Tanzania tujipange kupokea wazungu watakaokimbia baridi kali kwao

Tanzania tujipange kupokea wazungu watakaokimbia baridi kali kwao

Hali sio nzuri nchi za Ulaya na Marekani, mfumko wa bei ya mafuta, gesi na chakula umevuruga mipango ya serikali na raia ya wazungu. Hivi karibuni majira ya baridi yataikuta Ulaya ikiwa na uhaba wa gesi na umeme kupashia nyumba joto. Hii itawafanya wazungu wengi kuja kujisalimisha nchi za joto tukiwemo Tanzania.

Tusije kuuchanganya ugeni huu na Royal tour movie yetu. Watakuja wengi kwaajili ya kujisalimisha kwa baridi na unafuu wa maisha hapa kwetu.

Serikali, utalii na wajasiliamali tukae mkao wa kula, maana bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi katika sehemu na wakati mmoja. Tujipange.
Hatuwataki hawa. NDIO MAPANYA BUKU Wenyewe.
Kwa wale ambao hawawajui hao, ni Wazungu wa Ulaya.
 
Leo nimeona wazungu wengi kule gongolamboto baa inaitwa Leo tena njia panda ya Kampala university wanakula makongoro, nikasema mtumeee kumekucha!!!! Utabiri umetimia.
 
Inaweza kuwa wasije pia
Thubutuuwee!! Kuna wazungu wengi wananiomba niwaandikie barua kama ya invitation (mwaliko)letter ili kuja kwao kuwe rahisi kidogo. Tanzania ina amani kuliko kwingine, hawatakubari kuganda kwa baridi kiboyaboya. Kumbuka kuwa hiyo baridi inayokuja inatishia kuuvunja umoja wa Ulaya, EU. Wazungu wamegawanyika juu ya vikwazo vya Urusi hali inayotishia kuvunjika kwa Muungano wao. Simchezooo!!
 
Royal Tour mlisema wazungu watamiminika hapa Tz kama mvua cha kushangaza ni matozo ndiyo yanamiminika kama gharika.
 
Thubutuuwee!! Kuna wazungu wengi wananiomba niwaandikie barua kama ya invitation (mwaliko)letter ili kuja kwao kuwe rahisi kidogo. Tanzania ina amani kuliko kwingine, hawatakubari kuganda kwa baridi kiboyaboya. Kumbuka kuwa hiyo baridi inayokuja inatishia kuuvunja umoja wa Ulaya, EU. Wazungu wamegawanyika juu ya vikwazo vya Urusi hali inayotishia kuvunjika kwa Muungano wao. Simchezooo!!
Ili kupata kituko kama hichi, Bonyeza neno UGORO tuma kwenda namba 157216
 
Back
Top Bottom