Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Mkuu 'Proved', wewe mwenyewe bila shaka umegundua mleta mada kaweka mada ya kichokonozi kuamsha hisia za watu tu kwa jinsi alivyo iwasilisha.

Tuondoke huko kwenye 'dogma' za kizamani enzi za "Vita Baridi". Hizi ni enzi tofauti kabisa nasi tunatakiwa kuangalia maslahi ya nchi yetu katika mazingira haya ya leo, siyo yale ya juzi.

Mleta mada analaumu akina Mwinyi na wengineo; lakini anasahau kwamba tayari tulikuwa kwenye matatizo makubwa kama nchi siyo kwa sababu ya Ujamaa, bali haliya uchumi wa duniaani kote ilikuwa na mtikisiko; na kwa bahati mbaya sana kwetu tukawa na majanga mfululizo wakati huo huo. Vita Kagera, ukame uliosababisha ukosefu wa chakula, n.k.

Ni wapi katika ukanda huu ambapo hapakutokea mtikisiko wakati huo, iwe wana siasa za kibepari au za kijamaa Hapo jirani enzi za Moi huwezi kusema uchumi wao ulikuwa mzuri, ukiacha tu hizi propaganda zisizokuwa na miguu.

Kuna mambo ninayokubaliana na mkuu 'Burkinabe' katika mada yake, ikiwa ni pamoja na upotofu wa msimamo wa serikali zetu tukea enzi za Ruksa, Mkapa na Kikwete.

Matatizo yetu sasa yatakayotuchelewesha kusonga mbele kimaendeleo sasa hivi, siyo sababu ya siasa za kijamaa au kibepari. Tumekwishaona kwamba, hata katika ujamaa maendeleo yanawezekana, kama ilivyo katika ubepari. China katufundisha kuwa 'Socialist Economy" inao uwezo wa kuliondoa taifa katika rindi la umaskini.

Na tunajua pia, kwamba hata katika ubepari, nchi inaweza kabisa isifanikiwe bila ya kuweka mkazo katika baadhi ya mambo muhimu, kama kubana ufisadi na kuweka mfumo mzuri wa kiutawala ili shughuli za wananchi ziende vizuri.

Hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea wawekezaji toka nje na huku sisi wenyewe tukipanga kupeleka manamba nchi za nje.

Hali kadhalika, hatuwezi kuendelea kama serikali haiweki mipango madhubuti kujenga uwezo wetu wenyewe kujenga taifa letu

Kamwe hatuwezi kuendelea kama tunayo serikali isiyokuwa na uwezo wa kuwabana mabepari na mijizi ili raslimali zetu zisaidie ujenzi wa taifa letu.

Ukitaka kufungua nchi, hakikisha umejijengea uwezo wa kuhakikisha kuwa hukujisahau na kuruhusu kuliwa hata usikotaka uliwe.

Socialist economy
 
Huna akili!

Nadhani hata kuzaliwa utakuwa umezaliwa mwaka 1995.

Kama ulikuwa na akili miaka ya 1982- 1985 na ulishuhudia namna watu kwalivyokuwa wanavaa viraka na kuogea majani ya mipapai kama sabuni sidhani kama unaweza kuja kuandika huu upuuzi wako hapa.

Ujamaa ni laana.
Ilikuwa ni hatari miaka hiyo vijana wengi wa mjini walianza kuzamia meli kwenda ulaya
 
Huyu dogo ndo anataka kuturudisha kule.

Hawa vijana wa juzi wana matatizo sana. Hawajui nchi yetu enzi izo ilikuwa kama Ethiopia raia wanaikimbia kwa kuzamia meli
Maendeleo mazuri ni yale ambayo yanawajumuisha wananchi wote kwa ujumla Mkuu.
 
Umeshindwa kuelezea
Learning Experience huwa hailezewi. Ndio maana nilitaka ujue dhana ya participant observation.

Nakuelezea Sweden, Germany, Slovenia na Israel huko nimefika na kuishi na ninachokushauri ufike, uishi na ujipatie ufahamu kwa kuwa na real experience ya usoshalist
 
Hiki ndiyo kitu gani. Kilifanyika wapi hiki?
It's a suggestion, pure market economy with very limited government intervention is a way to go. Or rather serikali ibaki kama regulator na policy maker ila uchumi mzima uwe unaendeshwa na private sector. Hata chadema ndio sera yetu, market economy ambapo hata barabara za lami yanaweza jengwa na mtu binafsi then akatoza charges kwa muda fulani hela yake irudi.
 
Mkuu 'Proved', wewe mwenyewe bila shaka umegundua mleta mada kaweka mada ya kichokonozi kuamsha hisia za watu tu kwa jinsi alivyo iwasilisha.

Tuondoke huko kwenye 'dogma' za kizamani enzi za "Vita Baridi". Hizi ni enzi tofauti kabisa nasi tunatakiwa kuangalia maslahi ya nchi yetu katika mazingira haya ya leo, siyo yale ya juzi.

Mleta mada analaumu akina Mwinyi na wengineo; lakini anasahau kwamba tayari tulikuwa kwenye matatizo makubwa kama nchi siyo kwa sababu ya Ujamaa, bali haliya uchumi wa duniaani kote ilikuwa na mtikisiko; na kwa bahati mbaya sana kwetu tukawa na majanga mfululizo wakati huo huo. Vita Kagera, ukame uliosababisha ukosefu wa chakula, n.k.

Ni wapi katika ukanda huu ambapo hapakutokea mtikisiko wakati huo, iwe wana siasa za kibepari au za kijamaa Hapo jirani enzi za Moi huwezi kusema uchumi wao ulikuwa mzuri, ukiacha tu hizi propaganda zisizokuwa na miguu.

Kuna mambo ninayokubaliana na mkuu 'Burkinabe' katika mada yake, ikiwa ni pamoja na upotofu wa msimamo wa serikali zetu tukea enzi za Ruksa, Mkapa na Kikwete.

Matatizo yetu sasa yatakayotuchelewesha kusonga mbele kimaendeleo sasa hivi, siyo sababu ya siasa za kijamaa au kibepari. Tumekwishaona kwamba, hata katika ujamaa maendeleo yanawezekana, kama ilivyo katika ubepari. China katufundisha kuwa 'Socialist Economy" inao uwezo wa kuliondoa taifa katika rindi la umaskini.

Na tunajua pia, kwamba hata katika ubepari, nchi inaweza kabisa isifanikiwe bila ya kuweka mkazo katika baadhi ya mambo muhimu, kama kubana ufisadi na kuweka mfumo mzuri wa kiutawala ili shughuli za wananchi ziende vizuri.

Hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea wawekezaji toka nje na huku sisi wenyewe tukipanga kupeleka manamba nchi za nje.

Hali kadhalika, hatuwezi kuendelea kama serikali haiweki mipango madhubuti kujenga uwezo wetu wenyewe kujenga taifa letu

Kamwe hatuwezi kuendelea kama tunayo serikali isiyokuwa na uwezo wa kuwabana mabepari na mijizi ili raslimali zetu zisaidie ujenzi wa taifa letu.

Ukitaka kufungua nchi, hakikisha umejijengea uwezo wa kuhakikisha kuwa hukujisahau na kuruhusu kuliwa hata usikotaka uliwe.

Socialist economy
Mkuu, Kalamu!

Mchango wako wa Mada Husika ni mzuri sana! Mimi binafsi naunga mkono tuwe na "A Socialist Economy!
 
It's a suggestion, pure market economy with very limited government intervention is a way to go. Or rather serikali ibaki kama regulator na policy maker ila uchumi mzima uwe unaendeshwa na private sector. Hata chadema ndio sera yetu, market economy ambapo hata barabara za lami yanaweza jengwa na mtu binafsi then akatoza charges kwa muda fulani hela yake irudi.
Kuna mambo yanapaswa fanywa na watu binafsi na kuna mambo hayapaswi fanya na sekta binafsi labda kwa mkataba wa mashirikiano baina ya sekta binafsi na serikali.

Huo mfano uliotoa wewe ni mmoja ya mambo hayapaswi kuachiwa sekta binafsi kutekeleza. Serikali haipaswi kuona uvivu kujengea barabara raia wake ili kurahisisha shughuli za maendeleo.

Mfano upo hivi serikali yaweza gharamia ujenzi wa miundombinu kama barabara/reli wa mabilioni ya pesa na pesa isiweze kurudi kwa haraka na kuacha madeni ila shughuli za kiuchumi zilizo rahisishwa au kuwezeshwa kupitia miundombinu hiyo zikawa na manufaa kwa maendeleo ya eneo husika.

Sekta muhimu kwa taifa hazipaswi kuachwa mikononi wa mwa watu binafsi zitageuka kuwa ghali na ushindani wa gharama za uendeshaji wakati jukumu namba moja la serikali ni kutoa hudua kwa raia kwa uhakika.

Sekta ya mawasiliano, miundombinu, nishati, afya hizi ni sekta muhimu ambazo hazipaswi kuwa ndani ya mikono michache ya watu binafsi ni bora ziwepo mikononi mwa mashirikiano kati ya serikali+watu binafsi.
 
Serikali inajukumu la kupanga uchumi wetu uwe wapi, utoke wapi na uende wapi.

Serikali inapaswa kujenga uangalizi na ufuatiliaji wa soko kwa wakati wote.

Serikali kuu inapaswa kutengeneza maeneo maalumu ya kiuchumi mikoa au kanda.

Serikali kuu inapaswa kuzipa baadhi ya local governments uhuru wa kimaamuzi, kiusimamizi na kiuratibu wa sera za kiuchumi za maeneo yao husika huku serikali kuu ikibaki muangalizi.

Tunahitaji kupitia upya sheria zetu za kikodi zina afya au bora liende.

Tusifikiri kuhusu kukusanya kodi nyingi kwa watu wachache bali kodi chache kwa watu wengi.

Sera zetu za kiuchumi zipo vipi au bora liende.

Nafikiri tuna mambo mengi ya kufikiri bila kuanza kuwazia kuhusu sijui uchumi wa kipebari mara kijamaa mara kikomunisti
 
Huo mfano uliotoa wewe ni mmoja ya mambo hayapaswi kuachiwa sekta binafsi kutekeleza. Serikali haipaswi kuona uvivu kujengea barabara raia wake ili kurahisisha shughuli za maendeleo.
Mkuu profit incentive ndio inafanya private sector kuwa serious. Mfano Road fund inatoa say billion 100 za lami ila sio tu kuna ufisadi mkubwa, urasimu na untimely completion sababu hakuna "hasara" serikali inapata with or without barabara kuisha mapema. Ila private sector ni lazima ikimbizane both in quality and speed ili barabara iishe haraka aingize pesa coz they have all to lose.
Mfano upo hivi serikali yaweza gharamia ujenzi wa miundombinu kama barabara/reli wa mabilioni ya pesa na pesa isiweze kurudi kwa haraka na kuacha madeni ila shughuli za kiuchumi zilizo rahisishwa au kuwezeshwa kupitia miundombinu hiyo zikawa na manufaa kwa maendeleo ya eneo husika.
Issue sio pesa kurudi ila hauwezi expect serikali ijenge kilometre 1000 za lami kila mwaka ila ingekua ni private sector ina maana unaweza pata wawekezaji 10 wakajenga km 100 za lami nchi nzima na wakawa wanatukata watumiaji sio serikali mpka pesa irudi. Kuliko serikali kubeba risk ya kujenga barabara zote say ichukur mkopo au isubiri bajeti 20 kujenga km 1000 za lami. Which is better?
Sekta muhimu kwa taifa hazipaswi kuachwa mikononi wa mwa watu binafsi zitageuka kuwa ghali na ushindani wa gharama za uendeshaji wakati jukumu namba moja la serikali ni kutoa hudua kwa raia kwa
Ndio maana nimesema serikali ni regulator kupitia Fair Competition Commission inazuia predatory pricing ama cartels za kuweka premium pricing. Pia kukiwepo na ushindani bei hushuka not kupanda. Mfano kipindi Air Tanzania, Precision na Fast jet zipo bei zilipanda? In fact ATCL ilikua ife maana hakuna angelipa bei juu ilihali kuna cheaper alternative ya Fast jet or Fly540!!
Sekta ya mawasiliano, miundombinu, nishati, afya hizi ni sekta muhimu ambazo hazipaswi kuwa ndani ya mikono michache ya watu binafsi ni ziwepo mikononi mwa mashirikiano kati ya serikali+watu binafsi.
Zipo chini ya serikali lakini zimeprove failure, mfano NIDA imefeli kabisa ila tender ya kuchapisha angepewa kampuni binafsi inayolipwa based on number ya ID mbona tungeshapata wote.
Pia malalamiko ya huduma mbovu, rushwa, vifo vya kizembe hospitali za serikali zipo kwa miaka 60 sasa kuangalia tu affordability kuliko service quality ndio hayo unalipa cheap ila kupona ni majaliwa ya Mungu. Same to shule za serikali ni cheap ila performance ni zero kabisa. Sasa why ukomae tu kuwa ni nyeti alafu matatizo ni kila siku?. Serikali inaweza regulate tu pricing na standards ila implementation zifanywe na hospital zenyewe. Yes it's gonna be expensive lakini effective na efficient. Mbona serikali ina fund hospitali za dini na huduma ni nzuri sana licha ya kwamba serikali pays billions? You know why? Maana ipo chini ya watu binafsi so they have all to lose kama huduma zikiwa mbovu watanyimwa pesa!!
 
Mkuu profit incentive ndio inafanya private sector kuwa serious. Mfano Road fund inatoa say billion 100 za lami ila sio tu kuna ufisadi mkubwa, urasimu na untimely completion sababu hakuna "hasara" serikali inapata with or without barabara kuisha mapema. Ila private sector ni lazima ikimbizane both in quality and speed ili barabara iishe haraka aingize pesa coz they have all to lose.

Issue sio pesa kurudi ila hauwezi expect serikali ijenge kilometre 1000 za lami kila mwaka ila ingekua ni private sector ina maana unaweza pata wawekezaji 10 wakajenga km 100 za lami nchi nzima na wakawa wanatukata watumiaji sio serikali mpka pesa irudi. Kuliko serikali kubeba risk ya kujenga barabara zote say ichukur mkopo au isubiri bajeti 20 kujenga km 1000 za lami. Which is better?

Ndio maana nimesema serikali ni regulator kupitia Fair Competition Commission inazuia predatory pricing ama cartels za kuweka premium pricing. Pia kukiwepo na ushindani bei hushuka not kupanda. Mfano kipindi Air Tanzania, Precision na Fast jet zipo bei zilipanda? In fact ATCL ilikua ife maana hakuna angelipa bei juu ilihali kuna cheaper alternative ya Fast jet or Fly540!!
Zipo chini ya serikali lakini zimeprove failure, mfano NIDA imefeli kabisa ila tender ya kuchapisha angepewa kampuni binafsi inayolipwa based on number ya ID mbona tungeshapata wote.
Pia malalamiko ya huduma mbovu, rushwa, vifo vya kizembe hospitali za serikali zipo kwa miaka 60 sasa kuangalia tu affordability kuliko service quality ndio hayo unalipa cheap ila kupona ni majaliwa ya Mungu. Same to shule za serikali ni cheap ila performance ni zero kabisa. Sasa why ukomae tu kuwa ni nyeti alafu matatizo ni kila siku?. Serikali inaweza regulate tu pricing na standards ila implementation zifanywe na hospital zenyewe. Yes it's gonna be expensive lakini effective na efficient. Mbona serikali ina fund hospitali za dini na huduma ni nzuri sana licha ya kwamba serikali pays billions? You know why? Maana ipo chini ya watu binafsi so they have all to lose kama huduma zikiwa mbovu watanyimwa pesa!!
Yes nakubaliana nawe kuwa usimamizi wa serikali ya Tanzania katika mambo mengi haufanyi vizuri hata katika hayo maeneo machache uliyosema.

Lakini kuhusu pia sekta binafsi nazo zimeonesha kushindwa mfano mawasiliano, afya, nishati sekta binafsi licha ya kupokea ruzuku za mabilioni toka serikali kuu zimeleta unafuu gani kwa Watanzania zaidi ya kuzidi kuwanyonga kila uchwao ?

Ni sekta ngapi binafsi katika hayo maeneo niliyo taja ni mabingwa wa huduma mbovu zisizo ridhisha licha ya kutoza gharama za juu ?
 
Inashangaza taifa letu lina bahari, mito mikubwa, ziwa Tanganyika limepakana na nchi kadhaa, ziwa Viktoria limepakana na nchi kadhaa na ni chanzo cha mto mkubwa, ziwa nyasa limepakana na nchi kadhaa.

Kwa nini hatuna maeneo maalumu ?

Sheria za kikodi za maeneo haya zinasemaje ?

Sera za kiuchumi kwa maeneo haya zipoje ?

Sera, sheria za makazi, shughuli za kiuchumi, kazi za hayo maeneo zipoje ?

Upi mpango mkakati wa muda mrefu wa serikali kuu kwa maeneo yote yaliyo mipakani ?
 
Mkuu tatizo ni uongozi tulionao..
Siku Mungu akitubariki kupata uongozi bora, Tanzania itakua kwa kasi ya ajabu sana.
Wanasema watu wanakuwa kama kiongozi wao alivyo. Kiongozi fisadi hupelekea kila mtu kuwa fisadi. Kiongozi mwadilifu na mwajibikaji, hupelekea raia wake kuwa waadilifu na wawajibikaji pia.
 
It's a suggestion, pure market economy with very limited government intervention is a way to go. Or rather serikali ibaki kama regulator na policy maker ila uchumi mzima uwe unaendeshwa na private sector. Hata chadema ndio sera yetu, market economy ambapo hata barabara za lami yanaweza jengwa na mtu binafsi then akatoza charges kwa muda fulani hela yake irudi.
Ukishaitaja tu serikali katika eneo lolote, hata huko ku 'regulate' unakokusema wewe, tayari dhana nzima ya 'pure' imekwisha katika.

Look, ifike mahali tuachane na hizi 'mentalility' za kizamani za nani mzuri nani mbaya. Haya hayatusaidii chochote sisi. Tunachotaka ni huduma nzuri, na kuwa huru kuamua sisi wenyewe (kama nchi) tunataka tufanye nini kwa manufaa yetu.
Hilo swala la serikali kujiondoa katika kila kitu, kwa kusema tu haiwezi kufanya chochote kwa ufanisi ni dhana nisiyokubaliana nayo kabisa.

Kama maana ya serikali ni hiyo, basi ijiondoe kabisa hata katika maisha ya watu kabisa; jambo ambalo haliwezekani popote.

Hizo unazo sema ni sera za CHADEMA; hujui kuwa hilo ni moja ya mambo yanayowafanya CHADEMA wasikubaliwe sana sehemu mbalimbali nchini? Sera hizo mara nyingi zimekuwa kama ni siri kubwa, hazielezwi kinagaubaga, matokeo yake yanakuwa kama ni hila za chama kuingiza maswala wasiyo yaelewa wananchi.
 
Mkuu, Kalamu!

Mchango wako wa Mada Husika ni mzuri sana! Mimi binafsi naunga mkono tuwe na "A Socialist Economy!
Tatizo hakuna chama kinacholenga huko. CCM, kama hawa wengineo wote hakuna anaye lenga kuelekea huko ingawaje CCM wamebaki na maneno tu kuhadaa watu huku wakifanya mambo tofauti kabisa.
 
Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.

Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.

Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!

Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.

Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Ww utakuwa ni mzee unayeamini kwenye ujamaa, lakini hakuna siasa ya kipuuzi kama ujamaa. Hata huu uzombie tulio nao kama ni nchi ni kutokana na siasa hiyo ya ujamaa.
 
Watu wengi wanamlaumu Nyerere na kuponda ujamaa wakidhani USA anauchukia ujamaa.
Ujamaa ni usoshalist ambao upo Israel ambao wana kibbutzim na Moshav.
Sweden ni wajamaa. Ujerumani ni wajamaa na ndio maana wana mpaka chama cha kijamaa (SDU cha akina Gerhard Shroder)
Japan ni wajamaa.

Na fuatilia mataifa yenye ujamaa, hakuna umasikini wala hakuna tajiri sana kama Elon Musk ila unashangaa taifa lenye uchumi mkubwa Ulaya ni wajamaa.
Hata timu kubwa ya kandanda kama Beyern Minchen inaendeshwa kijamaa.

Nyerere alikosa watu ambao walikuwa falsafa ya kujenga uchumi as kijamaa. Bahati mbaya alimpa Kawawa kuongoza jahazi wakati akiwa hajui model ya ujamaa inafanya vip kazi.
Japan ni wajamaa?
Kina Toshiba na Toyota ni wajamaa? Kina Rakuten?

Ujerumani ipi ya wajamaa? Hii hii ya kina Volkswagen? Sweden ya kina Volvo ndo unasema wajamaa?! Acha uongo wewe
 
Lakini kuhusu pia sekta binafsi nazo zimeonesha kushindwa mfano mawasiliano, afya, nishati sekta binafsi licha ya kupokea ruzuku za mabilioni toka serikali kuu zimeleta unafuu gani kwa Watanzania zaidi ya kuzidi kuwanyonga kila uchwao
Why una focus kwenye unafuu? Sisi tunaongelea UFANISI. Cheap is not always efficient or effective. Having said that, nakupa mfano TRA inapaswa ku audit MNCs zaidi ya 300 kwenye eneo la transfer pricing CAG anasema ni 10% ya MNCs hukaguliwa. Cha ajabu private sector kampuni kama KPMG au Deloitte n.k zinaweza audit hizo kampuni zote!! Ndio unajiuliza why waweze ila TRA ishindwe? Kwanini? Sababu serikali hawana profit incentive wala shareholders wa kuwashika koo!!

Kuhusu Nishati bado haijawahi kuwa supplied na kampuni binafsi otherwise mgao ungebaki historia maana competition ingekua kubwa so kampuni A ikifeli kwenye distribution watu wanahamia kampuni B.
Ni sekta ngapi binafsi katika hayo maeneo niliyo taja ni mabingwa wa huduma mbovu zisizo ridhisha licha ya kutoza gharama za juu ?
Yeah zipo kampuni mbovu hata sekta binafsi ila sio nyingi as compared to sekta ya umma zilizo mbovu. Katika kampuni zaidi ya 100 za serikali zinazo underperform ni zaidi ya 80!! Na hili hata JPM alisema hazikuwahi toa gawio tokea zianzishwe.
 
Back
Top Bottom