kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hali sio nzuri nchi za Ulaya na Marekani, mfumko wa bei ya mafuta, gesi na chakula umevuruga mipango ya serikali na raia ya wazungu. Hivi karibuni majira ya baridi yataikuta Ulaya ikiwa na uhaba wa gesi na umeme kupashia nyumba joto. Hii itawafanya wazungu wengi kuja kujisalimisha nchi za joto tukiwemo Tanzania.
Tusije kuuchanganya ugeni huu na Royal tour movie yetu. Watakuja wengi kwaajili ya kujisalimisha kwa baridi na unafuu wa maisha hapa kwetu.
Serikali, utalii na wajasiliamali tukae mkao wa kula, maana bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi katika sehemu na wakati mmoja. Tujipange.