Tanzania tujitoe Jumuiya ya Madola

Tanzania tujitoe Jumuiya ya Madola

By extrapolation, tujitoe pia kwenye SADC, EAC, na UN kwani huoni faida yoyote ya kuwa mwanachama kwenye jumuia yoyote ya kimataifa.
Haya maneno ni yako sio yangu .yangu kwenye hii thread yana zungumzia jumuiya ya madola tu.

N.b: Ningependa ujibu maswali yangu [6] niliyo uliza.
 
Hujajibu swali; kumwambia mtu alisoma tena post yako huku alishaisoma na akakuta pumba tupu ni kutwanga maji ndani ya kinu. Kama unadhani ni vizuri kujitoa kwenye Jumuia ya madola weka sababu za msingi kujadiliwa siyo kuandika vijiswali visivyokuwa na mkia wala miguu.
Mkuu umesoma vizuri thread yangu . Maana mwanzoni tu mwa thread nimeeleza lengo la hii thread ni nini na nimeandika hii thread ili nipate nini kutoka kwa wadau wa humu jf .

N.b: Hebu rudi kuisoma tena upya thread neno kwa neno wenda utaelewa lengo la thread yangu.
 
Swali zuri lkn majibu ya watu ni takataka, ndiomaana tunasema JF imebadirika sana tofauti na hapo mwanzo, ambapo hakukuwa na wahuni wa kileo ambao hawajui kushusha hoja za mtoa mada zaid ya kutukana, kukashifu, kudharau na kuleta matani ya kijinga ila hao hao wapuuzi utawaona kwenye maswala ya kipumbavu kama mpira na udaku jinsi wanavyoweka attention.

Kuna ulazima wa hawa mods kufunga baadhi ya ID humu ambazo hazina maana
Sahihi kabisa.
 
Katiba imetungwa 1977, Harakati za kudai uhuru zilianza toka utawala wa Ujerumani Chifu Abushiri, Mkwawa , Kinjekitile n.k awamu ya pili chini ya mkoloni muingereza baada ya vita vya pili vya dunia 1939-1945 harakati za kudai Uhuru zikarudi tena miaka ya 1950 s. 1953 TAA, 1954 TANU Mwalimu , Bibi Titi Mohammed, Abdulhman sykes n.k wakalianzisha varangati la kumng'ang'niza mkoloni muingereza awape uhuru, Mwalimu akawekwa rumande kwa kosa la kujihusisha na siasa wakati wa ukoloni hasa hasa siasa za harakati za ukombozi wa Tanganyika kitu kilicho kuwa kimepigwa marufuku na mkoloni muingereza . 1961 tukapata Uhuru wa masharti/Uhuru wa bendera. Ningependa ujibu maswali yangu niliyo uliza.

N.b: Uhuru hatukupewa kama mama ampatiavyo mwanaye pipi.
Wala sijakuelewa na sijaona swali hapo

Soma historia ya katiba ya Tanzania sana sana ulenge kitu kiitwacho TANGANYIKA ORDER IN COUNCIL,

Halafu tofautisha kati ya Utawala na PROTECTORATE
 
Shule ya msingi ulisoma nje ya Tanzania? Maswali yako yote majibu yake wanafunzi wanafundishwa wakiwa shule ya msingi.

Kwa ufupi, hakuna hasara Taifa linapata kwa kuwa member. Faida ni nyingi, ikiwa ni pamoja na kuwa na jukwaa lenye nguvu kimataifa la kusemea mambo mbalimbali.

Usisahau kuwa nchi inapata msaada wa bure wa zaidi ya trllioni moja inayotolewa na Uingereza alimradi uzingatie demokrasia ya vyama vingi.
 
Aliyetutoka angejitutumua. Tuliye naye anatokea sehemu wanaoamini kwamba mdhungu na Mwarabu ndo wenye uwezo wa kutumia rasilimali za Mwafrika ila Mwafrika mwenyewe hawezi kujiendeleza kwa kutumia rasilimali zake.
Ila Mungu ni mwema sana kwa kulidondosha lile libwana.
 
♦️ Kuanzia katiba tuliyo nayo nasheia zoye tunazotumia zimetungwa na huyo MADOLA ambaye leo hauoni umuhimu wake

♦️ Ndiye huyo huyo madola alitotoa kwwnye ukoloni na alitulea na kutufunza mpaka tukapata uzoefu akatukabidhi nchi yetu kwa amani
Sioni hasara ya kuwa jumuia ya madola tena nafikiri tuna upendeleo flani flani kwa kuwa wanachama
 
Wala sijakuelewa na sijaona swali hapo

Soma historia ya katiba ya Tanzania sana sana ulenge kitu kiitwacho TANGANYIKA ORDER IN COUNCIL,

Halafu tofautisha kati ya Utawala na PROTECTORATE
Tulitawaliwa na Ujerumani hili halina ubishi pia tulitawaliwa na Uingereza kwa mgongo wa kuwa msimamizi wetu wala hakuna kupinda ukweli kuupaka paka rangi ndio maana utawala mzima ulikuwa unatoka London.

N.b: Turudi kwenye mada na maswali yangu tuachane na hayo mengine.
 
Tunaanzaje kujitoa wakati wanatudai??

Wakisema je hakuna kujitoa mpaka mlipe madeni yenu yote toka uhuru tutafanyaje hapo??
Kwani wanatudai shilling ngapi ? Je haziwezi kulipika ?
 
Tulitawaliwa na Ujerumani hili halina ubishi pia tulitawaliwa na Uingereza kwa mgongo wa kuwa msimamizi wetu wala hakuna kupinda ukweli kuupaka paka rangi ndio maana utawala mzima ulikuwa unatoka London.

N.b: Turudi kwenye mada na maswali yangu tuachane na hayo mengine.
Umekwisha soma historia ya katiba ya (Tanganyika) ilitungwa wapi na kwa sheria gani?
 
- Habari za muda huu wana jamii wenzangu, natumai ni njema.

- Nilikuwa na dukuduku kuhusu uwepo wa taifa letu la Tanzania Jumuiya ya Madola, dukuduku langu limezaa maswali kadhaa yenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu wana jamii wenzangu.

1. Kwanini Taifa la Tanzania lipo Jumuiya ya Madola?

2. Ni faida zipi tunapata kuhusu uwepo wetu Jumuiya ya Madola?

3. Ni hasara zipi tutapata endapo hatuta kuwepo kwenye Jumuiya ya Madola?

4. Tukipima katika mizani faida na hasara za Jumuiya ya Madola kwetu, kipi kitakuwa ni bora kwetu? Tanzania kuendelea kuwepo katika jumuiya ya madola au tujitoe na kuendeleza maisha yetu ya kawaida kama Taifa nje ya Jumuiya ya Madola?

5. Kwa nini taifa la USA na Hongkong (China) hayapo Jumuiya ya Madola?

6. Je, inawezekana kwa njia ya amani member wa Jumuiya ya Madola akitaka kutoka naye akaruhusiwa kufanya hivyo?
View attachment 2353028
N.b: Karibuni wadau mwenye swali pia anaweza kuongeza swali lake.
Ukijigaragua ukajitoa ,watu wako na wewe mwenyewe mtakufa njaa.
 
Back
Top Bottom