SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Mradi wa kutenga maeneo ya majaribio ya kisayansi na bunifu kwa vijana

SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Mradi wa kutenga maeneo ya majaribio ya kisayansi na bunifu kwa vijana

Tanzania Tuitakayo competition threads

Vallekh

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3
Reaction score
5
UTANGULIZI

Kumekuwa na changamoto nyingi zinazo wakabili vinaja wabunifu nchi nifurahi kuleta wazo hili kwa mara ya kwanza kama mtu ninayependa kushauriana nawe katika maana ya kuleta maendeleo katika kizazi kijacho, binanfisi nimejaribu kufanya majabio kazaa ambao hayakufanikiwa kwa sababu labda za kukosa maeneo mahalumu ya kufanyia majaribio na hali hii imekuwa ikiwa waumiza vijana wengi nchini:-

1. Nadharia ya kwanza: kwamba Kukosa mazingira salama ya kufanyia majaribio ya ndoto za vijana kunawafanya vijana wengi kufa na ndoto zao na kupoteza kusudi la MUNGU juu ya kuzaliwa kwao.

2. Kwamba kukosa maeneo ya majaribio kunashindwa kuziamsha au kusisimua nguvu za kimungu “ potential energy” ndani ya vijana wengi kutafakari nguvu hizi aidha bila wao kujua au kutojua kama wanazo. Nadharia ya pili “ kwamba kuna watu uzaliwa na uwezo wa kubuni na kutengeneza maajabu au kufanya vitu kwa upekee lakini wanakuwa hawajijui sababu nguvu hizi wakati mwengine uwitaji mazingira au matukio mengine ya kuzisisisimua zitoke ndani ya mtu na kufanya kazi.

3. Nadharia ya tatu : Kwamba kutoona watu wakaijaribu matukio makubwa au kufanya majaribio kuna wafanya vijanA wengi kushindwa kabisa si tu kufanya kama wenzao bali hata kujaribu yale wanayoota kuyafanya au kushauri na matokeo yake vijana WENYE nguvu ya kiMUngu kutotumia nguvu hii katika kusudi la mungu ivyo wanajiingiza kwenye matukioa, tabia na ubunifu usiyo usiendana na nguvu za kiMungu zilizo ndani yao na matokeo yake wanakufa na uwezo wao au wanafanikiwa maeneo ambao nguvu zao hazifanyi kazi.

Hakuna ubishi kuwa Tanzania ni moja nchi yenye watu wenye uwezo mkubwa vipaji lakini kwa bahati mbaya serikali zilizopita aidha kwa kutojua au kudharau wakijua wamekuwa hawawekezi kwenye matumizi ya kutumia watu wenye kalama na upekee kama tarifa bank ya dunia inavyosema ya mwaka 2017 juu ya uwekezaji barani Afrika.


CHANGAMOTO ZA WABUNIFU
i. Kukosa maeneo ya majaribio yaliyo rasmi kwa ajili majaribio ya kisayansi.

ii. Kukosa majukwaa ya kisayansi ambao yatayowakutanisha na wenzao

iii. Kukosa vifaa vya na maitaji muhimu kwa ajili ya majaribio
iv. Kukosa heshima,kunyanyasika,kutengwa na kutothaminika juu ya kile wanachojaribu kukifanya kwa taifa.

v. Kukosa taratibu au muongoza wa kiserikali mbadala pale wanapojaribu ndoto zao Hakuana ubishi kuwa nchini nyengine zinanufaika na Watanzania kwa ubunifu wao, upekee wao, na uwepo wao wa ajabu katika aidha kubuni au kusanifu vitu vilivyopo kwenye mwonekano wa kipee, inaumiza sana pale ninapoona kijana kwa kupuuzwa tu nchi nyengine inamchukua na kumtumia bila hata kulipa shilingi mia lazima hali tuimabadilisha sasa lazima watu wetu wawe bidhaa muhimu kwa nchi yetu, LAZIMA watu awa wawe zaidi ya dhababu zetu sababu uzaliwa kwa bahati na wanapaswa kutumika zaidi pale walipozaliwa tofauti na sasa.

MALENGO YA MRADI HUU
1. Kuwamasicha na kuwamsha nguvu ya kubuni( nguvu ya kiMungu) vkwa vijana kwa kuwapa uhuru wa kubuni au kusanifu upya vitu vilivyopo kwa katika muonekano wa kipekee. Hoja hii iko katika nadhali hizi:-

Mosi: “ mtu anaweza kubuni jambo aidha kwa kuota akiwa amelala, kufikiria jambo hili kwa mda mrefu, matatizo yaliyomkabili awali au sasa na kwa njia hisia tu kwamba akifanya kitu Fulani anaweza pata matokea Fulani hataka kama matokeo yenyewe yeye hayajui yatakuwaje lakini mtu huyu lazima awe nguvu kama ilivyoelezwa kwenye

Nadharia ya kwanza ya juu ya nguvu ya kiMUngu kwa binadamu wachache”

AU

Pili: kwamba “ mtu anaweza asingunduwe jambo jipya lakini anaweza pia kusanifu kitu kilichopo kuwa cha kipekeke, kisasa na thamani kubwa pia mtu huyu kamalivyoelezwa kwenye Nadharia za lazima awe na nguvu za kiMUngu ndani”

2. Kuwandaa vijana na kuwatambua watu wenye upekee, nguvu za kutenda makubwa na kuwasajili kisha kuwafatilia kila mara na kuweka utaratiu mahalumu wa watu awa kutumika na nchi nyengine kama Nadharia hii:-

Mosi: “ tunaweza tukawa na watu wenye uwezo mkubwa na sisi tukawa hatuna uwezo wa kuwatumia sasa lakini tutafuta namna ya watu haya kutafutia nafasi katika nchi nyengine na sisi kama nchi tukapa heshima kupitia wao na kunufaika kwa namna yeyote hata kama wako mbali nasi” Pili: “ kwamba tunaweza tukawagundua watu wa wenye uwezo mkubwa sababu tu wamezaliwa nao na wakatumika katika majaribio ya watu wengine ndani na nchi na nje ya nchi”

3. Kuwatumia watu wenye upekee kwasababu tu wamezaliwa na kuwatumia katika kutatua matatizo ya wananchi kwa njia na kuwapa majukumu mahalumu ya kisayansi.

4. Kutumia maeneo haya ya majaribio kwa ajili a uzinduzi wa bidhaa za kitanzania, sera ya kisayansi, mikutano ya kisayansi na huduma mpya za kisayansi.

5. Kutumia maeneo aya ya kisayansi kwa ajili ya kubuni maonyesho ya ugunduzi na utundu wa kitanzania

6. Kuwapa watu kushindana kwatika kugundua vitu, kubuni na kusanifu Mfano: nchi za BARA la ASIA watu wake ushindana kila siku kusanifu na kubuni vitu sababu kuna mwendelezo wa tabia hizi tokea babu zao na wao wanaendeleza inaumiza mda mweningine kusoma kuona nchi yenye eneo dogo, idadi ndogo ya watu na wakiwa na vikwazo vya kiuchumi lakini watu wao kila siku wanajaribu kufanya jambo kubwa, wajaribu mifumo yao wenyewe ya simu, siraha zao wenyewe za kisasa na teknolojia ya pekee, je kwanini isiwe kwetu na sisi? Kama serikakali tunapaswa hali hii kuwa iwe kwetu pia.

7. Kuanzisha kwa viwanda vya vikra Tanzania hivi ni viwanda ambavyo bidhaa zitakuwa zinabunia na Watanzania lakini sababu ya kuitaji teknolojia kubwa basi kwa makubaliano mahalumu zitazilishwa na nchi rafiki na kuuzwa kote duniani bidhaa itakayotokana na ubunifu hii itaandikwa “ made in china but innovated in Tanzania”

D. FAIDA YA MRADI HUU

1. Utawavutia watu wengi zaidi nchi kujaribu au kuvuvua ndoto zao katika ulimwengu wa ubunifu, sababu labda wataona wenzao wakifanya na kupewa heshima, mazingira ambao ahayakuwep yapo kwao sasa

2. Utaongeza ajira na thamani za bidhaa za kitanzania kama ubunifu utaenda sambamba na uwekezaji wa bidhaa au huduma

3. Utawapa utambulisho wangunduzi, wabunifu na wasanifu wa mawazo kwamba kwa kuwapa “CERTIFIACTE FOR TRIAL OF SUCEESS”, kituo mahalumu cha kusajili ubunifu wao ndani ya maeneo husika kutawapa wabunifu heshima kubwa kwenye familia zao

4. Utasaidia kuwa wapata watu wenye uwezo mkubwa katika kufanya mambo makubwa.

ASANTE na huu ndio mwisho wa andiko langu.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom