Mkuu 'Proved', wewe mwenyewe bila shaka umegundua mleta mada kaweka mada ya kichokonozi kuamsha hisia za watu tu kwa jinsi alivyo iwasilisha.
Tuondoke huko kwenye 'dogma' za kizamani enzi za "Vita Baridi". Hizi ni enzi tofauti kabisa nasi tunatakiwa kuangalia maslahi ya nchi yetu katika mazingira haya ya leo, siyo yale ya juzi.
Mleta mada analaumu akina Mwinyi na wengineo; lakini anasahau kwamba tayari tulikuwa kwenye matatizo makubwa kama nchi siyo kwa sababu ya Ujamaa, bali haliya uchumi wa duniaani kote ilikuwa na mtikisiko; na kwa bahati mbaya sana kwetu tukawa na majanga mfululizo wakati huo huo. Vita Kagera, ukame uliosababisha ukosefu wa chakula, n.k.
Ni wapi katika ukanda huu ambapo hapakutokea mtikisiko wakati huo, iwe wana siasa za kibepari au za kijamaa Hapo jirani enzi za Moi huwezi kusema uchumi wao ulikuwa mzuri, ukiacha tu hizi propaganda zisizokuwa na miguu.
Kuna mambo ninayokubaliana na mkuu 'Burkinabe' katika mada yake, ikiwa ni pamoja na upotofu wa msimamo wa serikali zetu tukea enzi za Ruksa, Mkapa na Kikwete.
Matatizo yetu sasa yatakayotuchelewesha kusonga mbele kimaendeleo sasa hivi, siyo sababu ya siasa za kijamaa au kibepari. Tumekwishaona kwamba, hata katika ujamaa maendeleo yanawezekana, kama ilivyo katika ubepari. China katufundisha kuwa 'Socialist Economy" inao uwezo wa kuliondoa taifa katika rindi la umaskini.
Na tunajua pia, kwamba hata katika ubepari, nchi inaweza kabisa isifanikiwe bila ya kuweka mkazo katika baadhi ya mambo muhimu, kama kubana ufisadi na kuweka mfumo mzuri wa kiutawala ili shughuli za wananchi ziende vizuri.
Hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea wawekezaji toka nje na huku sisi wenyewe tukipanga kupeleka manamba nchi za nje.
Hali kadhalika, hatuwezi kuendelea kama serikali haiweki mipango madhubuti kujenga uwezo wetu wenyewe kujenga taifa letu
Kamwe hatuwezi kuendelea kama tunayo serikali isiyokuwa na uwezo wa kuwabana mabepari na mijizi ili raslimali zetu zisaidie ujenzi wa taifa letu.
Ukitaka kufungua nchi, hakikisha umejijengea uwezo wa kuhakikisha kuwa hukujisahau na kuruhusu kuliwa hata usikotaka uliwe.
Socialist economy