Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Kwa hiyo si kweli kwamba ugumu wa maisha kwa miaka hiyo ambayo imekuwa ikirejelewa na wapinga Ujamaa wengi, ilisababishwa na Ujamaa wenyewe, bali ulisababishwa na mambo niliyoyataja hapo juu na wahujumu uchumi kwa kiasi walichangia hali ya ugumu wa maisha kwa wananchi pia.
Kabisa kabisa ! Sisi wengine tulikuwepo wakati ule na sasa pia bado tupo we knew and we know the whole truth !!
Hatujalishwa matango pori sisi !!
 
Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Mkuu Burkinabe, kwanza asante kwa mjadala huu, japo umejiita mzee, kwa posts zako wewe ni kijana wa 80s, wazee humu JF tupo ila tumebaki wachache wale wangumu wenye uwezo wa kuvumilia ujinga ujinga wa vijana humu.

Nimefurahi kuona bado kuna vijana wa Nyerere type, wanaoamini kwenye Ujamaa. Nakuunga mkono, Tanzania ingekuwa njema zaidi na salama zaidi kwenye Tanzania ya Ujamaa kuliko Tanzania hii ya ubepari.

Ukilisoma Azimio la Arusha lililotangaza Tanzania kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ni zuri kabisa, tatizo lilikuja kwenye utekelezaji, tulifanya mistakes ya kwanza ni kwenye mzizi wa mfumo wenyewe wa Ujamaa wa Mwalimu, ulikuwa na kosa moja kubwa la msingi ambalo ndilo chanzo cha kufeli kwa Ujamaa. Kosa hilo nililitaja kwenye uzi wangu huu Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Wanabodi,

Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere alikuwa ni muumini wa falsafa ya "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu" ,

Naomba kutumia falsafa mbili kutolea mifano Falsafa ya Mwalimu Nyerere, na Falsafa ya Adam Smith.

Falsafa ya Mwalimu Nyerere: Ili Tuendelee Tunahitaji Vitu Vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?. Kati ya watu milioni 55 wa Tanzania, watu milioni 15 wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.

Nyerere alipotangaza Azimio la Arusha la siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, alisema kazi ya kujenga ujamaa ingechukua miaka 30. Lakini siku anatangaza kung'atuka alikiri kuwa tumekosea!, akakiri kwa kusema "kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa"

Je, mnajua tulikosea wapi?. Tumsikilize mwanauchumi Adam Smith kwenye theory yake ambayo itaonyesha kosa la Nyerere.

Economic Theory Ya Adam Smith-Land, Labor, Capital & Entrepreneurship
Katika theory hii ya Adam Smith, inashabihiana na theory ya Nyerere kwenye watu na ardhi, na itatofautiana na Nyerere kwenye Siasa Safi na Uongozi Bora, Adam Smith anasema tunahitaji Capital na Entrepreneurship. Hivyo theory ya Nyerere kuweka siasa safi na uongozi bora ni kitu kile kile, kwenye theory ya Nyerere kulikosekana Capital, Nyerere alifanya kosa kubwa kwa kuamini fedha sii msingi bali ni matokeo, but in reality, pesa ni msingi sana wa kupata mitaji. Kama una watu, na ardhi, na una siasa safi, na uongozi bora, bila mitaji ya kuwawezesha hao watu kuitumia ardhi kuzalisha mali, tulitwanga maji kwenye kinu kutegemea kilimo cha jembe la mkono, kutokuwa na mitaji ya kuchimba madini, mitaji ya kujenga viwanda. Mwinyi alipoingia, alifanya sera ya ubinafsishaji kwa uongo kuwa fedha za ubinafsishaji zitawekwa kwenye mfuko maalum wa mitaji kuwawezesha Watanzania ili waje kuwa wamiliki wa uchumi wao!, it was all a lie na hapa ndipo matabaka ya wenye nacho na wasionacho yalipoanzia!.
Hivyo the 1st mistake ya Ujamaa wa Nyerere ni kwenye root cause ya kuamini ili tuendelee tulihitaji vitu 4, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, vitu vyote hivi tulikuwa navyo, kwanini tulishindwa kuendelea?. Kosa la kwanza ni kuaminishwa na Mwalimu kuwa fedha, sio msingi, fedha ni matokeo!.

That was wrong, ili tuendelee tulihitaji mitaji, bila mitaji hatuwezi ku exploit potentials zozote tulizo nazo, hivyo licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye rutuba, kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kulikomboa taifa, bila mitaji ya kufanya Mapinduzi ya kilimo, kilimo hakiwezi kuwa productive hivyo hapa Nyerere alifeli.

Tulipofanya Operesheni Vijiji, that was another mistake, Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walimgomea ndio makabila yenye afadhali kiuchumi.

Ilipojuja vita ya Kagera ndio ikafunga kazi, uchumi wetu ukadidimia kabisa, IMF na WB wakatuletea masharti ya kutukopesha na kutulazimisha kuukumbatia ubepari, hivyo Mwalimu Nyerere akaamua kuliko kugeuka nyuma ageuke jiwe, bora anyooshe mikono juu na kuachia ngazi, ndipo akang'atuka na kumpisha Mwinyi aliyekubali kila kitu.

Mkapa, na JK nao played their part lakini the biggest impact came with JPM. Huyu alikuwa kama Nyerere, kupitia Magufulification, alikuwa anairudisha Tanzania kuwa nchi ya Kijamaa na chama kimoja. Akaanzisha elimu bure, alikuwa anakuja na afya bure!, Mungu ndio akamchukua.

Mimi ni mtu wa Nyerere type, na nimefurahi kuona watu wa Nyerere type bado wapo wengine ni hawa Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! na hawa Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa na huyu Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa? na huyu Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...

Jumapili Njema
P
 
Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Unapenda ujamaa ?
 
Hatutakiwi kurudi kwenye ujamaa ule wala kubaki katika ubepari huu. Kwa maoni yangu tunatakiwa kuwa katikati ya hayo mawili...Tuchukue Yale ya wakati ule mazuri na haya ya Sasa mazuri Ili tuweze kuwa taifa Bora kabisa la mfano Africa.

Hii inawezekana kama tutapata viongozi ambao watakubali nchi iishi kile kilicho Bora na kuacha kupelekea maslahi Yao binafsi mbele
China wamefanya hivyo na wamepiga hatua.

Mambo mengi hutegemea political will ili yaende.

Sisi hatuna viongozi wa aina ya China na Russia.

Yaani viongozi mabeberu lakini wazalendo, hao hatuna.
 
Huna akili!

Nadhani hata kuzaliwa utakuwa umezaliwa mwaka 1995.

Kama ulikuwa na akili miaka ya 1982- 1985 na ulishuhudia namna watu kwalivyokuwa wanavaa viraka na kuogea majani ya mipapai kama sabuni sidhani kama unaweza kuja kuandika huu upuuzi wako hapa.

Ujamaa ni laana.
Wewe ndio huna akili na ikiwezekana una matope kabisa,badlands ya kusema athali za ujamaa katika kipindi chake wewe unaleta athali za ujamaa baada ya mabeberu kuwapiga pini juu ya kuendesha Nchi kwa sera ya Ujamaa.
 
Mto hoja wewe ni Mwamba sana,tumerudi nyuma mara 1000 na sababu kuu ni moja veranda vyote vilivyojengwa na kufanya kazi katika kuishi sera ya ubepari vilibinafisihwa na wajanja wachache wakanufaika na badaye vilikufa-na matatizo ya kiuchumi kama kukosekana kwa ajili yakaanzia hapo.
 
Mkuu nimekuwekea hapo rejea ya gazeti la The Citizen la tarehe 17/04/2017 ambalo lilinukuu toka IMF. Ofcourse awamu ya 5 kama tungeenda nayo kwa miaka 10 tu nina uhakika Tanzania ingekuwa kubwa tena kama ilivyokuwa zamani. Lakini kwa mwendo huu wa kutambaa tunaoenda nao kwa sasa, tutasubiri sana kwa kweli.
Kwa sasa watanzania wengi hawana matumaini na hawaijui kesho yao, nchi imekuwa ya ovyo maradufu.
 
Alifanyiwa figisu na mabeberu ili kukwepa aibu ndio akaamua kung'atuka.
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
 
Wewe uliishi kipindi cha ujamaa au umesoma tuu history ? Kwa data zipi za mwaka 1987 kuwa Tanzania ilikuwa imara kiuchumi kuliko Kenya??

Kimsingi by that time kutokana na vita vya Uganda na Sera zetu za ujamaa zilisababisha nchi kuwa na madeni makubwa saana

Vile vile wizi na ufisadi pamoja na uhujumu uchumi ulisababisha mashirika mengi ya umma kutokuwa na perfomance nzuri.

Wananchi kutokuielewa vzr Sera ya ujamaa na kujitegemea hili pia lilikuwa tatzo.

Ili kuinusuru nchi kulikuwa hakuna namna lazima tuingie kwenye mfumo WA uchumi huria.....

Shida yetu SASA baaada ya kuingia huko ufisadi na wizi bado ni tatzo pesa nyingi za kuleta maendeleo Kwa umma zinanufaisha watu wachache saana (wanasiasa).

Uwepo wa tofauti kubwa ya kipato Kati ya walio nacho na wasio nacho ni matokeo ya kimfumo hususani huu WA kibepari Ila serekali SASA ndio Baba WA wasio na nacho inatakiwa ipambane kutoa huduma Bora za msingi kwa wasio nacho mfano elimu Afya miundombinu n.k...

But Kwa bahati mbaya viongozi hawatuthamini watu wa Hali ya Chini haha tunaishi Kama yatima tuu kwenye nchi hii.

Lastly ni vema tujikite kwenye kuchapa Kazi kujikwamua kwenye kundi la wasionacho..
Mkuu ulizoandika hapa ni propaganda,ukweli ni kuwa kuanzia miaka ya 1970's USA alianzisha mgogoro wa kiuchumi kupitia uhaba wa mafuta wenye lengo la kuua Sera ya ujamaa Duniani ili kuendeleza ukiranja wake wa Dunia ili apate uungaji mkono na kudidimiza Russia na China.
 
Ni kweli unachosema Mkuu, kuna baadhi ya mambo yaliyopelekea hiyo hali ngumu;
1. Athari ya njaa iliyotokana na ukame miaka ya mwanzoni mwa 70 (1973/1974)
2. Vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idi Amin
Hali ngumu ya kimaisha ilitengenezwa na USA,jamani someni haya mambo.
 
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
Miradi ya ujamaa ilibinafisishwa,emu tuleteee maendeleo ya hiyo miradi baada ya kubinafisishwa.
 
Miradi yake ya kijamaa ilifeli, kuficha aibu na hasara aliyoingia akamwachia kijiti Mwinyi ila akamsihi aje na sera ya capitalism ili apate misaada hali ilikuwa mbaya
IMF walimfinya na kwakua hakutaka kukubaliana na masharti yao akasepa.
 
Watu wengi wanamlaumu Nyerere na kuponda ujamaa wakidhani USA anauchukia ujamaa.
Ujamaa ni usoshalist ambao upo Israel ambao wana kibbutzim na Moshav.
Sweden ni wajamaa. Ujerumani ni wajamaa na ndio maana wana mpaka chama cha kijamaa (SDU cha akina Gerhard Shroder)
Japan ni wajamaa.

Na fuatilia mataifa yenye ujamaa, hakuna umasikini wala hakuna tajiri sana kama Elon Musk ila unashangaa taifa lenye uchumi mkubwa Ulaya ni wajamaa.
Hata timu kubwa ya kandanda kama Beyern Minchen inaendeshwa kijamaa.

Nyerere alikosa watu ambao walikuwa falsafa ya kujenga uchumi as kijamaa. Bahati mbaya alimpa Kawawa kuongoza jahazi wakati akiwa hajui model ya ujamaa inafanya vip kazi.
 
Mkuu Burkinabe, kwanza asante kwa mjadala huu, japo umejiita mzee, kwa posts zako wewe ni kijana wa 80s, wazee humu JF tupo ila tumebaki wachache wale wangumu wenye uwezo wa kuvumilia ujinga ujinga wa vijana humu.

Nimefurahi kuona bado kuna vijana wa Nyerere type, wanaoamini kwenye Ujamaa. Nakuunga mkono, Tanzania ingekuwa njema zaidi na salama zaidi kwenye Tanzania ya Ujamaa kuliko Tanzania hii ya ubepari.

Ukilisoma Azimio la Arusha lililotangaza Tanzania kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ni zuri kabisa, tatizo lilikuja kwenye utekelezaji, tulifanya mistakes ya kwanza ni kwenye mzizi wa mfumo wenyewe wa Ujamaa wa Mwalimu, ulikuwa na kosa moja kubwa la msingi ambalo ndilo chanzo cha kufeli kwa Ujamaa. Kosa hilo nililitaja kwenye uzi wangu huu Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Hivyo the 1st mistake ya Ujamaa wa Nyerere ni kwenye root cause ya kuamini ili tuendelee tulihitaji vitu 4, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, vitu vyote hivi tulikuwa navyo, kwanini tulishindwa kuendelea?. Kosa la kwanza ni kuaminishwa na Mwalimu kuwa fedha, sio msingi, fedha ni matokeo!.

That was wrong, ili tuendelee tulihitaji mitaji, bila mitaji hatuwezi ku exploit potentials zozote tulizo nazo, hivyo licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye rutuba, kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kulikomboa taifa, bila mitaji ya kufanya Mapinduzi ya kilimo, kilimo hakiwezi kuwa productive hivyo hapa Nyerere alifeli.

Tulipofanya Operesheni Vijiji, that was another mistake, Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walimgomea ndio makabila yenye afadhali kiuchumi.

Ilipojuja vita ya Kagera ndio ikafunga kazi, uchumi wetu ukadidimia kabisa, IMF na WB wakatuletea masharti ya kutukopesha na kutulazimisha kuukumbatia ubepari, hivyo Mwalimu Nyerere akaamua kuliko kugeuka nyuma ageuke jiwe, bora anyooshe mikono juu na kuachia ngazi, ndipo akang'atuka na kumpisha Mwinyi aliyekubali kila kitu.

Mkapa, na JK nao played their part lakini the biggest impact came with JPM. Huyu alikuwa kama Nyerere, kupitia Magufulification, alikuwa anairudisha Tanzania kuwa nchi ya Kijamaa na chama kimoja. Akaanzisha elimu bure, alikuwa anakuja na afya bure!, Mungu ndio akamchukua.

Mimi ni mtu wa Nyerere type, na nimefurahi kuona watu wa Nyerere type bado wapo wengine ni hawa Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! na hawa Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa na huyu Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa? na huyu Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...

Jumapili Njema
P
Mkuu tunashukuru sana kwa bandiko hili lililosheheni "madini" tupu. Binafsi huwa navutiwa sana na nyuzi zako pamoja na michango yako kwa ujumla ukiachilia michache ambayo kwa kweli binafsi huwa nafikiria kuna watu huwa wanatumia account yako! Huyu aliyetoa "madini" haya ndo Pascal Mayala original.
😁😁😁😁
Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Mkuu Burkinabe, kwanza asante kwa mjadala huu, japo umejiita mzee, kwa posts zako wewe ni kijana wa 80s, wazee humu JF tupo ila tumebaki wachache wale wangumu wenye uwezo wa kuvumilia ujinga ujinga wa vijana humu.

Nimefurahi kuona bado kuna vijana wa Nyerere type, wanaoamini kwenye Ujamaa. Nakuunga mkono, Tanzania ingekuwa njema zaidi na salama zaidi kwenye Tanzania ya Ujamaa kuliko Tanzania hii ya ubepari.

Ukilisoma Azimio la Arusha lililotangaza Tanzania kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ni zuri kabisa, tatizo lilikuja kwenye utekelezaji, tulifanya mistakes ya kwanza ni kwenye mzizi wa mfumo wenyewe wa Ujamaa wa Mwalimu, ulikuwa na kosa moja kubwa la msingi ambalo ndilo chanzo cha kufeli kwa Ujamaa. Kosa hilo nililitaja kwenye uzi wangu huu Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?
Hivyo the 1st mistake ya Ujamaa wa Nyerere ni kwenye root cause ya kuamini ili tuendelee tulihitaji vitu 4, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, vitu vyote hivi tulikuwa navyo, kwanini tulishindwa kuendelea?. Kosa la kwanza ni kuaminishwa na Mwalimu kuwa fedha, sio msingi, fedha ni matokeo!.

That was wrong, ili tuendelee tulihitaji mitaji, bila mitaji hatuwezi ku exploit potentials zozote tulizo nazo, hivyo licha ya kuwa na watu wa kutosha na ardhi yenye rutuba, kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kulikomboa taifa, bila mitaji ya kufanya Mapinduzi ya kilimo, kilimo hakiwezi kuwa productive hivyo hapa Nyerere alifeli.

Tulipofanya Operesheni Vijiji, that was another mistake, Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walimgomea ndio makabila yenye afadhali kiuchumi.

Ilipojuja vita ya Kagera ndio ikafunga kazi, uchumi wetu ukadidimia kabisa, IMF na WB wakatuletea masharti ya kutukopesha na kutulazimisha kuukumbatia ubepari, hivyo Mwalimu Nyerere akaamua kuliko kugeuka nyuma ageuke jiwe, bora anyooshe mikono juu na kuachia ngazi, ndipo akang'atuka na kumpisha Mwinyi aliyekubali kila kitu.

Mkapa, na JK nao played their part lakini the biggest impact came with JPM. Huyu alikuwa kama Nyerere, kupitia Magufulification, alikuwa anairudisha Tanzania kuwa nchi ya Kijamaa na chama kimoja. Akaanzisha elimu bure, alikuwa anakuja na afya bure!, Mungu ndio akamchukua.

Mimi ni mtu wa Nyerere type, na nimefurahi kuona watu wa Nyerere type bado wapo wengine ni hawa Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! na hawa Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa na huyu Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa? na huyu Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...

Jumapili Njema
P
Nathubutu kusema wewe Pascal Mayalla ni "genius ". Una uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kupembua mambo.
Nina imani siku moja utatufaa sana sehemu mojawapo serikalini endapo tukipata viongozi wazalendo.
 
Back
Top Bottom