MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
TUJENGE MIFUMO YA UWAJIBIKAJI, KAMWE TUSITEGEMEE KUWA NA NAMBA ZA OCD AU ASKARI WA USALAMA BARABARANI.
Taifa tunapaswa kuwekeza sasa kwenye mifumo imara ya uwajibikaji ili leo na kesho hata kama kiongozi hayupo basi mifumo ifanye kazi, tuweke mifumo tukifikiria kwamba kuna siku viongozi wote hawatakuwepo kwa mkupuo na itakuwaje? Tutampigia nani simu? Tutakusanya kodi? Tutakamata wahalifu? Kesi zitaendeshwa kweli?
Ulio kuwa Umoja wa Kisovieti, wakati wa vita baridi walitengeneza kifaa na kukipa jina la Dead hand kwa maana ya mkono ulio kufa, USSR walitengeneza kifaa hicho wakiamini kwamba hata ikitokea nchi nzima viongozi wote wamekufa kwa shambulio la silaha za atomic basi kifaa cha dead hand kiweze chenyewe kufyatua makombola ya atomic kuelekea Ulaya na Marekani.Waliwaza vongozi wanaweza wasiwepo wote kwa wakati huo.
Wakati wa Hayati Rais Magufuli, Taifa lilitengeneza mfumo wa mtu, Rais alitegemewa kwa kila kitu, kuwakemea mafisadi, kuamuru mafisadi wakamatwe, kuamuru wahujumu uchumi washughurikiwe na kadhalika. Wakati wa awamu hiyo Wafanyakazi walienda kazini, wananchi walihudumiwa vyema sana Hospitali, kulikuwa na uwajibijaki wa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo tangu enzi za awamu ya kwanza.
Mara tu baada ya Rais Magufuli kufariki, kila kitu kilharibika, hakuna Fisadi anayekamatwa tena, hakuna nidhamu ya kazi tena, wahujumu uchumi hawafanywi chochote kile, mtaani misemo ya unanijua mimi imerudi kwa kasi sana. Sababu kuu ni kujenga mfumo juu ya mtu mmoja.
Kwa Tanzania kwa sasa kutokana na kutokuwa na mifumo imara ya uwajibikaji, kuna watu ni lazima awe na namba ya simu ya askari wa usalama Barabarani huyu ni wa kumsaidia hata kama yeye ndie ana kosa, Kuna watu wana namba za OCD ili tu OCD awasaidie kuwatetea, kuna wenye namba za RPC ili awasaide, kuna wenye namba za Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, kuna wenye namba za Waziri na kuna wenye namba za Majaji, Namba za mabosi wa mamlaka ya mapato yaani TRA, na kadhalika, Hizi zote ni ili mtu akipata tatizo basi hao watu watamsaidia hata kama yeye ndie mwenye makosa.
Taifa tunapaswa kujifunza sana kutokana na kilichotokea awamu ya tano na pia tujifunze hatari ya kutegemea mtu mmoja atatue matatizo yetu yote yanayo tukabili.
Madhara ya kutegemea mtu mmoja kutatua changamoto zeti ni kama vile?
Tunaweza fanya nini katika kuandaa mifumi imara ya uwajibikaji?
Taiasi za umma hivi leo zinalalimikwa sana kwa utendaji usioridhisha na wengi kufikia wakati na kuanza kumkumbuka Hayati Rais wa awamu ya Tano.
Mifumo imara ya uwajibikaji ni nguzo kuu ya ustawi wa nchi, hatuwezi fikia mapinduzi ya viwanda kama hadi leo tuna mifumo ya uwajibikaji ya kujuana, mifumo imara ya uwajibikaji itasaidia nchi kuendelea bila kutegema mtu yoyote Yule, bila kutegemea mtu wa kusaidia. Mifumo ya uwajibikaji itatuondolea kutegema kuwa na namba za watu walioko kwenye vyeo ili tu watusaidie wakati tunapo pata matatizo.
Mataifa yalioendelea kama ya Magharibi na hata Asia waliwekeza sana pia kwenye mifumo ya uwajibikaji na leo hii huwezi kutegemea mtu akutatulie shida zako bali mfumo ndio utako kutatulia shida zako.

- Huyo mtu anaweza tumia muanya huo kuonea wale wabaya wake au kufanya upendeleo wa wazi kabisa, kwa sababu yeye ndio kila kitu nazani shahidi zinaweza patikana kusapoti hii point yangu.
- Mtu unayemtegemea anaweza kufa, vipi kama unamtegemea Jaji na huyo Jaji kafariki? Utafanyaje?
- Kutumika kisiasa, Kutegemea mtu ndio awe mfumo anaweza tumia hio nafasi kujijenge yeye mwenyewe kisiasa kwa ajili ya kujidnaa na nafasi Fulani.
- Kuna kuwa na utendaji kazi wa nidhamu za uoga, Watendaji hufanya kazi kwa kuogopa mtu fulani na sio kufuata kanuni za kufanya kazi, na hiki ndicho kilicho tokea awamu ya 5 ambapo kulitokea utendaji kazi wa kufanya kazi kwa kuogopa mtu, na hii sasa inapelekea kwa sasa watu kuto kuwa na ule uoga kabisa wala uwajibikaji.
- Anaweza fariki na mifumo yote kusimama, kutegemea mtu mmoja kama mfumo madhara yake mengine ni anaye tegemewa kufariki, kuhama au kujidhuru na hii itafanya kila kitu kisimame kwa sababu alie kuwa anategemewa hayupo tena.
- Sio endelevu hata kidogo, kutegemea mtu mmoja kama mfumo sio endelevu kwa usatawi wa Taifa na hakuna tija kabisa, na ni hatari pale ambapo hayupo na hajaandaa mtu wake mwingine wa kufanya kama yeye.
- Kusababisha rushwa katika jamii.
Tunaweza fanya nini katika kuandaa mifumi imara ya uwajibikaji?
- Kufanya mageuzi makubwa katika vyombo vyote vya utaoaji haki, vyombo kama Jeshi la Polisi, Mahakama, magereza, Taasisi za upelelezi, hizi taasisi zote zinahitaji mageuzi makubwa sana ya kiutendaji, hizi zinawakilisha asilimia kubwa sana ya uwajibikaji katika jamii. Kuna matatazo makubwa sana katika vyombo ya utojai haki kama Polisi na Mahakama na ndio maana mtu kama Mh Mkuu wa mkoa wa Arusha anaamua yeye kuwa Polisi na yeye hakimu pia, hii inatokana na ukweli kwamba kuna matatizo makubwa sana kwenye hizi taasisi za uotaji haki, na hizi pia ndio zilifanya hata awamu ya 5 kukawa anategemewa mtu mmoja kututatulia matatsio yote.Ilivyo sasa taasisi zinafanya kazi kwa maagizo kutoka juu, sio kwa sheria za nchi bali ni kwa amri kutoka juu.
- Mageuzi makubwa kwenye taasisi za Serikali, kuna hitajika mageuzi makubwa sana kwenye taasisi za umma ili zifanye kazi bila kuuliza au kumuuliza mtu, ilivyo sasa hivi ufanyaji kazi ni wa kuangalia fulani kama hayupo kazi hazifanyiki, Mfano, Kwenye baadhi ya taasisi za Serikali kama mkuu wa idara Fulani hayupo labda anaumwa basi wale wa chini yake ni kama wanakuwa na likizo na kuna amabo hata kazini hawaendi kabisa kwa sababu tu mkuu wa Idara hayupo anaumwa.
Taiasi za umma hivi leo zinalalimikwa sana kwa utendaji usioridhisha na wengi kufikia wakati na kuanza kumkumbuka Hayati Rais wa awamu ya Tano.
- Elimu kubwa sana kwa raia, tukisha fanya mageuzi pia wananchi wanahitaji kupewa elimu ya uwajibikaji na kujua mtiririko wa tasisi za utoaji haki, kuliko hivi sasa kutegemea mtu kama Diwani, Mbunge, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, Waziri na hata Raisi ili awatatulie shida zo, elimu kwa raia itasaidia sana.

Upvote
0