Mkuu
Burkinabe, kwanza asante kwa mjadala huu, japo umejiita mzee, kwa posts zako wewe ni kijana wa 80s, wazee humu JF tupo ila tumebaki wachache wale wangumu wenye uwezo wa kuvumilia ujinga ujinga wa vijana humu.
Nimefurahi kuona bado kuna vijana wa Nyerere type, wanaoamini kwenye Ujamaa. Nakuunga mkono, Tanzania ingekuwa njema zaidi na salama zaidi kwenye Tanzania ya Ujamaa kuliko Tanzania hii ya ubepari.
Ukilisoma Azimio la Arusha lililotangaza Tanzania kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ni zuri kabisa, tatizo lilikuja kwenye utekelezaji, tulifanya mistakes ya kwanza ni kwenye mzizi wa mfumo wenyewe wa Ujamaa wa Mwalimu, ulikuwa na kosa moja kubwa la msingi ambalo ndilo chanzo cha kufeli kwa Ujamaa. Kosa hilo nililitaja kwenye uzi wangu huu
Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Hivyo the 1st mistake ya Ujamaa wa Nyerere ni kwenye root cause ya kuamini ili tuendelee tulihitaji vitu 4, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, vitu vyote hivi tulikuwa navyo, kwanini tulishindwa kuendelea?. Kosa la kwanza ni kuaminishwa na Mwalimu kuwa fedha, sio msingi, fedha ni matokeo!.
That was wrong, ili tuendelee tulihitaji mitaji, bila mitaji hatuwezi ku exploit potentials zozote tulizo nazo, hivyo licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye rutuba, kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kulikomboa taifa, bila mitaji ya kufanya Mapinduzi ya kilimo, kilimo hakiwezi kuwa productive hivyo hapa Nyerere alifeli.
Tulipofanya Operesheni Vijiji, that was another mistake, Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walimgomea ndio makabila yenye afadhali kiuchumi.
Ilipojuja vita ya Kagera ndio ikafunga kazi, uchumi wetu ukadidimia kabisa, IMF na WB wakatuletea masharti ya kutukopesha na kutulazimisha kuukumbatia ubepari, hivyo Mwalimu Nyerere akaamua kuliko kugeuka nyuma ageuke jiwe, bora anyooshe mikono juu na kuachia ngazi, ndipo akang'atuka na kumpisha Mwinyi aliyekubali kila kitu.
Mkapa, na JK nao played their part lakini the biggest impact came with JPM. Huyu alikuwa kama Nyerere, kupitia Magufulification, alikuwa anairudisha Tanzania kuwa nchi ya Kijamaa na chama kimoja. Akaanzisha elimu bure, alikuwa anakuja na afya bure!, Mungu ndio akamchukua.
Mimi ni mtu wa Nyerere type, na nimefurahi kuona watu wa Nyerere type bado wapo wengine ni hawa
Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! na hawa
Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa na huyu
Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa? na huyu
Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
Jumapili Njema
P