Tanzania tuhifadhi akiba yetu kwa Dhahabu badala ya Dollar

Tanzania tuhifadhi akiba yetu kwa Dhahabu badala ya Dollar

28 November 2022
Accra, Ghana

Probing Ghana's Gold For Oil Barter Deal - The Probe with Emefa Apawu

Ghana has a total gold reserve of 8.7 tonnes according to the central Bank of Ghana latest report , GTG Government to Government arrangements with UAE govt for gold for oil option.. is on the table for discussions..

To explain how this move will work, JoyNews invites Dr. Mohammed Amin Adam deputy energy minister, Dr. Kwabena Donkor member - mines and energy Committee of Parliament and Dr. Sulemanu Koney CEO of Ghana chamber of mines ... and behind the scene government is engaging stake holders in oil industry .... is there enough gold reserve and does the sellers of oil in the international market ...
Source : Joy News
 
ACCRA, GHANA

MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI GHANA🇬🇭

Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.

Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.

Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.

Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.

Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.
Source : JoyNews
 
Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei​

Julai 28, 2022
Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei
Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya akionyesha sarafu mpya ya dhahabu kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, Zimbabwe, Julai 25, 2022. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)​

HARARE - Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya Jumatatu wiki hii alitambulisha sarafu mpya za dhahabu ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika kama hifadhi ya thamani na kupunguza mahitaji ya dola za Marekani wakati nchi hiyo ikipambana kudhibiti mfumuko wa bei unaoongezeka.

"Benki hii leo imeingiza sokoni kundi la kwanza la sarafu 2,000 za dhahabu za Mosi-oa-Tunya (Moshi unaovuma). Mashirika ya ndani yalianza kuuza sarafu hizo za dhahabu kwa misingi ya uwakala kwa bei ya awali ya dola za Kimarekani 1,823.83 kwa kila sarafu ya dhahabu au dola za Zimbabwe 805,745.35 kwa kutumia viwango vya bei vinavyokubaliwa na mnunuzi na muuzaji vya Ijumaa (wiki iliyopita)," Mangudya amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe.

Miongoni mwa sifa nyingine, sarafu hiyo ya dhahabu itakuwa na thamani ya ukwasi wa mali, thamani ya mali iliyowekwa, inaweza kutumika kama dhamana, kuuzwa na kununuliwa kwa idhini ya mmiliki.

Watu binafsi, makampuni ya ndani ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa kitaasisi wataruhusiwa kununua sarafu hizo za dhahabu kwa fedha za ndani pamoja na fedha za kigeni, wakati wanunuzi wa kimataifa watanunua tu sarafu hizo kwa fedha za kigeni ambazo ni pamoja na dola ya Marekani, Randi ya Afrika Kusini na Pauni ya Uingereza miongoni mwa nyinginezo.

Bei ya sarafu inategemea bei ya kimataifa ya dhahabu pamoja na asilimia 5 ili kufidia gharama ya uzalishaji na usambazaji wa sarafu kwa malipo dhidi ya utoaji.

"Sarafu za dhahabu kama tulivyoshauri hapo awali, ni bidhaa mbadala nzuri ya uwekezaji kwa wale wanaotaka kuhifadhi thamani. Dhahabu ni mali ya akiba iliyo salama na ya kutegemeka duniani kote," amesema Mangudya.

Pia amesema wanunuzi binafsi na wa kitaasisi wanatakiwa kushikilia sarafu hizo kwa angalau siku 180 kabla ya kuziuza, na kuongeza kuwa mauzo yote yatakuwa chini ya Mfahamu Mteja Wako na wanunuzi wanatakiwa kutangaza chanzo cha fedha zao.

Kuanzishwa kwa sarafu hizo za dhahabu ni sehemu ya hatua za Serikali ya Zimbabwe za kukabiliana na mgogoro wa sarafu ya nchi hiyo ambao umepelekea dola ya ndani kushuka kwa kasi.

"Tunachotarajia kuona ni kwamba tunashuhudia utulivu katika kiwango cha ubadilishaji na kwahivyo kwa kuongeza athari za kupita kwenye mfumo wa bei, viwango vyote vitashuka. Kwa hivyo tunatarajia kuona utulivu wa bei katika uchumi," Mangudya amesema.

Kufuatia miaka mingi ya mfumuko mkubwa wa bei, Zimbabwe iliachana na sarafu yake ya dola Mwaka 2009, na kuamua kutumia fedha za kigeni, hasa dola ya Marekani.

Serikali ilirejesha sarafu ya ndani Mwaka 2019, lakini imepoteza thamani kwa haraka, na hivyo kurudisha kumbukumbu za kipindi cha mfumuko wa bei ambao ulipunguza akiba za watu wengi
 
Najiuliza sana, sijui kwenye sera zetu za fedha, BOT wanafuatilia mapinduzi haya yanayoirudisha Dunia kwenye dhahabu,

Dodoma, Tanzania

HALI YA UCHUMI WA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MWAKA 2021

Thamani ya mauzo ya dhahabu ilipungua kwa asilimia 7.2 na kufikia dola za Marekani milioni 2,743.1 mwaka2021 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 2,957.5 mwaka 2020.

Hii ilitokana na kupungua kwa uzalishaji wa dhahabu ambapo uzalishaji katika migodi mikubwa ilipungua kutoka tani 44.8 mwaka 2020 hadi tani 39.7 mwaka 2021.

Hata hivyo, bei ya dhahabu katika soko la dunia iliongezeka kutoka wastani wa dola za Marekani 1,770.3 kwa wakia moja mwaka 2020 hadi wastani wa dola za Marekani 1,799.6 kwa wakia moja mwaka 2021.

Aidha, mapato ya mauzo ya madini yalichangia asilimia 53.8 ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia na mauzo ya dhahabu yalichangia asilimia 88.4 katika mauzo ya madini mwaka 2021.

Soma zaidi : source :
Ministry of Finance and Planning
https://www.mof.go.tz › sw-1...PDF
HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2021

10 Jun 2022 — HALI YA UCHUMI WA DUNIA NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA . ... Thamani ya mauzo ya dhahabu ilipungua kwa asilimia ...
 
03 October 2022
Accra, Ghana

JINAMIZI LA DHAHABU KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NCHINI GHANA PART 1

Serikali ya Ghana yapambana na wachimbaji wadogo inaowatuhumu wanaharibu mazingira, mito ya maji safi.

Hivyo serikali kuingia porini kuwasaka wachimbaji hao na kuiponda kwa nyundo mitambo kama generator, pump za maji na kuchoma moto excavators huku operation Vanguard ikizidi kuwaandama wachimbaji wadogo .... .

Tatizo hilo pia lipo katika nchi za kiAfrika mfano Tanzania nchi tajwa kwa uzalishaji mkubwa wa dhahabu ambapo wachimbaji wadogo hufurushwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo wachimbaji wakubwa kutoka nje kupewa leseni kuchimba sehemu ambazo wachimbaji wadogo wa kiTanzania wamekuwa wakijitafutia riziki zao ...

DESTRUCTION FOR GOLD PART 1

Source : JoyNews

31 Oct 2019 — Operation VANGUARD is a Ghanaian Presidential initiative aimed at ending an illegal mining activities otherwise referred to as “galamsey ...
LAUNCH OF OPERATION VANGUARD
Ghana Ministry Of Defence
https://mod.gov.gh › 2019/10/31

Source: JoyNews
 
11 November 2022
Tarime, Tanzania

Wachimbaji wadogo wasusa mkutano, wanyanyuka na kutoka ukumbini, walalamika tumeumizwa sana na kufilisiwa

Walaani vitendo vya kufilisi wachimba wadogo wa Nyamongo.

Mgodi mkubwa wa Barrick pia upo katikati ya makaazi ya watu vipi wao wachimbaji wadogo wana pigwa vita na kamishna wa Madini kuwa wanachimba katika makaazi ..... wamkumbuka John Pombe Joseph Magufuli ...
Source : Nyamwaga online TV
 
Dunia inabadilika sana, wanasiasa, wachumi na watu wa mipango wetu wasije kuja kutoa visingizio kuwa hawakujua kuwa itakuwa hivi.

Mabadiliko ya uchumi na mpangilio wa uchumi wa dunia inaonekana wazi hata kwa sisi tusiokuwa wanasiasa wala wachumi kuwa dollar itapungua umuhimu wake siku chache tu zijazo. Tuanze kufikiria kuongeza akiba yetu ya ununuzi na uhifadhi wa dhahabu bala ya kurundika US Dollar.

Nchi zote zenye akili zimeanza mchakato huu, sisi pia tusisubiri tusikie filimbi ndio tuanze kuongeza akiba yetu ya dhahabu. BoT iwe mnunuzi mkuu wa dhahabu yetu nchini na hata nyingine kutoka nje kama ni bora zaidi ya kwetu.

tumeachiwa mashimo la kwanza lipo kahama
 
Duh !! Mfumo fake ?? Hebu tudadavulie kidogo Mkuu
Kasome mkuu upate nondo za kweli,rudi darasani,hujasoma umebebeshwa mchanga.

Fuata link zifuatazo kwa kuanzia uone jinsi tulivyo ingizwa mkenge.This is to be frank the most brutal hoax that has ever been perpetrated on the human race.Mtu unampa dhahabu halafu wewe anakupa "karatasi"(paper money),halafu unachekelea,kama sio uzuzu wa kupindukia ni nini.😭

Kuikwepa dollar inakuwa ngumu sana. Na ulimwengu kwa sasa unaondoka kwenye kuifanya dhahabu kuwa kigezo cha thamani ya fedha kwa nchi husika. Hata dolla kwa sasa haipimwi thamani kwa kigezo cha wingi wa dhahabu ulioko kwenye akiba ya Marekani.

Uchina ndiyo nchi inayoongoza kwa kununua amana na hatifungani za Benki Kuu ya Marekani kwa ivo kila dollar iliyoko mtaani mchina naye ana hisa zake. Uchumi kwa sasa unapimwa kwa kuzalisha na kuuza na fedha inayowezesha kununua kokote duniani ni dollar na siyo dhahabu.

Kwa ivo kama unataka kufanya manunuzi duniani badala ya kuwa na dhahabu utatakiwa kuwa na Dollar, kwa mfumo huo ni heri kuwa na akiba ya dollar badala ya kurundika dhahabu. Ingawa pia akiba ya dhahabu inahitajika.
Hiyo unaongea zamani, amka kaka usiendelee kuota ndoto za hivyo.
 
Mrema alitoa wazo hili miaka karibia 10 iliyopita, leo hii tungekuwa na tani zaidi ya mia. Lini waafrica wakawa na long term plan ndugu yangu wakati unajua utakufa sasa hiyo mipango umwachie nani afaidi.
 
Mkuu haya mambo kwa mtu ambaye unategemea Economics ya Chuoni si rahisi kuyaelewa.Ndio maana natoa angalizo.Inasikitisha kwamba mtu wa Chuo Kikuu hajui hata kwamba kuna kitu kinaitwa Fiat Money,na kwamba mfumo wa pesa uliopo sasa ni fake.
Mfumo wa hela duniani umetengenezwa kuwa mabeberu waweze kuishi popote kwa gharama nafuu, lakini nchi maskini ziishi maisha ya taabu sio tu wanapoingia nchi za kibeberu bali hata ndani ya mataifa yao wenyewe. Mabeberu wanaweza kuishi Tanzania kwa amani kabisa kwa miaka 3 wakiwa na Dolla 100,000 tu, lakini wewe hata ukiwa na sh. 50,000,0000 huwezi kuishi hata kwa miezi 2 kwao.
 
Wilaya ya sikonge yote dhahabu na hakuna mwekezaji anayechimba,changeni bukubuku kila siku kila mtz mpate mtaji wa kuchimba
Tuchange tuchimbe chuma yetu ya liganga na mchuchuma, dunia yote itatupigia magoti kama tukiwa na chuma. Chuma hii itatupa uwezo mkubwa wa kutengeneza vifaa vya kuchimbia dhahabu sisi wenyewe, tutajenga reli kila kona kwa bei nafuu kuliko sasa.
. Huu sio muda wa kukumbatia Dollar tena, tuzijaze hazina zetu kwa madini yetu safi (dhahabu, silver, tanzanite, ruby, etc).

Siku za mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke sio nyingi, Lazima tuwe visionaries, huu sio muda wa kuwa na viongozi wa kulipana hisani, kubakisha chama madarakani au wa jinsia ile au hii au wanaosifu sana. Tunahitaji viongozi wanaofahamu kule dunia inakoelekea na kuchukua hatua leo na sasa kwaajili ya mustakabali wa vizazi vyetu badala ya kuwaaza matumbo yaao na yale ya jamaa zao tu. Tusiwe wasindikizaji (passive) kwenye mchakato wa mabadiliko haya ya dunia. Kama ni lazima kutumia jinsia, elimu, kabila, dini, jeshi letu, mahakama zetu, ardhi au watu wetu kwenye mchakato huo hakuna budi kutumia tu bila kujali wengine watasema nini. Taifa lazima lijue linataka nini na linaelekea wapi kwa njia zipi, Taifa liwe tayari kukabaliani na vikwazo vya aina mbalimbali kutoka kwa watu na mataifa tofauti wakati wa kusonga mbele.

Binafsi ninamuona JPM kama mtu ambae alikuwa anajua kile kinachotakiwa kufanyika kama taifa, ila alishindwa kuliunganganisha taifa ili liwe nyuma yake kwenye safari hii.
 
Duh !! Mfumo fake ?? Hebu tudadavulie kidogo Mkuu
Soma hapa mkuu.Mfumo wa pesa tulio nao ndio the most brutal hoax that has ever been perpetrated on the human race.Ni huruma sana.Yaani mtu anakupa karatasi(printed money),halafu wewe unampa kitu cha thamani kama dhahabu halafu unachekelea kwamba ume-win,kama zuzu hivi......!

Dunia inabadilika sana, wanasiasa, wachumi na watu wa mipango wetu wasije kuja kutoa visingizio kuwa hawakujua kuwa itakuwa hivi.

Mabadiliko ya uchumi na mpangilio wa uchumi wa dunia inaonekana wazi hata kwa sisi tusiokuwa wanasiasa wala wachumi kuwa dollar itapungua umuhimu wake siku chache tu zijazo. Tuanze kufikiria kuongeza akiba yetu ya ununuzi na uhifadhi wa dhahabu bala ya kurundika US Dollar.

Nchi zote zenye akili zimeanza mchakato huu, sisi pia tusisubiri tusikie filimbi ndio tuanze kuongeza akiba yetu ya dhahabu. BoT iwe mnunuzi mkuu wa dhahabu yetu nchini na hata nyingine kutoka nje kama ni bora zaidi ya kwetu.
Congratulations. Hii thread nzuri na ya maana sana. Sitashangaa haitapata wachangiaji wengi! Ndiyo Tanzania. Thread za umbea na kuzungumzia watu ndiyo utakuta changio la watu elfu+
Kwa kuchangia: mara nyingi miye nachanganyikiwa kama tuna wachumi waliokwenda shule! Ukitazama mambo chungu nzima yanayohusu uchumi yanavyoendeshwa bila fikra za kiuchumi, zingine wala hazihitaji elimu kubwa, common sense tu yatosha: kwa mfano Kodi kubwa ya kupita kiasi inayoua biashara hasa ndogo ndogo, kufanya internet kuwa ngumu, wakati dunia nzima, watu wanakuwa mamilionea kwa biashara ya mtandaoni..... na mengi mengine.
Lakini hili la dhahabu ndiyo laonesha 'ubahau' usio mfano wa wachumi wetu. Ukitazama nchi ambazo safaru zake zina nguvu duniani, ni zile ambazo zina akiba kubwa ya dhahabu. Hebu angalia list hii:
USA: tani 8,133
Ujerumani: tani 3,362
Italy: 2, 451
Ufaransa 2,436
Urusi, 2,298
Uchina: 1,958
Uswisi: 1,040......
Nyingi ya nchi hizi, kasoro Urusi, hazina hata machimbo ya dhahabu!
Katila listi hiyo hata ukiendelea chini hadi nchi ya 18, hakuna hata nchi moja ya Afrika.
Tuje Tanzania. Kweli twashindwa kuweka hata nusu tani kila mwaka katika benki yetu? Tena siyo ya dhahabu tu, tuweke tani ya Tanzanite, ya pekee duniani, iwe reserve?
Kweli wachumi wetu na wanasiasa hawajui umuhimu wa hili katika kutia thamani ya sarafu yetu! Wao wanaendelea kuweka reserve ya dola tu maana hiyo tu ndiyo waliyofundishwa na kunata akilini mwao!
Sasa dola haina miaka kumi ijayo itapikuliwa na sarafu nyingine, hapo ndipo mijitu itaanza kuamka!
Mleta mada umeleta mada ambayo nimekuwa nikiifikiria kwa muda mrefu na kujiuliza.
Pia tujiulize, lile bulungutu la Tanzanite ambalo marehemu Magufuli, kwa hekima kabisa, amekataa lisiuzwe na liwekwe liwe maonesho........bado lipo? Sidhani!
 
Usa wanachimba dhahabu weka sawa hiyo taarifa
 
Mkuu mbona kila kitu unaweka sijui tutakuelewa
Haya sasa hatujakuelewa amua la kutufunya
Yaan sentensi mbili tu looh sijui kama mmenielewa sijui nini!!
Wewe andika achia server wala huhitaji kujua kuwa umeewleweka au laaah
Ni kwa faida yako mkuu jitahidi kuelewa na hakuna ninachoweza kukufanya kama hujaelewa.

Nimesema repeatedly sijui utanielewa kwa sababu nipo concerned kwamba watu wanaweza wasinielewe kwa sababu ya background ya elimu zetu tulio wengi.Elimu zetu si nzuri sana,frankly elimu yetu imechakachuliwa sana.
 
Kasome mkuu upate nondo za kweli,rudi darasani,hujasoma umebebeshwa mchanga.

Fuata link zifuatazo kwa kuanzia uone jinsi tulivyo ingizwa mkenge.This is to be frank the most brutal hoax that has ever been perpetrated on the human race.Mtu unampa dhahabu halafu wewe anakupa "karatasi"(paper money),halafu unachekelea,kama sio uzuzu wa kupindukia ni nini.😭

Hiyo sio defense nzuri!! Ile ni karatasi tu ila inakua na thamani sababu ya kuwa legal tender ni sawa na mkataba ya kimataifa Ina thamani ya mabilioni ila inafungwa kwa karatasi ya shillingi 50 tu!! Au cheque ni karatasi tu ila unakuta ina thamani ya mabilioni so issue sio karatasi hata Leo wakiamua tutumie cryptocurrency watu watakua wanauziana Nyumba kwa kutumia simu Sasa hapo si ndio utashangaa zaidi.

Au umewahi ona hati fungani yaani unauziwa karatasi kwa say billion 5!! Yaani unatoa billion tano kununua karatasi!! Ila siku Ile karatasi Ina mature unapata zaidi ya hiyo billion 5.

So issue sio karatasi au Dhahabu issue ni kitu Gani kinakubalika kama means of exchange ya bidhaa na huduma. Siku wakiamua matunda yatumike nayo yatapanda thamani.
 
Zitto wewe ni mhanga wa "Con Economics." Follow the following links ujifunze.Kama hutanielewa,siwezi kukusaidia,wewe ni sikio la kufa.Hata mimi ni mhanga,lakini niliamua kwa makusudi kutafuta ukweli.

Back
Top Bottom