionavyo kuweza kupata timu competitive kwa hawa wachezaji tulionao ni ndoto..ni vema kuelekeza nguvu kwene michezo mingine tu..

Truth hurts..
 
Mheshimiwa rais kawapungia mashabiki na alikuwa anasalimiana na wachezaji kwa kugongeshana mabega (ushkaji?) na anatabasamu muda wote
Ni mechi yake ya mwisho kuhuzulia kama rais ndiyo maana alienda kuuza sura
 
Afadhali umeliona hili la pasi. Mi nimeona mengi..kuna ball control mbovu, kutaka kudribble bila sababu, kushoot bila sababu, positioning mbovu..yaani kila kosa wamelifanya. Naona wachezaji wetu wana-lack vitu vya msingi kabisa, tena karibia vyote. Nionavyo kuweza kupata timu competitive kwa hawa wachezaji tulionao ni ndoto..ni vema kuelekeza nguvu kwene michezo mingine tu..

Truth hurts..

Kweli mkuu, wapeleke nguvu kwa timu za vijana hawa wakubwa akili zishakomaa hawafundishiki au hawajifunzi na ujuaji mwingi.
 
Kusema ukweli mpira wa Tanzania upo kisiasa zaidi. Tafuta kocha mwenye CV kubwa siyo mara Maximo mara....ila mradi muonyeshe mmemleta mzungu. Ila kisiasa hii imetulia nitaweza kuwa na moyo wa kuishabikia baada ya 31st. Muhimu sana
 
watu weshazungumza sana mapungufu yetu yako wapi

moja tunapenda kuvuna bila ya kupanda
au kutumia nguvu ndogo kuvuna sana

kiukweli tuanzie kwenye ligi zetu tuziimarishe
tuandae wachezaji professional tokea wakiwa wadogo si hawa waliochepukia kifluku fluku

tuekeze kweli sio makelel kwenye mpira usichukuliwe kisiasa

tuwe tayari kukubali mpira una matokeo mengi

tusomeni kwa kujifunza na tuanze kutoa ushauri wa nn kifanyike ili tuwe na timu nzuri hapo baadae
 
kweli maumivu yaliyotabiriwa kuwa yanakuja yamenikomesha, kukodoa kote kwenye screen naambulia vituko, hata kupiga pasi pia hatuwezi....duh safari bado ni ndefu. Kwa wachezaji hawa hata aje kocha ambaye ndio namba moja kwa ufundishaji duniani bado tutapata kichapo.
 
Huyu kocha nina waiswasi na uwezo wake Taifa stars iliyopikwa na Maximo ina matatizo ma2 tu, moja ni kipa hilo amelifanyika kazi nampa heko, mbili ni ushambuliaji hapo amefeli kwa kweli ukiangalia timu inaanza vizuri ila mwisho wetu nusu ya kwanza ya eneo la wapinzani tunapotexa mipira na pale kati washambuliaji wetu akina Ngassa na Mrwanda ni wafupi wakati mabeki pinzani ni warefu pia Ngassa hafai kucheza kama mshambuliaji wa kati bwana Poulsen wewe kocha wa wapi? Next time ukitaka timu ishinde foward line uipange hivi Ngassa winger wa kulia, Mrwanda winger ya kushoto na namba 9 na 10 waweke John Boko na Tegete lazima tutafunga tu halafu jamaa wa Sofapaka yule Idrissa mweke bench I am sure kwa viuongo tulionao na beki makini tutaambulia chochote mh. Kocha. Ni hayo tu mwanawane
 
uwanjani siendi tena, taifa siendi tena ,mpirani siendi tena kwani kuna maumivu mengi bila kutengeneza mfumo bora kwa soka yev kwa kuendeleza vipaji, mafanikio siku zote tutayasikia kwenye bomba safu ya ushambuliaji ni butu na vilabu vina wajibu wa kutengeneza fowadi na si jukumu la kocha wa timu ya taifa
 
10_10_9jyh3c.jpg
 
Jk na wenzake wanapigwa na putwaa....nyimbo za taifa vp??:embarrassed::A S confused::angry:
 

Attachments

  • IMG_1734[1].jpg
    IMG_1734[1].jpg
    33.6 KB · Views: 39
Hao mapro wetu utumbo mtupu! Mchezaji kama Nizar ameshindwa kucheza tangu dakika ya kwanza, kocha anamchezesha hadi dakika ya 85! Huyu kocha naye, mmmhh! Ngoja tusubiri tuone!
 
Niliangalia hii mechi naona bado tuna safari ndefu, kama alivosema Abdulhalim kwenye ufundi (technical abilities) timu yetu ilikosa kila kitu!! wachezaji ni butuabutua, tackles mbovu, hakuna ball control, positioning yaani sikuamini macho yangu, hawa wachezaji wetu ilionekana kama tumewaokota kwenye ligi zile za vijiweni. Tuna wachezaji wana uwezo ila sijui woga ama system ya kocha? Ni afadhali hata ile timu ya Maximo
 
Hili kunde kwa kweli litakuwa gumu sana jana Cenral Africa Rep kashinda 2-0 dhidi ya Algeria so wanaongoza lwa point 4 then Morocco nao wana point 4 then sie na Algeria tunafunga mkia kwa point 1 sasa mechi zijazo ni Algeria vs Morocco and Tanzania vs Cenral Africa Rep, and if both us and Algeria will win then kundi linarudi at par kila mmoja akiwa na point 4 ila tatizo la kocha wa sasa sijui kama ataambulia hata point moja kwa mechi zilizobaki?
 
Niliangalia hii mechi naona bado tuna safari ndefu, kama alivosema Abdulhalim kwenye ufundi (technical abilities) timu yetu ilikosa kila kitu!! wachezaji ni butuabutua, tackles mbovu, hakuna ball control, positioning yaani sikuamini macho yangu, hawa wachezaji wetu ilionekana kama tumewaokota kwenye ligi zile za vijiweni. Tuna wachezaji wana uwezo ila sijui woga ama system ya kocha? Ni afadhali hata ile timu ya Maximo
Mkubwa..hili tatizo la soka mi naona ni sugu sasa ni wakati wa kunyoosha mikono! Kufungwa ndio ni sehemu ya mchezo, lakini kufungwa repeatedly and dissapointingly, over and over, haikubaliki kwa mzani wowote ule. Nadhani at some point a man has to do something about it. Sio siri tena.

Hatuwezi kulizungumzia hili hili kizazi hadi kizazi na bado tunachukua route ileile na kutarajia tutaibukia mjini tafauti!

Mi kwa kweli nimechoshwa naona tuwekeze kwenye michezo mingine kwa sasa wakati tunajenga timu za vijana. Hakuna uvunaji bila kupanda..its natural that way. Hata Ghana ile tuliyoiona Woza ilipikwa kuanzia mbali sana, akina Essien, Gyan na wenzake ni batch ya timu ya vijana iliyofungwa fainali ya dunia ya vijana kule Argentina. Mafanikio hayakurupushwi!
 
Back
Top Bottom