kudhibiti soko kama ilivyoagizwa kwenye sheria ya mwaka 2017.
SHERIA YA MADINI MABADILIKO HOTUBA YA PROF. KABUDI
HOTUBA YA MHESHIMIWA PROF. PALAMAGAMBA J.A.M.
KABUDI, WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKIWASILISHA
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA
MBALIMBALI WA MWAKA 2017 (THE WRITTEN LAWS
(MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2017)
________________________________
1.0 Utangulizi
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 86 ya Kanuni
za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2016, naomba kutoa
hoja kwamba Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2017 (The Written Laws
(Miscellaneous Amendments) Act, 2017) sasa usomwe kwa
Mara ya Pili na Bunge lako Tukufu lijadili na hatimaye
lipitishe Muswada huu na kuwa sehemu ya sheria za
Kuweka masharti yatakayowezesha kuunzishwa kwa .........
vyombo mbalimbali vitakavyohusika katika shughuli
za madini kwa niaba ya serikali. Vyombo hivyo ni
pamoja na:
(i) Hifadhi ya dhahabu na vito chini ya Benki Kuu
(Establishment of the National Gold and Gemstone Reserve); Rejea ibara ya 27 C
(ii) Maeneo maalumu ya masoko ya dhahabu na
vito (Gem and Minerals Houses); Rejea kifungu kipya kinachopendekezwa cha 27B
(iii) Maghala ya Serikali ya kuhifadhia madini
(Government Mineral Warehouses); Rejea kifungu
kipya kinachopendekezwa cha 27D ......