Wewe uliishi kipindi cha ujamaa au umesoma tuu history ? Kwa data zipi za mwaka 1987 kuwa Tanzania ilikuwa imara kiuchumi kuliko Kenya??
Kimsingi by that time kutokana na vita vya Uganda na Sera zetu za ujamaa zilisababisha nchi kuwa na madeni makubwa saana
Vile vile wizi na ufisadi pamoja na uhujumu uchumi ulisababisha mashirika mengi ya umma kutokuwa na perfomance nzuri.
Wananchi kutokuielewa vzr Sera ya ujamaa na kujitegemea hili pia lilikuwa tatzo.
Ili kuinusuru nchi kulikuwa hakuna namna lazima tuingie kwenye mfumo WA uchumi huria.....
Shida yetu SASA baaada ya kuingia huko ufisadi na wizi bado ni tatzo pesa nyingi za kuleta maendeleo Kwa umma zinanufaisha watu wachache saana (wanasiasa).
Uwepo wa tofauti kubwa ya kipato Kati ya walio nacho na wasio nacho ni matokeo ya kimfumo hususani huu WA kibepari Ila serekali SASA ndio Baba WA wasio na nacho inatakiwa ipambane kutoa huduma Bora za msingi kwa wasio nacho mfano elimu Afya miundombinu n.k...
But Kwa bahati mbaya viongozi hawatuthamini watu wa Hali ya Chini haha tunaishi Kama yatima tuu kwenye nchi hii.
Lastly ni vema tujikite kwenye kuchapa Kazi kujikwamua kwenye kundi la wasionacho..
Hali yetu ilikuwa dhaifu sana hata kabla ya Vita ya Kagera
Ujamaa ni mfumo unaolea wavivu kwa kuwa wana uhakika wa kipato sawa na wachapa kazi.
Ilikuwa ukifikia level ya kuwa Afisa Mwandamizi Serikalini unapelekwa kwny semina ya uongozi na moja ya mafunzo muhimu ni kupigwa marufuku kujishughulisha na shughuli zozote zitazokuongezea kipato nje ya Ajira
Kizazi cha sasa huenda wasiamiani ila tulipigwa marufuku kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi,
tunashukuru sana 1992 Comrade Ally Hassan Mwinyi alikutana na miamba wenzie wakimya lakini wenye misimamo kina Comrade Ibrahim Kaduma kulifutilia mbali Azimio lililokuwa linakiuka misingi ya haki za binadamu
bila ya ushujaa ule sasa hivi sijui hali ingekuaje, imagine kumiliki fridge ya kupoza maji ya kunywa ilikuwa ni uhujunu uchumi, kumiliki TV ni unyonyaji.
Viongozi waliokuwa wanasimamia kuhakikisha hatuna Mafriji wala TV ilikuwa tukienda kuwatembelea kwao tunakunywa maji baridi na tunaangalia movie za kina Sarafina
Waliokuwa wanazuia tusiwinde wanyama pori kwa kitoweo ilikuwa tukienda kuwatembelea lazima tule mishikaki ya Pongo na Swala
ujamaa ni mfumo wa unafiki
Sent from my SM-G9500 using
JamiiForums mobile app